DC mdogo kuliko wote Tanzania, ashirikiana na mbunge kuimba wimbo kuhamasisha Elimu Wilayani

DC mdogo kuliko wote Tanzania, ashirikiana na mbunge kuimba wimbo kuhamasisha Elimu Wilayani

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
Anaitwa Zainaba Abdallah Issa,ni mkuu wa Wilaya mdogo kiumri kuliko wote Tanzania.Binti Issa ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani iliyopo Mkoa wa Tanga.Moja ya changamoto kubwa anazokumbana nazo ktk Wilaya hiyo ni umasikini na ukosefu wa Elimu kwa wakazi wengi wa
Wilaya ya Pangani.

Yeye anakuwa mkuu wa Wilaya wa 21 toka kuanzishwa kwa Wilaya hiyo,na anasema mara baada ya kupangiwa kufanya kazi Wilaya hiyo watu wengi walimueleza kuwa anaenda kuongoza moja kati ya wilaya ngumu sana na iliyotopea kwa umasikini.

Ili kuendana na kasi ya maendeleo,Bi Zainabu ameamua kujikita katika elimu na hasa elimu ya mtoto wa kike,kwani katika eneo hilo elimu kwa watu na hasa mtoto wa kike imekuwa duni sana.Wilaya nzima ina shule za upili zipatazo 30's ambapo alipofika katika shule hizo zote,hapakuwepo na Shule yenye kidato cha tano na cha sita.

Amefanya juhudi za kuanzisha shule ya kidato cha tano na cha sita kwa kufanya upanuzi katika moja ya shule za Wilayani hapo.Miundo mbinu ni tatizo lingine,kwani wilaya hiyo haiunganishwi na maeneo muhimu kama jiji la Dsm.Umbali wa kutoka Pangani kwenda Handeni ni mrefu kuliko kutoka Pangani kwenda Dsm,lkn hakuna miundombinu inayounganisha Pangani na Dsm.

Kwa kushirikiana na mbunge Kijana wa Jimbo la Pangani,Mh.Zainabu A Iss amezindua wimbo wenye kuhamasisha elimu kwa mtoto wa kike ktk Wilaya ya Pangani,kwa kuwahimiza wazazi kutokuwaoza watoto wa kike wakiwa wadogo bali wawasisitize kupata elimu kwa lengo la kuondoa umasikini.

Hongera sana DC Zainabu .A. Issa,Kila la heri ktk kuwaletea wana Pangani maendeleo ya kweli.
 
Huyu dogo nliona siku hiyo wanamfukuza na mawe kijiweni hadi noma,
Naona anataka kujirudi kivingine...any ways thats creativity

ILA NYIMBO NI MBAYAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Huyu dogo nliona siku hiyo wanamfukuza na mawe kijiweni hadi noma,
Naona anataka kujirudi kivingine...any ways thats creativity

ILA NYIMBO NI MBAYAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Dogo yupi kati ya hao wawili(DC na Mbunge),Kijiwe hukohuko Pangani?
 
Serikali haiajili mtoto mdogo. Fafanua mkuu mdogo kiaje
 
Mkuu kwenye andiko lako umesema kuna shule za upili zipatszo 30's ikiwa na maana kuwa shule za sekondari? Kama ndivyo umekosea, Pangani ina shule za sekondari za serikali saba tu (7) na shule mbili za mashirika ya dini na moja ni ya jumuiya ya wazazi.
 
Huyo MB ndugu, ana kazi ya kufanya kwakweeeli mana ni wanamchukia utadhani alitaka kuwalisha sumu
Mbona jamaa yupo vizuri sana. Huwa anajenga hoja za maana na anapigania kweli wana Pangani. Alipambana na Mama Mwidau kwenye uchaguzi mkuu akambwaga
 
Mbunge na mkuu wa wilaya ni vijana na wote wapo vizuri katika kujenga hoja tatizo lipo kwenye jamii wanayoiongeza bado haijitambui.
 
Back
Top Bottom