Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata kama mmetengua uteuzi wake lakini Marco Ng’umbi kasema ukweli mchungu.

Kauthibitishia Umma mambo matatu-;

1. Kathibitisha kuwa Maccm hatakubaliki,

2. Kathibitisha kuwa maccm huwa yanaiba Kura,

3. Kathibitisha kuwa Serikali huwa inateka watu na kuwatupa kwenye mapori.
20240901_190016.jpg
 
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."


View attachment 3084265

Pia soma:

Tunaposema kuwa CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu tunamaanisha
 
Alitumwa na serikali kuua Wapinzani ili wapite bila kupingwa, Iko hivi, January, Nape,Riziwani na Kasimu Majaliwa walipita bila Kupingwa huku wagombea wa upinzani wakikamatwa ama kuokotwa kwenye mapori ya Mkurunga, Kwa Mfano, Mgombea wa Chadema Mtama aliyeitwa Suleiman Mathew alikamatwa kwenye ofisi ya Ded akirejesha fomu ya kugombea Ubunge, akapewa kesi ya uongo ya Uhujumu Uchumi, Mgombea wa upinzani Jimbo la Rwangwa aliokotwa Mkuranga akiwa nusu Maiti, hili ni Jimbo la Kasimu Majaliwa.

Haya Mambo yalifanywa Mchana kabisa huku kila mtu akiona kwa macho.

Mwingine ambaye baadaye atakamatwa na kushitakiwa ni Abood wa Morogoro, huyu pia aliteka Wagombea wa Upinzani akiwemo Mgombea wa Chadema

Mnyororo ni mrefu mno na nakuhakikishia kwamba siku zijazo watakamatwa na kushitakiwa, Ushahidi umejaa tele, hakutakuwa na Mswalie Mtume, Usalama wao ni Kufa kabla ya Kukamatwa, lakini wakiwa Hai watakamatwa hata wakiwa kwenye Wheel Chair
Aisee kumbe mambo yalikuwa mazito hivyo?
 
Tunaposema kuwa CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu tunamaanisha
Hivi hawa viongozi wa CCM huwa wanajiuliza madhara ya maneno Yao kwa wananchi yatapokelewaje?
 
Back
Top Bottom