DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Mkuu wa Wilaya Jerry Muro anamtukana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Dr.Wilson Mahela (PhD) mbele ya Mkuu wa mkoa na macamera ya waandishi wa habari yanawamulika. Uongozi wa kijinga sana huu. Kanuni za maadili ya uongozi haziruhusu kufanya huu utoto. Kama Mkurugenzi alichelewa kufika, kuna namna bora ya kumuwajibisha ambayo ingekua na tija kuliko huu ujinga uliofanya Jerry. Tatizo mnateuliwa teuliwa tu bila hata kupewa semina elekezi.

Mtu hajawahi kuwa hata CR darasani leo anakuwa DC ama RC what do u expect? Matokeo yake ndio haya ya kuja kutukanana hadharani na mnaona sifa kurekodiwa. Halafu wewe Jerry sio mamlaka ya nidhamu ya DED. Pengine huo uDC umekulevya. Mamlaka ya nidhamu ya DED ni RAS. Kwahiyo kama alichelewa ungeweza kuzungumza nae baadae na kumueleza masikitiko yako, na kama angekaidi ungemripoti kwa RAS. Sio kutukanana hadharani.

Unamtukana DED na kumuita mpuuzi na mpumbavu hadharani, halafu unategemea awasimamie watendaji wa Halmashauri. How that possible? Atawasimamiaje wakati wameona akiitwa mpuuzi na mpumbavu hadharani? Na wenyewe watampuuza tu kama ulivyompuuza wewe. Ni aibu viongozi kuzozana hadharani. Wahenga walisema wazazi wapumbavu pekee ndio wanaoweza kugombana mbele ya watoto. Kulikua na tatizo gani mngeendelea na hiyo ziara then badae mkae na kujadili?

Halafu kichekesho unamlaumu DED kwa kuchelewa dakika 10, lakini wewe umepoteza dakika nyingi zaidi kumtukana. Hivi lengo lako lilikua kuokoa muda kweli?

Huyu Dr.Wilson Mahela ni PhD holder. Amefundisha chuo kikuu UDSM muda mrefu wakati wewe ukifanya ukanjanja kwenye media. Amekuzidi umri, amekuzidi elimu, amekuzidi busara. Kama umeshindwa kumheshimu kwa nafasi yake basi ungemheshimu hata kwa umri wake tu.

Then huyo DED unayemdhalilisha ndo anayekuweka mjini. Tunajua maDC hamna budget. Mnalelewa na ofisi za DED kwa kila kitu. Hadi mafuta ya gari mnaomba kwao. Sasa how comes unamdhalilisha mtu anayekufanya usurvive? Kesho ukimuomba mafuta akikunyima utamfanya nini? Au ndo utaita tena macamera uanze kumtukana? Growup na uache sifa za kijinga. Uongozi ni kujifunza. Take time to learn from your elders kabla ya kukurupuka. Unajidhalilisha na kumdhalilisha aliyekuteua.!
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu, tukio hilo limetokea mbele ya RC ( Gambo ) na baadhi ya viongozi wa Arusha, huku Gambo akionesha dhahiri kutofurahiswa na tukio lile



Huu ndio mfano wa maudhui wa kale kawimbo kanakoitwa 'Madaraka ya Kukevya'

HIVII TURUDI NYUMA KWANZA .. Hawa wanaoteuliwa walishawahi kupitia mafunzo ya uongozi kwenye chuo chochote?
kile chuo cha MAADILI YA UONGOZI kipo kweli.
hizi teuzi za kukurupuka haya ndio matokeo yake
 
Atapandishwq cheo achukue nafasi ya Gambo.

Maana awamu hii ni ya viongozi vichaa
Kuchelewa hutokea hata malikia wa uingereza alichelewa dakika 10 alipotakiwa kukutana na Tramp.
Kuna siku MAKONDA alichelewa wakati mama Samiya alikuwa na mkutano
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu
Dakika kumi ni nyingi sana,alitakiwa afike saa nzima kabla
Ifike mahala uzembe uzembe kama huu tuachane nao
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Una maana yule aliyeiba Trillion 1.5 kwenda kuwanunua wanasiasa wa upinzani, kumlipa aliyefanya jaribio la kumuua Tundu Lissu na kujenga uwanja wa ndege nyumbani kwake? Kilangila.
Nilikuwa nimesahau hiyo
 
Huu ni ujinga wa kutojua matumizi ya ofisi. Sasa ofisi amepewa ya nini? Haya ni mambo ambayo alipaswa kuyafanya ofisini kwa kumwita mkurugenzi ofisini lakini sio kumfokea kama mtoto mdogo na kumnyooshea vidole namna ile kana kwamba anataka kumpiga. Hata mkuu wa mkoa anaonesha wazi kutopendezwa na hicho anachokifanya huyo DC limbukeni
 
Huyu angeachia tuu nafasi yake pamoja usomi wake ameenda kudhalilisha mbele ya kamera ni huyo mjinga
Kwani DC yeye hajawahi kuchelewa tangia amekuwa kwenye utumishi wa taasisi mbalimbali ambazo amewahi kutumikia kabla ya kuwa DC, ndio vile tunasahau haraka sana tulikotoka.
 
jerry muro anachapa kazi, ma ded wengine ni wazembe sana wanapata ela mpaka wanajisahau, imefika kipindi cha kupelekeshana sio kudekezana kiafrika kama zamani. Hata ded nae akikuta de au mtu mungine amefanya uzembe atamfkea hivyo hivyo.Imefika kipindi cha watu kuheshimu majukumu yao sio kuzoea majukumu kama walivyo wa japan na south korea hapo maendeleo yatakuja.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Sasa nimeamini ndege wanaofanana,huruka pamoja,
Ni mwendo wa vichaa tu
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu, tukio hilo limetokea mbele ya RC ( Gambo ) na baadhi ya viongozi wa Arusha, huku Gambo akionesha dhahiri kutofurahiswa na tukio lile



Huu ndio mfano wa maudhui wa kale kawimbo kanakoitwa 'Madaraka ya Kukevya'
Jerry kaharibu sana.
Aina hii ya uongozi si nzuri.
Haijengi timu na haina hekima wala busara.
Kwa mfano,
Je baada ya kubwata kooote angeambiwa walipata ajali ya gari, au ililazimu wasimame kuokoa maisha ya ndugu yake angefanyaje?
Si ndio kuumbuka huko?
Mdomo huponza kichwa.
Tujifunze.
 
Kwa nini achelewe?
Afteral huyu DED ni wa arusha manispaa, siyo wa Arumeru, ni nini kimem-washa DC wa Arumeru hadi amfokee DED wa wilaya nyingine? Tena mbele ya RC? RC Gambo amedhalilishwa sana.
 
Kuna inferiority complex kwa Jerry
Ndio maana namshauri atafute mtaalamu wa saikolojia ampe msaada.

Imembidi hata huyo mkurugenzi kumcheka,kwanza ni lazima adharaulike kwasababu wanajua amepata hiyo nafasi kwa kuropoka na kutukana hovyo.

Sidhani kama kuna mtu atamheshimu kwasababu yeye hakujiheshimu na hata sasa hafanyi hivyo.
 
Afteral huyu DED ni wa arusha manispaa, siyo wa Arumeru, ni nini kimem-washa DC wa Arumeru hadi amfokee DED wa wilaya nyingine? Tena mbele ya RC? RC Gambo amedhalilishwa sana.
Sura ya RC inaonesha kutofurahishwa kabisa na anayofanya DC.

Inamaana kiongozi wa msafara hapo ni DC au RC?
 
HIVII TURUDI NYUMA KWANZA .. Hawa wanaoteuliwa walishawahi kupitia mafunzo ya uongozi kwenye chuo chochote?
kile chuo cha MAADILI YA UONGOZI kipo kweli.
hizi teuzi za kukurupuka haya ndio matokeo yake
Kimekatazwa kufanya udahili.
 
kesho utasikia jerry piga kazi ww mi kichaa kama mm ndio maana lilikupa wilaya. nasema chapa kaziiiiiii!!!
 
Hii speed iliyopo dereva akikanyaga breki galfa wengi watatokea madirishani
 
Back
Top Bottom