DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Wamewala wengine wamekwisha sasa ni kulana wao kwa wao tu. Baada ya kumalizana watahamia kwa wapiga kura wao.
Muda ndio mwalimu sahihi kabisa ktk hili wadau


Kwamba Jerry Muro nae ni mmoja wao??.

Hakuna, aka CCM, hakafahamiki. He is not one of them. He is just being used.
Soon akiisha utamu/ matumizi,jalalani ndio itakuwa sehemu yake
 
Ila na huyo mwenye PHd analo la kujifunza toka hapo, mtu umesoma na una malengo yako uwe msomi ulobobea uwe profesa, from no where unateuliwa tu kijingajinga na wewe unakubali,tena anaekuteua anajinasibu ni kichaa na wengi mnajua bado mnakubali kuteuliwa.Basi mkubali na kutukanwa na mabashite yake.Uprofesa sahauni.
Kwa taarifa ni kuwa waraka umepelekwa kwenye vyuo vyote vya umma kuwa mwanataaluma yoyote aliyeteuliwa na jiwe,akishindwa huko alikopelekwa basi asipokelewe pindi atakapoomba kurudi baada ya kutumbuliwa alikoteuliwa.
Kazi mnayo
🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️
 
Dah ila kwamazingira yanavyoonesha jamaa anayefokewa ajachukulia serious anatabasamu nakumdharua jery muro, na RC gambo anaonesha kabisa ajafurahia kitendo hicho cha Jerry muro
 
Kwahiyo "dakika 10 tu" umemaanisha nini? Unaona dkk 10 ni muda mfupi sana? Ndio maana waafrika tuko nyuma sana, hatujui thamani ya muda. Na huyo ni DED ambaye ana gari na dereva. Tujifunze kuthamini muda.

Siku moja dada mmoja alienda ofisi fulani kwa bodaboda, kabla hajaingia ofisini akamwambia jamaa amsubiri dkk chache warudi nae, dada kakaa humo zaidi ya dkk 20. Alivyotoka jamaa akamwambia naomba kwanza sh 2,000 ya kuniweka hapa kabla hatujaondoka. Dada akakataa likazuka zogo jamaa kidogo amshushie dada kichapo baadhi ya watu wakaja pale kuamua na ikaonekana dada ana makosa msamaria fulani akatoa ile 2,000

Na maofisini ndio kuna ujinga zaidi, yani unaenda kwa ajili ya kuhamisha mtoto unaambiwa subiri, unakaa huko masaa kadhaa watu wanapiga zao story tu. Ukiingia tena ofisini jamaa anachukua fomu zako anasaini anakwambia hapa tayari nenda mkoani. Unajiuliza yani kumbe ilikuwa kusaini tu?

Pamoja na ukweli kuwa viongozi lazima waheshimiane lakini pia hata huyo DED kwa kuchelewa maana yake hakuwaheshimu DC na RC

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nimeona umezungumza maoni yako ambayo kiasi kikubwa uko sahihi, Ila kabla ya kumdhalilisha mtu kwenye umma lazima uwe na uhakika wa kile kilichomfanya yeye kuchelewa hapo alipo.Labda kwa kuzungumza ukweli ninaoufahamu juu ya tukio kwa sababu mimi naishi na huyu mkurugenzi kwake ila pia siwezi kuzungumza kwa kutetea upande wowote lakini nitazungumza namna stori ilivyokuwa na dr alivyofika nyumbani alivyotuambia nini kilitokea kabla ya kuenea mitandaoni.Ilikuwa ni juzi siku ya Jumanne usiku wakati mkurugenzi anarudi nyumbani alitukuta tumekaa sebuleni tunaangalia filamu ya marehemu Steven Kanumba dar 2 lagos chanel ya St swahili, alivyofika baada ya kumsalimia alikuwa tofauti na tulivyomzoea yaani hakuwa na furaha kuna simu ikawa imeingia ya kiongozi mmoja hivi wa serikali akamuuliza mkutano wenu umeendaje, akwambia haukuwa vizuri kulikuwa na tatizo baada ya kusikia hivyo ilibidi kupunguza sauti ya tv ili kusikiliza kilichotokea baada ya kuongea na simu akaanza kutuelezea ilivyokuwa.
Kwa kifupi ilikuwa hivi...... Asubuhi ya Jumanne viongozi hawa yaani Dc, Rc, Rpc, Ded na wengine walikuwa wamepanga kwenda ziara nahisi ilikuwa Arumeru hivyo wakati wanajiandaa kuondoka pale ofisini Mkurugenzi akawa amesahau baadhi ya documents ofisini hivyo akaomba kuzichukua haraka ili waondoke wakati anachukua documents hizo, akatoka nje akakuta msafara umeshaondoka ikiwepo gari ya King'ora ambayo hufanya gari na watu barabarani kupisha msafara hivyo basi akapanda kwenye gari lake na kuondoka ili kuwahi,Hivyo basi kutoka ofisini Sekei hadi kwenye mkutano Arumeru kulikuwa na foleni sana njiani pia Magari na watu hawa kupisha gari ya Mkurugenzi kwa sababu hakukuwa na gari ya king'ora kuonesha kuwa anawahi sehemu.
Baada ya purukushani hizo Mkurugenzi alifanikiwa kufika akiwa amechelewa kati ya dakika tano hadi kumi kwa hiyo kabla hajaeleza kitu chochote ndio akakutana na fedheha ya namna hii.Hivyo basi ningependa kushauri mtu yoyote kabla ya kutoa hukumu au kumuona mtu .. amekosea ni bora kwanza kusikiliza nini kimesababisha tatizo. kwa hiyo kwa tukio hili la Jumanne mheshimiwa Jerry Muro alikuwa akijua kabisa mkurugenzi amechelewa kwa sababu walimuacha bila kumpa taarifa wakati walikuwa pamoja na alikuwa anachukua documents ambazo ni mhimu kwa ajili ya mkutano wa siku ile hivyo inaweza kuwa Dc alifanya hivyo aidha kwa kupanga au bila kufikiria.
 
upuuzi ni Tabia
mpuuzi ni mtu mwenye tabia za kupuuza,
ni mtu asiyejali sana,
ni mtu ambae, hana utekelezaji, au ufuatiliaji, wa kina.

ukiitwa mpuuzi kama ndivyo ulivyo siyo tusi,

ila ukiitwa mpuuzi wakati uko makini unakuwa umetukanwa.

Mwisho wa kunukuu[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Siyo kweli. Ingekuwa hivyo DC asingeweza kumfokea. DC ni mwakilishi wa Rais ktk wilaya

Sent from my TECNO N5 using JamiiForums mobile app

Acha ujinga wewe.
Aliyekwambia ukiwa mwakilishi wa Rais kazi yako ni kutukana watu nnani?
Je, unataka kusema kwamba Rais Magufuli anayewateua ndio anawatuma kufanya kazi za kihunihuni za kutukana watu na kuwaweka L/up masaa 24/48?
 
Nafasi za asante Mzee kunisaidia; eti unacheka nini unacheka nini - duh!!!
 
Hizi teuzi za JPM kwa kweli nyingi zinaleta taswira mbaya kwa serikali ya awamu ya tano, semina elekezi ni muhimu sana kama ndiyo mtu ndiyo unaanza majukumu mapya, hili la Jerry Muro kumfokea mkurugenzi ambaye hana mamlaka yoyote ya kiutendaji ni swala kijinga kbs, hata ukijaribu kuangalia RC naye kakaa tu hapa kama picha, kwa tunaosoma alama kwa ile video inaonekana nafas ya RC Gambo iko wazi na kijana anaitamani ama kuna maelekezo ya ziada, ila kwa style hii za teuzi inaonekana hata vetting haifanyiki watu wanaokotezwa tu, mfano wa hizi teuzi::
1. Makonda
2. Jerry Muro
3. Kangi Lugola
4. Chalamila
5. Juliana Shonza
6. Dr. Philip Mpango
7.....
Unaweza ongezea hapo
 
Mkuu wewe unajua vigezo na masharti ya hizo teuzi? Msimpangie mkulu
 
Ukitoka Chadema kwenda CCM ni sifa kubwa ya kuteuliwa. Huko CCM wamejaa vilaza tu ndiyo maana wanapewa kazi ya kutukana wapinzani mitandaoni na kusifia watawala kazi ambayo haihitaji akili kubwa.
 
Hizi teuzi za JPM kwa kweli nyingi zinaleta taswira mbaya kwa serikali ya awamu ya tano, semina elekezi ni muhimu sana kama ndiyo mtu ndiyo unaanza majukumu mapya, hili la Jerry Muro kumfokea mkurugenzi ambaye hana mamlaka yoyote ya kiutendaji ni swala kijinga kbs, hata ukijaribu kuangalia RC naye kakaa tu hapa kama picha, kwa tunaosoma alama kwa ile video inaonekana nafas ya RC Gambo iko wazi na kijana anaitamani ama kuna maelekezo ya ziada, ila kwa style hii za teuzi inaonekana hata vetting haifanyiki watu wanaokotezwa tu, mfano wa hizi teuzi::
1. Makonda
2. Jerry Muro
3. Kangi Lugola
4. Chalamila
5. Juliana Shonza
6. Dr. Philip Mpango
7.....
Unaweza ongezea hapo
Kuna wakati nawaza,hivi vijana wa enzi hizo,kama Nyerere,Salim Ahmed Salim,ambaye alikuwa balozi baada tu ya kumaliza kidato cha sita,walifanya makubwa kuliko yanayofanywa na hawa wasomi wetu wenye PHD zao,
Kama Tanzania ndio iliwazaa hao vijana wa kale,basi vijana wa sasa,Makonda,Jerry Muro,watakuwa na baba mwingine,maana hawa wa sasa wanafanya madudu matupu,
 
Back
Top Bottom