DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Nawasalimu kwa jina JMT
Napenda nielekeze maoni yangu kwa DC mpya wa Gairo, mdogo wangu Jabiri M. Omari na nimzindushe kwamba wana gairo walinyanyaswa sana na yule dada. Nimepata kuzungumza na baadhi ya wananchi wa Gairo wakanieleza hili, kwamba yule dada hakuwa mstaarabu na wala hakua na mahusiano mema na wananchi, hivyo katika kazi uliyonayo mdogo wangu ni kurejesha imani ya wananchi kwa ofisi ya mkuu wa wilaya.
Nimeambiwa mtangulizi wako zilikua haziivi hata na MP wa hapo, hivyo hili lilikua ni tatizo kubwa. Nakuomba uyarekebishe hayo ili Gairo yetu ipige hatua kimaendeleo. Bado wana Gairo wanahitaji hospitali kubwa hako ka zahanati kalichopo hakakidhi haja za wananchi. Lakini pia suala la Administrative Block za utawala na nyumba maalumu ya DC lipewe kipaumbele.
Nakutakia utekelezaji mwema!
Kaka yako