DC Jokate, huu ni muda sasa wa kubadili aina ya mavazi yako

DC Jokate, huu ni muda sasa wa kubadili aina ya mavazi yako

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kwako DC Jokate

Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri unayofanya, binafsi nakukubali sana aina ya uongozi wako, umefanya kazi nzuri sana huko Kisarawe.

Pia, sina wasiwasi kuwa hata hapa Dar ulipohamishiwa katika wilaya ya Temeke utafanya vizuri.

Naamini kabisa kuwa kwa jinsi unavyochapa kazi ukiendelea hivi basi una future ya kuwa kiongozi mkubwa nchini.

Ila kuna kitu nataka nikwambie, Mavazi yako hasa yale yanayoacha kifua chako wazi si muafaka kwa mwanamama mwenye hadhi ya ofisi ya umma unayoishikilia.

Nafahamu kuwa una bsckground ya mambo ya mitindo na ulimbwende, lakini naomba ufahamu sasa kuwa sasa wewe ni mkubwa kuliko hayo, wewe ni mtumishi na kioo cha jamii, ni kioo cha mabinti nchini, nakuomba basi hilo vazi linaloacha kifua chako nje uliache na badala yake tafuta vazi zuri tu linaloendana na hadhi ya ofisi ya Umma.

Ndugu DC hii nchi imejaa marijali, wanaume shababi, ambao kiukweli wakiona kifua kizuri kama hicho wanaweza kupatwa mfadhaiko, kwa hiyo ili kuepusha hayo yote nakuomba ndugu DC kwa unyenyekevu mkubwa utuonee huruma kwa kuvaa mavazi muafaka zaidi.

Mheshimiwa wewe una potential ya kuwa kiongozi mkubwa huko mbeleni, naomba uanze kujiweka katika hali ya mtu aliyetayari kupokea majukumu makubwa kwa kujinasabisha na majukumu hayo kitabia na kiutendaji.

Natanguliza shukrani, na samahani sana kama nimekukwaza

images (22).jpeg
images (19).jpeg
images (18).jpeg
images (17).jpeg
 
Back
Top Bottom