DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Wachaga huwa hawana huo ujinga sijui kautolea wapi?
Mabogus wamejaa tunao maofisi. Halafu ni waoga ile mbaya ukiwaambia unawafukuza kazi wanalia kabisa walishanililia kama watatu hivi sijui wanashida sana huko kwao??
 
Eeeehhhh... Jamani Jerry anakoelekea sio kabisa.. Eeeeeh..!!😡😡😡😳😳😳😳 Mh Rais wangu tengua huyu mtu, plz plz plz...!!! Yaani nasema kweli kabisa ingekuwa ni mm ananinyooshea kidole hivyo napiga ngumi hadi atakimbia atasahau kila kitu hapo..hatarudia tena kabisa..!! Dr. Mahela is the most reputable academician, alafu Jerry anamfanyia hv? OMG..!!
Hivi huyu ndo jery wa ile katuni ya tom and jery
 
Comment yako inaondoa vidonda vya tumbo, ana Phd ya HISABATI? aseh... Sasa kwann asirudi kufundisha aseh
Ndiyo mkuu. Amefundisha Mlimani kwa muda mrefu. Sikujua kama alishachomolewa na kupewa uDED. Sijui mishahara na marupurupu ya maDED yalivyo ila kama alivyosema G. Malisa hapo juu inaonekana maDED wanadhibiti bajeti ya mamia ya mamilioni ya shilingi. Pengine ndicho kinachomfanya msomi huyu nguli wa Hisabati kutukanwa na kanjanja failure; na kuaibishwa mbele ya dunia. Tumbo !!!
 
PhD holder ana mshahara mkubwa kuzidi wa DED, DC hata mkuu wa Mkoa. Ukiongeza na uwezekano wa consultancy na winning big project, ni nonsense kuwa DED then ukatukanwa na vijana wa CCM. Pamoja kuna umuhimu wa kuwa na DED msomi ili atumie tafiti kuleta maendeleo ila ni aibu kutukanwa mbele za watu.


Ni kweli jamaa aliacha mshahara mkubwa na kukubali cheo cha DED chenye mshahara mdogo.
Kwasasa Dr ni part time lecturer Nelson Mandela University analipwa kwa masaa tofauti huyo DC mwenye madharau
 
Kilichonikera ni kuona PhD ya mathematics specifically financial mathematics anakemewa na dogo ambaye hata kula yake ilikuwa shida mpaka JPM alipomuona.

Taabu sana.
PhD ni part time lecturer Nelson Mandela University analipwa kwa masaa.Murro muda wake ni kutisha na kudharau wananchi.
 
Hasira za baadhi ya wanachi juu ya utawala wa awamu ya tano ndio naiona hap.
DC Jerry Muro alikuwa sahihi kabisa kumfokea DED kwa kuchelewa kufika sehemu husika na kuucheleweshwa msafara wa mabosi wake.
Hivi PHD holder ndio aruhusiwe kufanya kazi kwa muda anaotaka yeye ?
Aliyemwambia asahau dokumenti muhimu ni nani, huo ni uzembe kazini.
Au kwakuwa ana PHD basi afanye kazi anavyotaka yeye ?
Huwezi kuwachelewesha DC na RC wakati taarifa ya msafara wao ulikuwa nayo mapema halafu uchekewe tu.
Tena anabahati sana, angekutana na Jembe Kangi Mwana wa Lugola angemfukuzia mbali.
Hii ni Zama mpya wandugu wapendwa.
Zama za Hapa Kazi Tu.
We chapa kazi kwa juhudi na maarifa hutasumbuliwa.
Visababu vya, nimesahau, sikujua, nimechelewa, nk havitavumiliwa.
Nashangaa baada ya kumwonya mchelewaji ili siku za usoni awe anawahi katika majukumu yake, mnashutumu aliyemwonya.
DC Jerry, Piga kazi hakika uko sawasawa.
Kama wafanyakazi wenye PHD hawataki kuonywa wanapokosea basi hizo PHD hazina maana hata kidogo.
 
Sasa hawezi kuivumilia hiyo tabia siku nyingine, ina maana akiirudia atamfanyaje., kwani si wote wanateuliwa na yule yule?
Hawa DC wana mbwembwe sana pale wanapokua nyuma ya camera.
 
Nyie Watu wa ajabu sana Mkurugenzi anachelewaje dk 10 ana kila kitu kuanzia Mafungu mpaka vitendea kazi?
Au ni ile kwamba lazima mje hapa na kitu kuonyesha Wateule na Serikali hawafanyi ipasavyo? Mtasubiri sana
 
Hana busara, kova atakuwa ded wake tuone kama atatukanatukana
 
Wewe mzazi upo hapo umesimama. Halafu matoto yasiyo na adabu yakaanza kufokeana mbele yako. Ni kweli utakaa kimya tu? Mkuu wa mkoa ambaye naye hujifanya mkali sana hapa naona yuko kimya tu. Au Jerry naye ni mtoto wa dadiii ndo maana Gambo ameogopa kuingilia kati?

Halafu anayefokewa ni PhD holder tena bingwa kabisa wa Hisabati. Alipaswa kuwa ananoa vijana wetu Mlimani huyu hasa ukizingatia kuwa tuna wataalamu wachache sana wa somo hili muhimu. Leo yuko hapa anafokewa na failure na (certified) mropokaji. Tumbo mwanaharamu sana aisee. Na kwa mtindo huu wasomi wa Tanzania mkiendelea kudharauliwa msilalamike. Sad [emoji36][emoji36][emoji36]

Nakubalina na wewe mkuu 100%. Lakini huyu DED ana matatizo pia. Yaani taaluma yake ni muhimu kuitawanya kwa wanafunzi wa chuo ili tuzalishe wana hisabati wengi.. Na wanaohitajika sana kwenye kila masomo mengi hasa ya uinjinia na sayansi. Yaani kaivunja thamani Phd yake matokeo yake anatukanwa na mpumbavu kama huyo anayetafuta kiki. Hata rais pia inawezekanaje kumtoa chuoni mtaalamu kama huyo kumpa post ya kijinga kama hiyo ya DED? Very bad decision.
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu, tukio hilo limetokea mbele ya RC ( Gambo ) na baadhi ya viongozi wa Arusha, huku Gambo akionesha dhahiri kutofurahiswa na tukio lile



Huu ndio mfano wa maudhui wa kale kawimbo kanakoitwa 'Madaraka ya Kukevya'

AHAA UONGOZI WA KUOSHEANA MBELE YA VYOMBO VYA HABARI NA WANANCHI DUU NOMA
 
Nakubalina na wewe mkuu 100%. Lakini huyu DED ana matatizo pia. Yaani taaluma yake ni muhimu kuitawanya kwa wanafunzi wa chuo ili tuzalishe wana hisabati wengi.. Na wanaohitajika sana kwenye kila masomo mengi hasa ya uinjinia na sayansi. Yaani kaivunja thamani Phd yake matokeo yake anatukanwa na mpumbavu kama huyo anayetafuta kiki. Hata rais pia inawezekanaje kumtoa chuoni mtaalamu kama huyo kumpa post ya kijinga kama hiyo ya DED? Very bad decision.
Huyo DED mwenye matatizo amechagiwa sasa kuwa MKURUGUNZI TUME YA UCHAGUZI (NEC).
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu, tukio hilo limetokea mbele ya RC ( Gambo ) na baadhi ya viongozi wa Arusha, huku Gambo akionesha dhahiri kutofurahiswa na tukio lile



Huu ndio mfano wa maudhui wa kale kawimbo kanakoitwa 'Madaraka ya Kukevya'

hivi sa hivi akiangalia hii video na jamaa ndo mkuu wa NEC kweli muosha huoshwa
 
Back
Top Bottom