The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitwapwaki Tukai ameliagiza Jeshi la polisi kumkamata na kumuweka ndani Abraham Lwakajunguti ambaye ni mkuu wa chuo cha mmDadini Lusu kilichopo wilayani Nzega kwa madai ya utovu wa nidhamu akishindwa kutoa majibu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati walipokua kwenye mkutano wa hadhara alipotakiwa kutoa maelezo juu ya kikundi cha watu wanaoingia kuchimba madini ya dhahabu kwenye eneo la chuo hicho bila kuwa na leseni halali.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Paul Chacha akaagiza mkuu huyo wa chuo aondolewe kwenye nafasi ya ukuu wa chuo hicho cha madini kutokana na utovu huo wa nidhamu.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Paul Chacha akaagiza mkuu huyo wa chuo aondolewe kwenye nafasi ya ukuu wa chuo hicho cha madini kutokana na utovu huo wa nidhamu.