Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani huyu na Ahmed ally wa Ubaya ubwela ni ndugu? Mbona wanafanana kuongea.
Ila CCM bana ni kunywa mtori tu nyama waachie wakubwa.
 
sehemu ambayo ni very disturbing kwenye hii kauli yake ni hapo anaposema maporini. Na huyu yawezakana atakuwa TISS au ni kada wa ccm ambaye ni mmojawapo wa task force maalum ya kuratibu hizo harakati tena idara ya political wing. Maana anaposema 'tuna database ya nchi nzima...' inaonekana ni kitu anakijua haswa.. Dah hapo kwenye neno maporini nimewaza sana ya akina ben sa8 , ulimboka, azore et al. MAPORINI. Neno maporini. DAH! .
 
Huko polini kilifanyika Nini?
Hata nape wakati ule anatolewa bastola alisikika akisema amelala polini kuipigania ccm,na huyu tena anazungumzia mapoli Kuna Nini huko?
 
Na ni kwanini wanaanza kusema ukweli kipindi hiki tena bila kuulizwa?
Au ndo ukweli wa ule msemo, " karma never forget your address" inakurudia tu hata kama ni baada ya miaka 100!
Ukweli wanakili, sawa lakini kwanini iwe sasa.Utadhani walikuwa wakipewa dozi ya kutojitambua wakiwa wanatenda maovu, ila kwa sasa wamenyimwa hiyo dozi ndio wanajitambua?

Hii ngoma nzito ni bora ukaketi pembeni kuangali mchezo mzima,labda tutajifunza jambo.
CCM siyo mtoto mchanga katika medani ya siasa za makomredi.
Walishasema watabaki madarakani miaka 1000.
 
Ni kama wachawi wale wanaoroga na kuua watu, wakikaribia kufa wanaanza kuropoka..anawataja wote aliowaua na mambo yote mabaya aliyowafanyia watu.
Umenikumbusha kisa kigumu mno kilichoikumba familia moja hivi, Bibi aliharibu wajukuu kisa hamtaki mke wa mwanae, karibu anadedi akafunguka yooote.
 
Kuna haja ya kuanzisha shule Ya kukuza uelewa Kwa viongozi wapuuzi kama huyu DC,anaongea ambayo mama hayataki,akiwemo ofisini kufikia kesho itakuwa ni doa Kwa serikali yetu.
Huyo Mama mwenyewe aliwahi kusemaje??? "Hata mkiwapa kura huo upande wa pili sisi ndiyo tutaunda serikali". Wote ni walewale tu!!!
 
Back
Top Bottom