Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Afukuzwe na aseheme alifanya nini kwenye mapori,huenda aliuua,poor Tanzania!!
Siyo yeye ni Serikali ndio ilifanya hayo mambo huko maporini.
Inabidi serikali itoe tamko mambo gani yalifanyika huko maporini?
 
Kwani Rais hawapendi wasema kweli?
Sura kama hizi ndizo zilizojaa kwenye nafasi za utawala na uongozi. Isivyokuwa bahati hata watumishi wa Serikali kwenye nafasi zao wanafanana na huyo jamaa hapo juu kwa kauli na matendo yao. Wale wanaoingia mara kwa mara kwenye ofisi za Serikali wanaelewa hali ilivyo.
 
Hivi hawa viongozi wa CCM huwa wanajiuliza madhara ya maneno Yao kwa wananchi yatapokelewaje?

Luka 12:2-4

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.
 
Kuna chama kimebaki na mipini tu majembe yote yashajitafutia mahala Sasa,nawahakikishieni kunakucha soon.

Luka 12:2-4

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.
 
Haya wanaosemaga kwamba hakuna ushirikina, nini hicho? Huyu jamaa karogwa hapo na wale ndugu wa marehemu aliowaua.

Hayupo sawa huyu kaanza kuchanganyikiwa. Damu za watu zinamsumbua huyu. Na hata anaweza kupelekwa porini na yeye!

Mfuatilieni miaka kadhaa atakuwa chizi tayari wa kuvua nguo.
 
Mazingira ya kwenye mapori ndio yapi au ndio Yale ya watu kutekwa na kutupwa porini na kama ndio hivyo kumbe Sasa mpaka Sasa wanahusika na watu kupotea
 
Mkuu

Luka 12:2-4

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.
 
Kuna haja ya kuanzisha shule Ya kukuza uelewa Kwa viongozi wapuuzi kama huyu DC,anaongea ambayo mama hayataki,akiwemo ofisini kufikia kesho itakuwa ni doa Kwa serikali yetu.
Hoja sio kuwa mama hataki kusia hayo, ila huu ni ushahidi kuwa uchaguzi ni maigizo tu mara nyingi kuna uchakachuaji. Ilianzia kwa Nape sasa imekuja kwa huyu, hii ndio sababu kila mara watu wanataka Tume huru ya Uchaguzi ili wakushinda ashinde na wakushindwa ashindwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…