DC Gowele ataka uangalifu zoezi la fidia TSF-North Mara

DC Gowele ataka uangalifu zoezi la fidia TSF-North Mara

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
er (4).jpg

DC GOWELE ATAKA UANGALIFU ZOEZI LA FIDIA TSF-NORTH MARA

TARIME

Mkuu wa Wilaya ya Tarima mkoani Mara Mhe. Meja. Edward Gowele, amewaagiza viongozi wanaosimamia zoezi la uthamini wa fidia eneo la mradi wa ujenzi wa Bwawa la TSF-North Mara kuwa makini dhidi ya wananchi wanaojiingiza katika maeneo yanayoguswa na mradi kwa lengo la kujipatia fidia.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuzuia matumizi ya nyaraka au mikataba isiyo halali katika mchakato huo, akieleza kuwa vitendo hivyo vinaweza kusababisha migogoro sambamba na kuwaingiza wahusika kwenye matatizo ya kisheria.

Mhe. Meja. Edward Gowele, ametoa kauli hiyo Agosti 24, 2026 wilayani Tarime alipokutana na viongozi na wadau kujadili zoezi la uhamasishaji wa wananchi wanaoguswa na Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la (TSF) katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara mkoani Mara.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya ya Tarime, viongozi hao wanapaswa kuhakikisha kwamba, mchakato wa uthamini na fidia unaendeshwa kwa kuzingatia sheria, haki na uwazi.

Amesisitiza kuwa, viongozi hawapaswi kushiriki katika vitendo vya udanganyifu au dhuluma, bali wanapaswa kuwa sehemu ya kuhakikisha mchakato huo unalinda haki na maslahi ya wananchi pamoja na mwekezaji wa mradi huo kwa kuzingatia sheria.

Kwa upande mwingine, kikao hicho kimejadili umuhimu wa wananchi kupewa taarifa sahihi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali, hususan katika masuala ya uthamini, fidia na maeneo yote yanayoguswa na mradi.

Kikao hicho kimekuwa sehemu ya uratibu wa viongozi na wataalamu katika kuhakikisha zoezi la uthamini na hatua zinazofuata za fidia kwa wananchi wanaoguswa na Mradi wa North Mara zinafanyika kwa uwazi, uadilifu na kwa kuzingatia sheria.
 
Back
Top Bottom