DC Arusha, Kenani Kihongosi: Tutafundishana uzalendo mpaka tutaelewana vizuri

Wahuni wame hack acc yako nini?

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nilisikiliza utetezi wa DC huyu juu ya kitendo alichofanya nikasikitika sana.

Mwanzo mwisho DC anang'ang'ania uzalendo uzalendo uzalendo!

DC hajui kuwa anachotuhumiwa ni kujichukulia sheria mkononi na kupuuza utawala wa sheria.

Mob justice inayotumika kwa wezi, vibaka, majambazi inatokana na tabia ya kupuuza haki ndogo ndogo za raia.

Hakuna anayeunga mkono tabia mbaya za kuharibu mali za umma wala za mtu binafsi, bali kinachosisitizwa ni utawala wa sheria.
 
Mzee baba mbona kimya
Dc huyo mchapakazi sanaaaaa
Awamu hii inataka watu kama hao

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Hivi adhabu ya kuhujumu uchumi huwa ni viboko vya makalioni?Vinatakiwa vingapi?Ukoloni sasa ni rasmi!
 
Ujinga kabisa. Jitu linavunja sheria halafu unalisifia kuwa ni uzalendo? Uzalendo unapatikana kwa viboko? Huyo DC ni mwehu tu hakuna sheria inayo mruhusu kufanya hivyo. Mahakama itafanya kazi gani?
 
Huyu dogo anavimba kichwa anajibaribia anafikili rais ni Jpm tu
 
Wakati mwingine yanakuja maswali bila majibu.
Je katika kadhia ila ingetokea kijana mmoja akampiga na kumuumiza kiongozi aliyekuwa akitoa adhabu kwa kujihami asipigwe fimbo. Sheria ingempa nani haki?
Je kuna uhalali wa kumhukumu mtu kabla ya mamlaka husika kupatikana na hatia?
Kwa adhabu ile ya viboko wahusuka wakipatikana na hatia watatumiakia tena adhabu ? Au adhabu ya mwanzo ya fimbo inatosha?
Je ikitokea wakafikishwa mahakamani na ikatokea wakakosekana na hatia je adhabu ile ya fimbo itakuwa reversed vipi?
Hayo ndiyo baadhi ya maswali niliyonayo.
 
Akili za kindezi kabisa


Hivi adhabu ya kuhujumu uchumi huwa ni viboko vya makalioni?Vinatakiwa vingapi?Ukoloni sasa ni rasm
 

Attachments

  • VID-20201218-WA0033.mp4
    18.5 MB
Mkuu tatizo lako unajibu ukiwa na mihemko ya kisiasa, si kila mtu anaweka mawazo yake hapa kwa kulenga siasa angalia uhalisia wa maisha. Nimekuwa mwanafunzi muda mrefu najua ujinga wa wanafunzi ndiyo maana nasema bila woga achapwe kiboko anapokosea haijalishi anaadhibiwa na nani..
 
Raia hafanywi mzalendo kwa kuchapwa viboko.
 
Huwezi kumfundiaha mtu uzalendo Uzalendo ni moyo
 
Wewe ndo Una mihemko, ya kimila mkuu! Jamaa ameelezea fact man amequote vifungu vya sheria, sasa Wewe unatumia reference ya utukutu wako ku analyze mambo! Labda Unaweza usikumbuke, Lakini miaka kadhaa iliyo pita kuna mwalimu alimchapa mtoto, mtoto akafa! Kilicho semwa na jamaa ni; fimbo kwa wanafunzi ni kwa utaratibu maalumu, kama alivyo ainisha!
 
Tuache mahakama zifanye kazi zake tunainbilia kazi za mahakama.Haki inapatika mahakamani na si kwa kiongozi
 
Mshamba tu huyu dogo
 
Uzuri wa mwenye tatizo la afya ya akili hakawii kurusha mawe hata kwa wale wanaomshangilia. Madhara ya kutoheshimu utu na kuona ni jambo la kawaida na ustaarabu katika kudhalilishana miongoni mwa watumishi wa umma. Zamani watu waliamini katika utumishi wa umma sasa ni kinyume chake. Waliomo wanatamani kutoka na walio nje hawatamani kuingia... matokeo yake wasio na pa kwenda ndio wanatamani kuwamo ili wagange njaa. Je huyo mtukufu DC akifanya madudu au hao waliochapwa wakiteuliwa kuwa juu yake itakuwaje?
Ni suala la zamu tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…