DC Arusha mjini avunja ukimya kwa Gambo

Ushauri wa bure kwa Bw. DC Arusha. Huko tulikotoka, kabla nchi hii haijapoteza dira kisiasa na kiuongozi, ilikuwa ni utovu wa nidhamu kujibizana na kiongozi wa kuchaguliwa hadharani na kwenye vyombo vya habari. Kiongozi wa kuchaguliwa ni alama ya wananchi ambao ndiyo mamlaka ya juu kabisa katika nchi. Mahali pekee pa kujibizana na kiongozi wa kuchaguliwa, husuasn Mbunge ni kwenye vikao rasmi. Na hata huko kwenye vikao rasmi, DC akiwa mtumishi wa umma anapaswa kujibizana na Mheshimiwa Mbunge kwa staha na heshima zote. Ipo lugha ya kumjibu kiongozi wa kuchaguliwa bila kumdhalilisha hata kama amekosea au hata kama kiongozi mwenyewe ni Mhe. Gambo! Kumkejeli na kumdhalilisha Mbunge ni dharau kubwa sana kwa wananchi waliomchagua na mtumishi wa umma anayefanya hivyo hajui nafasi yake. Hii tabia mbaya ya kuwavunjia heshima viongozi wa kuchaguliwa ni kielelezo dhahiri cha jinsi ambavyo kama taifa tumepoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni. Chimbuko lake ni pamoja fikra potofu na ya kijima iliyoshika kasi miaka hii kuwa siasa za ushindani ni uadui. Sababu nyingine ile dhana potofu na ya kijinga ya hivi karibuni pia kuwa eti mhimili wa serikali unayo mizizi iliyojichimbia chini zaidi! Kwa ujinga huo tulianza kuona viongozi wa kuchaguliwa wakiwemo hata wale wa chama chenye serikali wakitendewa kinyume na matarajio ya raia, wakati mwingine kwa sababu tu ya kutofautiana na mtazamo na wakuu wa serikali. Kwa wale wa vyama vya ushindani hali ikawa mbaya zaidi kwani kazi kubwa ya wakuu wa serikali ikawa ni kuwadhalilisha wabunge wa upinzani hadharani ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuua ushindani wa kisiasa. Lakini kama alivyopata kusema kiongozi mmoja wa upinzani, baada ya kumalizana na wapinzani sasa ni zamu ya ndani ya nyumba moja.
 
Ma DC Huwa ni wapuuzi sana hapo kwa kuwa anamegewa ndio anajisemesha hivyo..

Kwamba mbunge asiongelee ubadhirifu Kwa sababu ipi hasa?

Ndio maana cdm wanataka hivi vyeo kufutwa wamekuwa ni watu wa migogoro sana.
 
Gambo atakuwa na kinyongo sana baada ya madili yake mengi kufeli!
NB: Mivutano ya viongozi na Watendaji pale Arusha ni kikwazo kwa maendeleo. Miradi mingi haifikii malengo yake kwa sababu ya hiyo mivutano ya maslahi binafsi!
 
Uzuri aliyempa ubunge Gambo hayupo tena.
 
Kazi ya kukaimu anataka iwe ya kudumu mwenyewe Jimbo tayari yupo
 
PONGEZI kwako DC kumwambia ukweli Mbunge huyo mbunge ana Majungu sana
 
Huyu DC aandike barua kwa spika ya kumshitaki Gambo kwa tuhuma alizoziongea bungeni ili spika amtake Gambo kumpa vielelezo na ushahidi.

HGambo asilitumie vibaya bunge ili kuchagua maDC na maDED
 
Katibu tarafa aliyepanda cheo nakuwa mkuu wa wilaya ni tatizo,angetafutiwa wilaya nyingine,kwamaana amekuwa sehemu ya siasa chafu za jiji la Arusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…