Kwahiyo "dakika 10 tu" umemaanisha nini? Unaona dkk 10 ni muda mfupi sana? Ndio maana waafrika tuko nyuma sana, hatujui thamani ya muda. Na huyo ni DED ambaye ana gari na dereva. Tujifunze kuthamini muda.
Siku moja dada mmoja alienda ofisi fulani kwa bodaboda, kabla hajaingia ofisini akamwambia jamaa amsubiri dkk chache warudi nae, dada kakaa humo zaidi ya dkk 20. Alivyotoka jamaa akamwambia naomba kwanza sh 2,000 ya kuniweka hapa kabla hatujaondoka. Dada akakataa likazuka zogo jamaa kidogo amshushie dada kichapo baadhi ya watu wakaja pale kuamua na ikaonekana dada ana makosa msamaria fulani akatoa ile 2,000
Na maofisini ndio kuna ujinga zaidi, yani unaenda kwa ajili ya kuhamisha mtoto unaambiwa subiri, unakaa huko masaa kadhaa watu wanapiga zao story tu. Ukiingia tena ofisini jamaa anachukua fomu zako anasaini anakwambia hapa tayari nenda mkoani. Unajiuliza yani kumbe ilikuwa kusaini tu?
Pamoja na ukweli kuwa viongozi lazima waheshimiane lakini pia hata huyo DED kwa kuchelewa maana yake hakuwaheshimu DC na RC
Sent using
Jamii Forums mobile app