Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bagonza na Dr Kitime wanatimiza majukumu yao kwa asilimia 100.

Msikilize na mlevi mwingine huyu kutoka Lumumba
Askofu Bagonza na Padre Kitime ndio Vionozi Pekee wanaoongozwa na Roho wa Mungu kama Nabii Yeremia na Nabii Eliya wa leo.
 
Shukrani nyingi zimwendee aliyemdukua, huyu mjinga alikuwa anaropoka akijua hakuna anayemrekodi, Masikini wasipewe vyeo, wakivipata wanajipa Uungu
Oooohh kumbe ndio maana Msigwa mkamnyima Uenyekiti wa Kanda sababu hana hela kumzidi Sugu 😂😂😂

Ndo maana tajiri Mbowe chama haachii kwa maskini akina Lissu na Heche!!
 
"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."

Anaitwa nani huyu bwana?

Mchengerwa na Wizara yake tayari wamemaliza kazi huko mitaani kuhusu uchaguzi wa serikali za Mitaa; na ni hao hao watakao kamilisha shughuli za Uchaguzi Mkuu 2025!

Sasa waTanzania wanataka waambiweje ndipo waelewe; kwamba zoezi la kwenda kupiga kura halina maana yoyote?

Na kama wanaelewa hivyo, kwa nini hali hii isiwastue na kufanya jitihada za kulinda haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka wao badla ya kuwekewa viongozi na CCM?
 
Oooohh kumbe ndio maana Msigwa mkamnyima Uenyekiti wa Kanda sababu hana hela kumzidi Sugu 😂😂😂

Ndo maana tajiri Mbowe chama haachii kwa maskini akina Lissu na Heche!!
Kumbe Lissu na Heche ni masikini? Nilikuwa sijui.
 
Yes kwa maana refa yupo kwa uoande mmoja,
Labda sheria ziabadilike
Iko hivi, asilimia kubwa ya changamoto tunazo zipata, (pitia), zinasababishwa na binadamu kwa makusudi ama bila kujua hata yeye mwenyewe anaweza kujisababishia changamoto bila kujua kwa, wivu uzembe, uvivu ujinga na ushamba hata tamaa
 
Alitumwa na serikali kuua Wapinzani ili wapite bila kupingwa, Iko hivi, January, Nape,Riziwani na Kasimu Majaliwa walipita bila Kupingwa huku wagombea wa upinzani wakikamatwa ama kuokotwa kwenye mapori ya Mkurunga, Kwa Mfano, Mgombea wa Chadema Mtama aliyeitwa Suleiman Mathew alikamatwa kwenye ofisi ya Ded akirejesha fomu ya kugombea Ubunge, akapewa kesi ya uongo ya Uhujumu Uchumi, Mgombea wa upinzani Jimbo la Rwangwa aliokotwa Mkuranga akiwa nusu Maiti, hili ni Jimbo la Kasimu Majaliwa.

Haya Mambo yalifanywa Mchana kabisa huku kila mtu akiona kwa macho.

Mwingine ambaye baadaye atakamatwa na kushitakiwa ni Abood wa Morogoro, huyu pia aliteka Wagombea wa Upinzani akiwemo Mgombea wa Chadema

Mnyororo ni mrefu mno na nakuhakikishia kwamba siku zijazo watakamatwa na kushitakiwa, Ushahidi umejaa tele, hakutakuwa na Mswalie Mtume, Usalama wao ni Kufa kabla ya Kukamatwa, lakini wakiwa Hai watakamatwa hata wakiwa kwenye Wheel Chair
Huyu DC angefaa sana kuwepo kwenye Mdahalo wa jana lkn ndiyo hivyo tena.
 
Iko hivi, asilimia kubwa ya changamoto tunazo zipata, (pitia), zinasababishwa na binadamu kwa makusudi ama bila kujua hata yeye mwenyewe unaweza kujisababishia changamoto bila kujua kwa, wivu uzembe, uvivu ujinga na ushamba hata tamaa
Nini kifanyike sasa?
 
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."

View attachment 3084265

Pia soma:

Amesema ukweli.
 
Yes kwa maana refa yupo kwa uoande mmoja,
Labda sheria ziabadilike
Iko hivi, asilimia kubwa ya changamoto tunazo zipata zinasababishwa na binadamu kwa makusudi ama bila kujua hata yeye mwenyewe anaweza kujisababishia changamoto bila kujua kwa uzembe, uvivu ujinga na ushamba
Nini kifanyike sasa?
Elimu ya kukabiliana na majanga,(how to overcome uncertainty), lakini chanzo kikuu ni jamii ndiyo ilaumiwe kuto chukua hatua jamii ni wewe yule, huyo niliyo naye karibu na mimi yaani tukiendelea kunyamaza hata arudi huyo aliye ahidi kurudi hata fanya chochote Mungu katupa akili na utashi lakini sisi ni wazembe tunawafurahia wanao ahirisha kufikiri kwa nafsi zao yaani kujizima data,tena tunawasifu na kuwapigia makofi
 
Back
Top Bottom