DC Jokate Mwegelo na Uongozi wenye tija

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Ama kwa hakika Tanzania ingepata viongozi wenye kujitoa bila kujali maslahi yao binafsi,ubabe,majivuno,ukandamizaji na kiburi cha madaraka nchi ingesonga sana hii

Kwa anayoyafanya huyu binti kule Kisarawe hakika yanafaa kuigwa,sema tu nature ya wakazi wa wilaya yenyewe sio wachakarikaji wanamuangusha sana mheshimiwa DC kwa kutochangamkia fursa.

Ubunifu,uhamasishaji,ucheshi,uwazi,kusimamia maslahi ya wengi,kusikiliza na kutatua shida zao huo ndio uongozi bora.

Hongera Jojo kwa kuifanya kisarawe kuwa kubwa kulingana na ukaribu wake na jiji la Dar.

 
Tumekusikia mkuu naona umefikisha ujumbe uliotumwaa kuja kuutangaza hapa na DC Jokate hongera sana na ni kweli anafanya kazi nzuri kila mtu anaona sema aende pole pole tu Rais amuona kazi zake....
 
Tumekusikia mkuu naona umefikisha ujumbe uliotumwaa kuja kuutangaza hapa na DC Jokate hongera sana na ni kweli anafanya kazi nzuri kila mtu anaona sema aende pole pole tu Rais amuona kazi zake....
Wewe una chuki labda au roho ya husda ambao ndio first level ya kuwa mchawi.

Hata mimi nampongeza kwa kuviibua vivutio vilivyopo hapo vya utalii.ni kwel hapo Tfs ilikua kama imepaacha hakuna action plan ya kueleweka.

Kiutalii walikuwa wanahifadhi tu bila kuwa na mikakakati.

Nchi za wenzetu uwepo wa hilo mto la kazimzumbwi tu bila hata kuunganisha na park ni hela tupu.
apewe hongera yake kwa kupaibua.
na nimeona anapropose kuwe na information center tourist nampa heko.

Pako vizur. Maeneo kama hayo wenzetu wanzung wanashinda na watoto wao wana fanya kayaks. Ile kuendesha mtumbwi inamkuza sana mtoto uelewa.

Uache kujiona kila kitu husda na wewe ni mchawi.
 
Kwani hiyo kampeni ya Ushorobo inataka nini? Naona siku chache zilizopita alimwita mpaka ex wake Diamond kuja kufanya nae mazungumzo ya kushiriki!!
 
Dada Joket, naona leo umeamua kujipigia promo, mrembo.
 
Muda siyo mrefu kuna panga pangua tumbua inakuja.
Ni vizuri kuendelea ku trend masikioni na mitandaoni regardless ume achieve au huja acjieve chochote.
Vyombo vya habari vinaweza ku kubrand ukaonekana unapiga kazi.
Jamii nayo inajua nani anafanyakazi na nani ni porojo.
Changamkeni.
 
sina shaka na uwezo wa huyu binti,licha ya kuwapo tetesi kwamba ni usingizi wa bwana BUPIJI.
 
Tulishawahi kushauri humu naona bado mchakato tu, JoJo anastahili kuwa RC.
 
Anapiga hela balaa ile michango ya 20 kiinvilio alafu tamasha limeahirishwa kapeleka wapi
 
Nakupa heshima yako maana naona ni mkubwa kwangu so heshima yako lazima nikupe siwezi kukuvunjia heshima kama ulivyofanya....Nipo humu ndani zaidi ya miaka 15 so naijuwa hii site vizuri na kuheshimu watu wote humu ndani kuliko wewe umeingia hata mwaka bado huna unakuwa na maneno machafu....kila mtu ana freedom ya kuongea apendacho....
 
Wabongo wengi huwa tunabisha Kwa Hsia , na mahaba mtu Yuko radhi kutukana akitetea lakn ukimuomba data Kwa ajili ya utetezi wake hamna kila kitu ...... Nyanja ulizoainisha kupata data zake ni ngumu ...ni kweli Jokate anafanya vzuri kwenye media lakn tunahitaji data ili kuverify sifa anazopata hapo ndo kizungumkuti kinapoanzia...haya haya ya RC Mtaka wa Simiyu ...
 
Anajitahidi sana huyu dada
 
Waliokimbia tunaomba mrejesho wa mbio zilikuwaje huko?
 

Mara nyingi uwa nasema uyu dada angepewa wilaya kama Bagamoyo au Pangani ambazo zinavivutio lukuki angetisha saaana
 
Tuache wivu huyu dada sijawahi kumuona anajimwambafai sana mbele ya makamera ila sio siri kina piga kazi sana .Mm naona hata angepewa mkoa wa dar maaana ni mtulivu sana na anachapa kazi vizuri.
 
Anajitahidi sana huyu dada

Yes, anajitahidi saana. TAMISEMI inapaswa kuchangua mabinti wapatao 100 wenye uwezo kama Jokate then ipeleke mswada bungeni wa kuwafanya watawa na baadaye wapewe ukuu wa wilaya kila mmoja naamini baada ya 10yrs watakuwa wamezisogeza mbali sana kimaendeleo. Bila kufanya hivyo wakiolewa tu wanaume watawapotezea focus ya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…