DC Arusha mjini avunja ukimya kwa Gambo

DC Arusha mjini avunja ukimya kwa Gambo

Arusha. Mkuu wa wilaya ya Arusha, Felisian Mtehengerwa amemtaka Mbunge wa jimbo lake Mrisho Gambo kutekeleza wajibu wake ndani ya halmashauri kuliko kubeba ajenda za ubadhilifu ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Mtahengerwa amesema hayo leo April 19,2023 wakati akizungumza na waandishi wahabari juu ya msimamo wake kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Gambo bungeni hivi karibuni akielezea ubadhilifu wa fedha za umma katika halmashauri ya jiji la Arusha na serikali.
"Gambo ifikie mahali aache siasa za maji taka maana kutuhumu viongozi kwa ufisadi wakati yeye ni sehemu ya viongozi wanaosimamia utekelezaji wa mipango ya jiji la Arusha ni kutafuta pa kutokea na huruma ya wananchi wakati yeye mwenyewe ni mmojawapo" amesema Mtahengerwa
"Gambo anaonyesha wazi hajui wajibu wake maana anasahau kuwa halmashauri inaundwa na madiwani na mbunge hivyo anapoona mambo hayaendi vizuri wangekuwa wakwanza kuzuia na kuchukua hatua za awali lakini matokeo yake anakubali utekelezaji ufanyike halafu baadae anaenda kuukosoa, awajibike ndani kwanza kwa kukataa isifanyike"ameongeza
Pia, amesema wakati mambo hayo yanatokea miaka ya nyuma ambayo pia yeye (Gambo) ni mmoja wa wajumbe wakuu hivyo anafaa kuwajibika maana ni sehemu ya mpango huo.
"Sisi kama wilaya tunawajibu wa kuingilia pale tunapoona akili za halmashauri zimefikia ukomo, mambo hayaendi, nilipoingia madarakani nilizungukia miradi yote na kuwaita madiwani wote na kutoa maelekezo yangu, ninachoshangaa yale yaliyowahi kuchukuliwa hatua bado anabeba Kama ajenda mpya na kuimba kila kukicha badala ya kuwajibika hivyo nimtake arudi jimboni tuchape kazi aache utoto wa mashtaka,”amesema.
Hivi karibuni Gambo akiwa bungeni dodoma alieleza mambo mengi ya ufisadi katika jiji la Arusha huku akidai changamoto kubwa ya ubadhilifu na usimamizi mbovu wa fedha za halmashauri.
Alitolea mfano baadhi ya tuhuma ukiwemo ujenzi wa jengo la utawala lenye urefu wa gorofa sita, na kusema halmashauri imetafuta fundi mjenzi akidai ni rafiki yao bila kutangaza tenda, taratibu za manunuzi hazijafuatwa na kumpatia kiasi cha fedha Sh199.7 milioni na kununua vifaa vya Sh132 milioni ambavyo havijafika eneo la mradi.
"Ziada ya nondo kiasi cha tani 6.48 zenye thamani ya Sh17 milioni pia waliongeza malipo ya sh21 milioni kwa fundi yanayotokana na uzembe wa wataalamu wetu, pia kumekuwepo na risiti feki za EFD zenye thamani ya Sh699.9 milioni,”alituhumu Gambo
Aidha sio mara ya kwanza Gambo kutoa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika halmashauri hiyo kwani mapema Mei, 2022 alitoa tuhuma hizo mbele ya waziri mkuu Kasim Majaliwa hali iliyopelekea kusimamishwa kazi watumishi sita wa jiji la Arusha akiwemo aliyekuwa mkurugenzi Dk John Pima.

MWANANCHI
Ushauri wa bure kwa Bw. DC Arusha. Huko tulikotoka, kabla nchi hii haijapoteza dira kisiasa na kiuongozi, ilikuwa ni utovu wa nidhamu kujibizana na kiongozi wa kuchaguliwa hadharani na kwenye vyombo vya habari. Kiongozi wa kuchaguliwa ni alama ya wananchi ambao ndiyo mamlaka ya juu kabisa katika nchi. Mahali pekee pa kujibizana na kiongozi wa kuchaguliwa, husuasn Mbunge ni kwenye vikao rasmi. Na hata huko kwenye vikao rasmi, DC akiwa mtumishi wa umma anapaswa kujibizana na Mheshimiwa Mbunge kwa staha na heshima zote. Ipo lugha ya kumjibu kiongozi wa kuchaguliwa bila kumdhalilisha hata kama amekosea au hata kama kiongozi mwenyewe ni Mhe. Gambo! Kumkejeli na kumdhalilisha Mbunge ni dharau kubwa sana kwa wananchi waliomchagua na mtumishi wa umma anayefanya hivyo hajui nafasi yake. Hii tabia mbaya ya kuwavunjia heshima viongozi wa kuchaguliwa ni kielelezo dhahiri cha jinsi ambavyo kama taifa tumepoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni. Chimbuko lake ni pamoja fikra potofu na ya kijima iliyoshika kasi miaka hii kuwa siasa za ushindani ni uadui. Sababu nyingine ile dhana potofu na ya kijinga ya hivi karibuni pia kuwa eti mhimili wa serikali unayo mizizi iliyojichimbia chini zaidi! Kwa ujinga huo tulianza kuona viongozi wa kuchaguliwa wakiwemo hata wale wa chama chenye serikali wakitendewa kinyume na matarajio ya raia, wakati mwingine kwa sababu tu ya kutofautiana na mtazamo na wakuu wa serikali. Kwa wale wa vyama vya ushindani hali ikawa mbaya zaidi kwani kazi kubwa ya wakuu wa serikali ikawa ni kuwadhalilisha wabunge wa upinzani hadharani ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuua ushindani wa kisiasa. Lakini kama alivyopata kusema kiongozi mmoja wa upinzani, baada ya kumalizana na wapinzani sasa ni zamu ya ndani ya nyumba moja.
 
Arusha. Mkuu wa wilaya ya Arusha, Felisian Mtehengerwa amemtaka Mbunge wa jimbo lake Mrisho Gambo kutekeleza wajibu wake ndani ya halmashauri kuliko kubeba ajenda za ubadhilifu ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Mtahengerwa amesema hayo leo April 19,2023 wakati akizungumza na waandishi wahabari juu ya msimamo wake kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Gambo bungeni hivi karibuni akielezea ubadhilifu wa fedha za umma katika halmashauri ya jiji la Arusha na serikali.
"Gambo ifikie mahali aache siasa za maji taka maana kutuhumu viongozi kwa ufisadi wakati yeye ni sehemu ya viongozi wanaosimamia utekelezaji wa mipango ya jiji la Arusha ni kutafuta pa kutokea na huruma ya wananchi wakati yeye mwenyewe ni mmojawapo" amesema Mtahengerwa
"Gambo anaonyesha wazi hajui wajibu wake maana anasahau kuwa halmashauri inaundwa na madiwani na mbunge hivyo anapoona mambo hayaendi vizuri wangekuwa wakwanza kuzuia na kuchukua hatua za awali lakini matokeo yake anakubali utekelezaji ufanyike halafu baadae anaenda kuukosoa, awajibike ndani kwanza kwa kukataa isifanyike"ameongeza
Pia, amesema wakati mambo hayo yanatokea miaka ya nyuma ambayo pia yeye (Gambo) ni mmoja wa wajumbe wakuu hivyo anafaa kuwajibika maana ni sehemu ya mpango huo.
"Sisi kama wilaya tunawajibu wa kuingilia pale tunapoona akili za halmashauri zimefikia ukomo, mambo hayaendi, nilipoingia madarakani nilizungukia miradi yote na kuwaita madiwani wote na kutoa maelekezo yangu, ninachoshangaa yale yaliyowahi kuchukuliwa hatua bado anabeba Kama ajenda mpya na kuimba kila kukicha badala ya kuwajibika hivyo nimtake arudi jimboni tuchape kazi aache utoto wa mashtaka,”amesema.
Hivi karibuni Gambo akiwa bungeni dodoma alieleza mambo mengi ya ufisadi katika jiji la Arusha huku akidai changamoto kubwa ya ubadhilifu na usimamizi mbovu wa fedha za halmashauri.
Alitolea mfano baadhi ya tuhuma ukiwemo ujenzi wa jengo la utawala lenye urefu wa gorofa sita, na kusema halmashauri imetafuta fundi mjenzi akidai ni rafiki yao bila kutangaza tenda, taratibu za manunuzi hazijafuatwa na kumpatia kiasi cha fedha Sh199.7 milioni na kununua vifaa vya Sh132 milioni ambavyo havijafika eneo la mradi.
"Ziada ya nondo kiasi cha tani 6.48 zenye thamani ya Sh17 milioni pia waliongeza malipo ya sh21 milioni kwa fundi yanayotokana na uzembe wa wataalamu wetu, pia kumekuwepo na risiti feki za EFD zenye thamani ya Sh699.9 milioni,”alituhumu Gambo
Aidha sio mara ya kwanza Gambo kutoa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika halmashauri hiyo kwani mapema Mei, 2022 alitoa tuhuma hizo mbele ya waziri mkuu Kasim Majaliwa hali iliyopelekea kusimamishwa kazi watumishi sita wa jiji la Arusha akiwemo aliyekuwa mkurugenzi Dk John Pima.

MWANANCHI
Ma DC Huwa ni wapuuzi sana hapo kwa kuwa anamegewa ndio anajisemesha hivyo..

Kwamba mbunge asiongelee ubadhirifu Kwa sababu ipi hasa?

Ndio maana cdm wanataka hivi vyeo kufutwa wamekuwa ni watu wa migogoro sana.
 
Gambo atakuwa na kinyongo sana baada ya madili yake mengi kufeli!
NB: Mivutano ya viongozi na Watendaji pale Arusha ni kikwazo kwa maendeleo. Miradi mingi haifikii malengo yake kwa sababu ya hiyo mivutano ya maslahi binafsi!
 
Uzuri aliyempa ubunge Gambo hayupo tena.
 
Arusha. Mkuu wa wilaya ya Arusha, Felisian Mtehengerwa amemtaka Mbunge wa jimbo lake Mrisho Gambo kutekeleza wajibu wake ndani ya halmashauri kuliko kubeba ajenda za ubadhilifu ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Mtahengerwa amesema hayo leo April 19,2023 wakati akizungumza na waandishi wahabari juu ya msimamo wake kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Gambo bungeni hivi karibuni akielezea ubadhilifu wa fedha za umma katika halmashauri ya jiji la Arusha na serikali.
"Gambo ifikie mahali aache siasa za maji taka maana kutuhumu viongozi kwa ufisadi wakati yeye ni sehemu ya viongozi wanaosimamia utekelezaji wa mipango ya jiji la Arusha ni kutafuta pa kutokea na huruma ya wananchi wakati yeye mwenyewe ni mmojawapo" amesema Mtahengerwa
"Gambo anaonyesha wazi hajui wajibu wake maana anasahau kuwa halmashauri inaundwa na madiwani na mbunge hivyo anapoona mambo hayaendi vizuri wangekuwa wakwanza kuzuia na kuchukua hatua za awali lakini matokeo yake anakubali utekelezaji ufanyike halafu baadae anaenda kuukosoa, awajibike ndani kwanza kwa kukataa isifanyike"ameongeza
Pia, amesema wakati mambo hayo yanatokea miaka ya nyuma ambayo pia yeye (Gambo) ni mmoja wa wajumbe wakuu hivyo anafaa kuwajibika maana ni sehemu ya mpango huo.
"Sisi kama wilaya tunawajibu wa kuingilia pale tunapoona akili za halmashauri zimefikia ukomo, mambo hayaendi, nilipoingia madarakani nilizungukia miradi yote na kuwaita madiwani wote na kutoa maelekezo yangu, ninachoshangaa yale yaliyowahi kuchukuliwa hatua bado anabeba Kama ajenda mpya na kuimba kila kukicha badala ya kuwajibika hivyo nimtake arudi jimboni tuchape kazi aache utoto wa mashtaka,”amesema.
Hivi karibuni Gambo akiwa bungeni dodoma alieleza mambo mengi ya ufisadi katika jiji la Arusha huku akidai changamoto kubwa ya ubadhilifu na usimamizi mbovu wa fedha za halmashauri.
Alitolea mfano baadhi ya tuhuma ukiwemo ujenzi wa jengo la utawala lenye urefu wa gorofa sita, na kusema halmashauri imetafuta fundi mjenzi akidai ni rafiki yao bila kutangaza tenda, taratibu za manunuzi hazijafuatwa na kumpatia kiasi cha fedha Sh199.7 milioni na kununua vifaa vya Sh132 milioni ambavyo havijafika eneo la mradi.
"Ziada ya nondo kiasi cha tani 6.48 zenye thamani ya Sh17 milioni pia waliongeza malipo ya sh21 milioni kwa fundi yanayotokana na uzembe wa wataalamu wetu, pia kumekuwepo na risiti feki za EFD zenye thamani ya Sh699.9 milioni,”alituhumu Gambo
Aidha sio mara ya kwanza Gambo kutoa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika halmashauri hiyo kwani mapema Mei, 2022 alitoa tuhuma hizo mbele ya waziri mkuu Kasim Majaliwa hali iliyopelekea kusimamishwa kazi watumishi sita wa jiji la Arusha akiwemo aliyekuwa mkurugenzi Dk John Pima.

MWANANCHI
Kazi ya kukaimu anataka iwe ya kudumu mwenyewe Jimbo tayari yupo
 
PONGEZI kwako DC kumwambia ukweli Mbunge huyo mbunge ana Majungu sana
 
Huyu DC aandike barua kwa spika ya kumshitaki Gambo kwa tuhuma alizoziongea bungeni ili spika amtake Gambo kumpa vielelezo na ushahidi.

HGambo asilitumie vibaya bunge ili kuchagua maDC na maDED
 
Katibu tarafa aliyepanda cheo nakuwa mkuu wa wilaya ni tatizo,angetafutiwa wilaya nyingine,kwamaana amekuwa sehemu ya siasa chafu za jiji la Arusha.
 
Back
Top Bottom