Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa elimu ya umuhimu wa maji na utunzaji miundombinu ya maji kwa wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya sekondari Chalinze Wilaya ya bagamoyo Mkoani Pwani
Lengo la elimu hii ilikuwa ni kuwaelemisha wanafunzi umuhimu wa maji na utunzaji wa miundombinu ya maji ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa huduma hii muhimu katika jamii.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo, Afisa Mawasiliano kutoka DAWASA, Ndugu Prisca Makenya amesema maji ni rasilimali muhimu ambayo inahitajika kwa viumbe hai ikiwepo binadamu, mimea na wanyama, hivyo kuna ulazima wa kuyatunza na kuhakikisha yanalindwa ili yaweze kufaa kwa matumizi ya kila siku.
"Utunzaji miundombinu ya maji ni muhimu kwani unapunguza gharama zinazojitokeza wakati wa uharibifu, unasaidia upatikanaji majisafi na ya uhakika.
Miundombinu ya maji inayotumiwa na DAWASA ni pamoja na mitambo ya uzalishaji na Uzalishaji maji, mabomba, pumpu za kusukuma maji, dira za maji na viungio vyake," amesema Ndugu, Makenya.
Ndugu Makenya amesema klabu za mazingira mashuleni zimeanzishwa kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo katika masuala ya maji na usafi wa mazingira ili wanafunzi hao wakawe chachu na mabalozi wa mabadiliko kwa jamii wanazotoka.
Wanafunzi wamejifunza njia mbalimbali ovu zinazofanywa na wanachi wasiowaaminifu kwenye miundombinu ya DAWASA ikiwa ni pamoja na kukata mabomba na wizi wa mita za maji.
Kwa upande wake, Mwalimu anayesimamia klabu ya mazingira Chalinze Sekondari, Prisca Chamoto ameishukuru Mamlaka kwa kutoa elimu hii muhimu kwa wanafunzi wa shule hiyo inayowajengea uelewa wa namma nzuri ya kutunza miundombinu ya maji na hatua za kuchukua punde wanapoona wananchi wasio waaminifu wanaoharibu miundombinu.
Amewataka wanafunzi waliopatiwa elimu hiyo kuwa mabalozi wazuri wa huduma za maji katika jamii yao.
Mwanafunzi, Ismail Issa aliyepata elimu hiyo, ameishukuru Mamlaka kwa kuwaelimisha na kuwasaidia kujua umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya maji na hatua za kuchukua pindi wanapoona uharibifu unapotokea, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa DAWASA kupitia namba 181 ya huduma kwa wateja.
"Kwa niaba ya wenzangu, tunaahidi tutakuwa mabalozi wazuri kwa jamii kuhakikisha tunalinda miundombinu ya maji kwa manufaa ya vizazi vijavyo," amesema Ismail
Klabu ya Mazingira Shule ya Chalinze ni moja ya klabu 12 za mazingira ambazo Mamlaka inazisimamia katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ili kuwajengea uwezo wa kutambua shughuli mbalimbali za Mamlaka kuhusu majisafi na usafi wa mazingira na kwenda kuwa mabalozi wazuri katika jamii.