DC mdogo kuliko wote Tanzania, ashirikiana na mbunge kuimba wimbo kuhamasisha Elimu Wilayani

DC mdogo kuliko wote Tanzania, ashirikiana na mbunge kuimba wimbo kuhamasisha Elimu Wilayani

View attachment 423733 View attachment 423731 View attachment 423732 Anaitwa Zainaba Abdallah Issa,ni mkuu wa Wilaya mdogo kiumri kuliko wote Tanzania.Binti Issa ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani iliyopo Mkoa wa Tanga.Moja ya changamoto kubwa anazokumbana nazo ktk Wilaya hiyo ni umasikini na ukosefu wa Elimu kwa wakazi wengi wa
Wilaya ya Pangani.

Yeye anakuwa mkuu wa Wilaya wa 21 toka kuanzishwa kwa Wilaya hiyo,na anasema mara baada ya kupangiwa kufanya kazi Wilaya hiyo watu wengi walimueleza kuwa anaenda kuongoza moja kati ya wilaya ngumu sana na iliyotopea kwa umasikini.

Ili kuendana na kasi ya maendeleo,Bi Zainabu ameamua kujikita katika elimu na hasa elimu ya mtoto wa kike,kwani katika eneo hilo elimu kwa watu na hasa mtoto wa kike imekuwa duni sana.Wilaya nzima ina shule za upili zipatazo 30's ambapo alipofika katika shule hizo zote,hapakuwepo na Shule yenye kidato cha tano na cha sita.

Amefanya juhudi za kuanzisha shule ya kidato cha tano na cha sita kwa kufanya upanuzi katika moja ya shule za Wilayani hapo.Miundo mbinu ni tatizo lingine,kwani wilaya hiyo haiunganishwi na maeneo muhimu kama jiji la Dsm.Umbali wa kutoka Pangani kwenda Handeni ni mrefu kuliko kutoka Pangani kwenda Dsm,lkn hakuna miundombinu inayounganisha Pangani na Dsm.

Kwa kushirikiana na mbunge Kijana wa Jimbo la Pangani,Mh.Zainabu A Iss amezindua wimbo wenye kuhamasisha elimu kwa mtoto wa kike ktk Wilaya ya Pangani,kwa kuwahimiza wazazi kutokuwaoza watoto wa kike wakiwa wadogo bali wawasisitize kupata elimu kwa lengo la kuondoa umasikini.

Hongera sana DC Zainabu .A. Issa,Kila la heri ktk kuwaletea wana Pangani maendeleo ya kweli.

Mbona anafanana na makamu wa rais??? Sio shangazi yake kweli??
 
Hii bongo ina vituko sana. Haya bna ajitahidi labda anaweza toa songi la mwaka 2020
 
Huyu alizunguka na mama samia suluhu kwenye campaign mwaka Jana watakuwa wana u karibu kindugu, na alisoma diploma Chuo cha kodi
Mi nakumbuka kuanza kumfahamu akiwa O'level kama sikosei Jangwani Sekondari.Kuna kipindi ITV kilikuwa kinarushwa Jpili mchana,kama "Debate" hivi...Huyu binti alikuwa akionekana sana akighani Mashairi,anaonekana ana uwezo mkubwa sana wa kukariri mambo.

Hiyo ilikuwa aeound 1999 to 2002,na hapo alikuwa kama sikosei form One au Two,sasa kusema sasa ana miaka 23,ina maana kipindi kile alikuwa ana miaka kumi akiwa Sekondari?
 
Mkuu 1999 alikuwa anasoma form one halafu leo ana miaka 23? kama ana miaka 23 alizaliwa mwaka 1993 ambapo 1999 alikuwa na miaka 6, 2002 alikuwa na miaka 9 na huyo hawezi kuwa mtoto wa sekondary
 
Mkuu 1999 alikuwa anasoma form one halafu leo ana miaka 23? kama ana miaka 23 alizaliwa mwaka 1993 ambapo 1999 alikuwa na miaka 6, 2002 alikuwa na miaka 9 na huyo hawezi kuwa mtoto wa sekondary
Yaani hapo hata mimi nimejaribu kutengeneza "Equation"....Nisaidie kui-balance
 
Mi nakumbuka kuanza kumfahamu akiwa O'level kama sikosei Jangwani Sekondari.Kuna kipindi ITV kilikuwa kinarushwa Jpili mchana,kama "Debate" hivi...Huyu binti alikuwa akionekana sana akighani Mashairi,anaonekana ana uwezo mkubwa sana wa kukariri mambo.

Hiyo ilikuwa aeound 1999 to 2002,na hapo alikuwa kama sikosei form One au Two,sasa kusema sasa ana miaka 23,ina maana kipindi kile alikuwa ana miaka kumi akiwa Sekondari?
Huyu atakua ameji Sitti Mtemvu aisee miaka hyo Niko primary hata sijafikiria secondary. Labda aliruka madarasa sana aisee kwa umri huo maana hana mda mrefu toka amalize diploma
 
Huyu atakua ameji Sitti Mtemvu aisee miaka hyo Niko primary hata sijafikiria secondary. Labda aliruka madarasa sana aisee kwa umri huo maana hana mda mrefu toka amalize diploma
Kwa kweli mimi namfahamu toka akiwa O'level,sasa hii ya miaka 23?hata mimi nimestuka.
Kuna kipindi kilikuwa ITV kikirushwa Jumapili mchana,nafikiri kilikuwa kabla ya TAMASHA LA MICHEZO la Captain Michael Maluwe!!Wanafunzi wa Dsm wakifanya kama "Debate" na kuonyeshwa na ITV
 
Mkumbuke Imekatazwa kuchukuana wa ccm na waupinzani ni marufuku wa ccm kwa ccm tu...- Msukuma

Ila Kazuri Shavu dodo mashallah... niliposoma mdogo nikajua anasoma shule bado kumbe turbo charger
 
Mbunge na mkuu wa wilaya ni vijana na wote wapo vizuri katika kujenga hoja tatizo lipo kwenye jamii wanayoiongeza bado haijitambui.
Ndugu acha matusi hatujielewi kivipi? Wao ndo hawajielewi maana wamekalili madesa lkn kwenye field ni empty
 
Huyu dogo nliona siku hiyo wanamfukuza na mawe kijiweni hadi noma,
Naona anataka kujirudi kivingine...any ways thats creativity

ILA NYIMBO NI MBAYAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Lengo sio kuuza copy za nyimbo, lengo Ujumbe ufike naona wamefanikiwa vizuri sana..
 
Udogo wake uko wapi? Mbona ana sura ya kizee hivyo?
Unajua hata mimi nilitaka kusema "Mbona kama jimama, au ndiyo habari za kujiachia achia mwili?"

Nikaona nishamaliza salio langu la kuanzisha kauli zisizo na staha kwa mwezi huu, lakini maadam ushaanzisha wewe, sishindwi kukuunga mkono.

Au ndiyo udogo wetu ule wa vyeti vya kina Mwigulu Nchemba aka Timu za Vijana za Nigeria, mtu ana cheti kinasema ana miaka 17 lakini ukimpima mifupa inaonesha ana miaka 27.

I hope not.
 
By the way kama anamiaka 23 kweli, basi alipaswa yeye kwanza arudi shule, kabla jakomaa ao wengine wasome.
 
Back
Top Bottom