BRN
JF-Expert Member
- Nov 18, 2013
- 5,188
- 6,633
Mkuu wako tofauti,Dc ni zaidi ya Mkurugenzi.Kuna kitu hapa kinaleta mvurugano ni kwa awamu hii ya tano wizara ya TAMISEMI kuwa china ya ofisi ya Rais hivyo Rais anapotamka na kuwatangaza Wakurugenzi imejengeka dhana ya wakurugenzi kujiona nao wana ngazi sawa na wakuu wa wilaya jambo ambalo sio.Mkuu wa wilaya ni kiongozi wa kisiasa na wakurugenzi ni watendaji, aidha, mfano rahisi tu ni kwamba unaweza kukuta kuna wilaya inazo halmashauri zaidi ya tatu zenye wakurugenzi lakini Mkuu wa wilaya anayeongoza wilaya hiyo ni mmoja tu.Ikumbukwe kwamba kuna wilaya na mamlaka za serikali za mitaa au halmashauri za wilaya,miji,manispaa na majiji.(rejea sheria ya tawala za mikoa 19,1998 na sheria namba 8-9/1984 za serikali za mitaa)Fafanua basi kama wote wako sawa kivipi...?
Tukirudi kwenye tukio,Kiitifaki Mkurugenzi alitakiwa awepo eneo la tukio hata kabla ya Dc na Rc,tukubaliane tu kwamba alikosea na kama kulikuwa na dharula angetoa taarifa.Upande wa pili Dc alikuwa sahihi kukemea jambo hilo ila namna alivyotoa karipio lake labda ndio linazua utata, ila ilibidi afanye hivyo ili kuonyesha mamlaka yake( ambalo ni hulka ya kibinadamu) na kumuonyesha bosi wa RC kwamba anasimamia watu walio chini.
Wasalam.