DC Msando aagiza Mabasi yote yaondolewe stendi ya Magufuli, na kuyapeleka yadi kwao hata kama yana abiria

DC Msando aagiza Mabasi yote yaondolewe stendi ya Magufuli, na kuyapeleka yadi kwao hata kama yana abiria

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando ametoa akizo kwa wenye mabasi katika kituo kikuu cha Mabasi Magufuli kuondoa magari yao na kuyapeleka yadi kwao hata kama yana abiria.

Msando ametoa agizo hilo mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha mabasi kufuatia mgomo wa madereva wa mabasi unaoendelea wakipinga mfumo wa kukatwa pointi.



​
 
Kila mtu atambe kwenye ofisi yake😀😀Bado zamu yetu sisi boda boda wamezoea sana kututumia kwenye kampeni baada ya hapo wanatutupa kama toilet paper shenzi kabisa
 

Attachments

  • FB_IMG_1790683578013.jpg
    FB_IMG_1790683578013.jpg
    227.3 KB · Views: 13
Sio ziongezeke Bali zifutwe kabisa huo utaratibu unamminya sana dereva hebu chukulia dereva anatokea dar anaenda Kongo unategemea Hadi akifika tunduma anakuwa kabakiza point ngapi?
Zisifutwe, ziwekwe kwenye makosa ya uzembe, ovatake zisizo na msingi sehemu isiyoruhusu, speed isiyo na ulazima n.k
 
Sio ziongezeke Bali zifutwe kabisa huo utaratibu unamminya sana dereva hebu chukulia dereva anatokea dar anaenda Kongo unategemea Hadi akifika tunduma anakuwa kabakiza point ngapi?
Naomben mnieleweshe hizo pointing wanazipataje na ukiwa na nyingi eefect yake ni ipi na zikiwa chache effect yake ni ipi? Ponti ni mbadala wa faini au?
 
Zisifutwe, ziwekwe kwenye makosa ya uzembe, ovatake zisizo na msingi sehemu isiyoruhusu, speed isiyo na ulazima n.k
Walau hata ziwekwe huko Yani haiwezekani makosa mengine ni ya mmiliki wa gari lakini hao hawaguswi kwa sababu wengi wao wapo nao bungeni huko wanabaki kumuumiza dereva
 
Back
Top Bottom