Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Upinzani ni kama umeumbwa na macho kwenye makalio, huwa wana kazi ya kuamua watembee uchi waone au wajisitiri wawe vipofu.
 
Upinzani ni kama umeumbwa na macho kwenye makalio, huwa wana kazi ya kuamua watembee uchi waone au wajisitiri wawe vipofu.
Kwa maana yako wapinzani ndiyo wanatoa hayo matamko ya hovyo kama huyo dc wa Longido?

Hivi nyinyi uvccm mafunzo yenu Hawa mnajifunzia maujinga?
 
Kwa maana yako wapinzani ndiyo wanatoa hayo matamko ya hovyo kama huyo dc wa Longido?

Hivi nyinyi uvccm mafunzo yenu Hawa mnajifunzia maujinga?
Kwa maana yangu ni upinzani una macho ila yapo makalioni, uamuzi ni kwao, kutembea uchi waone au wajisitiri wawe vipofu.
 
DC ambaye hana weledi kuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na USALAMA ni hatari sana,mwisho wa siku wanavujisha siri za taasisi.
 
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."

View attachment 3084265

Pia soma:

Huu ndio ukweli.

Wizi unaanzia katika kura na wakiingia madarakani ni mwendo ule ule.
 
Back
Top Bottom