Wamewala wengine wamekwisha sasa ni kulana wao kwa wao tu. Baada ya kumalizana watahamia kwa wapiga kura wao.
Muda ndio mwalimu sahihi kabisa ktk hili wadau
🙆🏽♂️🙆🏽♂️Ila na huyo mwenye PHd analo la kujifunza toka hapo, mtu umesoma na una malengo yako uwe msomi ulobobea uwe profesa, from no where unateuliwa tu kijingajinga na wewe unakubali,tena anaekuteua anajinasibu ni kichaa na wengi mnajua bado mnakubali kuteuliwa.Basi mkubali na kutukanwa na mabashite yake.Uprofesa sahauni.
Kwa taarifa ni kuwa waraka umepelekwa kwenye vyuo vyote vya umma kuwa mwanataaluma yoyote aliyeteuliwa na jiwe,akishindwa huko alikopelekwa basi asipokelewe pindi atakapoomba kurudi baada ya kutumbuliwa alikoteuliwa.
Kazi mnayo
Dokta mzima anakubali kuwa DED si uzuzu huo?Inatia uchungu. Mtoto mdogo unamshambulia mtu mzima mbele ya dunia nzima inaona, Professa mzima. Nalo professa zima linababaika tu.
Mkuu nimeona umezungumza maoni yako ambayo kiasi kikubwa uko sahihi, Ila kabla ya kumdhalilisha mtu kwenye umma lazima uwe na uhakika wa kile kilichomfanya yeye kuchelewa hapo alipo.Labda kwa kuzungumza ukweli ninaoufahamu juu ya tukio kwa sababu mimi naishi na huyu mkurugenzi kwake ila pia siwezi kuzungumza kwa kutetea upande wowote lakini nitazungumza namna stori ilivyokuwa na dr alivyofika nyumbani alivyotuambia nini kilitokea kabla ya kuenea mitandaoni.Ilikuwa ni juzi siku ya Jumanne usiku wakati mkurugenzi anarudi nyumbani alitukuta tumekaa sebuleni tunaangalia filamu ya marehemu Steven Kanumba dar 2 lagos chanel ya St swahili, alivyofika baada ya kumsalimia alikuwa tofauti na tulivyomzoea yaani hakuwa na furaha kuna simu ikawa imeingia ya kiongozi mmoja hivi wa serikali akamuuliza mkutano wenu umeendaje, akwambia haukuwa vizuri kulikuwa na tatizo baada ya kusikia hivyo ilibidi kupunguza sauti ya tv ili kusikiliza kilichotokea baada ya kuongea na simu akaanza kutuelezea ilivyokuwa.Kwahiyo "dakika 10 tu" umemaanisha nini? Unaona dkk 10 ni muda mfupi sana? Ndio maana waafrika tuko nyuma sana, hatujui thamani ya muda. Na huyo ni DED ambaye ana gari na dereva. Tujifunze kuthamini muda.
Siku moja dada mmoja alienda ofisi fulani kwa bodaboda, kabla hajaingia ofisini akamwambia jamaa amsubiri dkk chache warudi nae, dada kakaa humo zaidi ya dkk 20. Alivyotoka jamaa akamwambia naomba kwanza sh 2,000 ya kuniweka hapa kabla hatujaondoka. Dada akakataa likazuka zogo jamaa kidogo amshushie dada kichapo baadhi ya watu wakaja pale kuamua na ikaonekana dada ana makosa msamaria fulani akatoa ile 2,000
Na maofisini ndio kuna ujinga zaidi, yani unaenda kwa ajili ya kuhamisha mtoto unaambiwa subiri, unakaa huko masaa kadhaa watu wanapiga zao story tu. Ukiingia tena ofisini jamaa anachukua fomu zako anasaini anakwambia hapa tayari nenda mkoani. Unajiuliza yani kumbe ilikuwa kusaini tu?
Pamoja na ukweli kuwa viongozi lazima waheshimiane lakini pia hata huyo DED kwa kuchelewa maana yake hakuwaheshimu DC na RC
Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo kweli. Ingekuwa hivyo DC asingeweza kumfokea. DC ni mwakilishi wa Rais ktk wilaya
Sent from my TECNO N5 using JamiiForums mobile app
Kuna wakati nawaza,hivi vijana wa enzi hizo,kama Nyerere,Salim Ahmed Salim,ambaye alikuwa balozi baada tu ya kumaliza kidato cha sita,walifanya makubwa kuliko yanayofanywa na hawa wasomi wetu wenye PHD zao,Hizi teuzi za JPM kwa kweli nyingi zinaleta taswira mbaya kwa serikali ya awamu ya tano, semina elekezi ni muhimu sana kama ndiyo mtu ndiyo unaanza majukumu mapya, hili la Jerry Muro kumfokea mkurugenzi ambaye hana mamlaka yoyote ya kiutendaji ni swala kijinga kbs, hata ukijaribu kuangalia RC naye kakaa tu hapa kama picha, kwa tunaosoma alama kwa ile video inaonekana nafas ya RC Gambo iko wazi na kijana anaitamani ama kuna maelekezo ya ziada, ila kwa style hii za teuzi inaonekana hata vetting haifanyiki watu wanaokotezwa tu, mfano wa hizi teuzi::
1. Makonda
2. Jerry Muro
3. Kangi Lugola
4. Chalamila
5. Juliana Shonza
6. Dr. Philip Mpango
7.....
Unaweza ongezea hapo