masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Kuna kila dalili kwamba Dayosisi ya Konde KKKT inaweza kutawanyika na kubaki vipande vipande.
Ibilisi ameota mizizi ndani ya Konde, tena Ibilisi mwenye mapembe yake ya kiburi, hasira, ukaidi, utenganisho, fitna na kiujumla kupotea kabisa kwa upendo.
Kwa wengi tuliodhani ujio wa Dr Mwaikali ambaye ni kijana,kwa maono mapana ilikuwa ni heri kwa Kanisa.
Lakini hii miaka yake minne/mitano imekuwa ya ugomvi, kutoelewana na tabia zote zinazomwinua Ibilisi.
Wakristo wa Dayosisi hii tuombe sana.
Baada ya kikao cha Baba Askofu Shoo, Mkuu wa Kanisa KKKT cha tarehe 22/2/2022, huko Kyela na hata Mbeya Ruanda wafuasi wa Mwaikali wametoa matamko ya kumuunga mkono Askofu aliyeenguliwa na Mkutano Mkuu wa Dayosisi.
Hata hivyo Ibilisi hawezi kushinda mbele ya Mungu, maana atashindwa kama alivyoshindwa kale.
Tusali sana kuombea Dayosisi ya Konde KKKT.