chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Naona kama Magoti anataka kupandisha mabega juu kuliko ya aliyemteua. Maji ya mto huwa hayapandi juu zaidi kupita chanzo chake, bali huteremka chini.
Naona Magoti anajiona ni mnyampara kama wale wa enzi ya ukoloni. Hana uongozi shirikishi na jamii aliyoikuta. Najua na yeye ni mabaki ya yule jamaa aliyeenda zake, na ndiye alimuibua.
Sakata la mkaa, anaweza kulitatua kwa ushirikishaji wa kamati za mazingira zilizo mpaka ngazi ya vijiji. Wananchi wakawa sehemu ya utekelezaji kwa kuwa wao ndio wanawajua wauza mkaa. Sasa mtu ana mkaa fungu moja anaenda kupikia nyumbani kabeba kwa pikipiki, nalo ni kosa?
Masuala mengine pia, hata ya kiimani, waite watu, washirikishe. Watanzania wana akili.
Uongozi ni ushirikishwaji, ukiwashirikisha watanzania, hawana neno, waite, kunywa nqo kahawa, waeleze jambo lako, sikia maoni yao, fikieni uamuzi wa pamoja. Lakini ukivimba, mwenye mamlaka kwa niaba yao anaweza kuku-recall. Hata SSH mwenyewe havimbii watu na kuwatishia ubabe.
Kisarawe ni moja kati ya wilaya tulivu, utulivu huo upewe tafsiri ya maendeleo. Mkuu wa Wilaya aombe mbegu za korosho, parachichi, apiganie zao la mbaazi, ufugaji wa kisasa, elimu. Tembea na hayo.
Kisarawe ina hali ya hewa nzuri, na inaweza kulisha Dar es Salaam.
Ukiwawekea makucha katika ngozi zao, utaona macho yao makali.
Pia soma

- Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam
- Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
- Petro Magoti kupiga marufuku pikipiki kubeba mkaa, nimewaza Mtanzania wa hali ya chini na namna sahihi ya kuwa na hekima juu ya sera ya mazingira

- Kisarawe: DC Magoti apiga marufuku shughuli za ngoma kuhusisha wanafunzi