DC Nzega aagiza kukamatwa kwa mkuu wa chuo cha madini kwa kumdharau RC Tabora

DC Nzega aagiza kukamatwa kwa mkuu wa chuo cha madini kwa kumdharau RC Tabora

Hahahaha unamuweka lockup kwa Sheria ipo?4 4
Kwahiyo ukimdharau RC au DC basi wanabaki kisheria yakukuweka lockup?

Zipo taratibu za kumuadhibu mtumishi mtovu wa nidhamu, hizo ndio taratibu?
Mkuu wa wilaya au wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa eneo lake ana mamlaka kikatiba ya kumhifadhi mtu yeyote isipokuwa mteule wa Rais tu kwa masaa 44
 
Huyu mkuu wa mkoa ni aina ya viongozi wanaopenda sana sifa na kuonekana wanafanya kazi sana na wanataka sana watokee kwenye vyombo vya habari. Wanasahau kuwa ukifanya kazi vizuri huna hata haja ya kuita media bali wananachi wenyewe unaowahudumia bila hata ya kuombwa watatangaza utendaji wako mzuri na taarifa zitafika kila kona ya nchi hii.
 
Mkuu wa wilaya au wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa eneo lake ana mamlaka kikatiba ya kumhifadhi mtu yeyote isipokuwa mteule wa Rais tu kwa masaa 44

Kwasababu hiyo anaweza kumuweka mtu ndani bila hata kosa lolote.

Kifungu kipi cha sheria kinampa hiyo mamlaka yakuweka mtu ndani bila sababu?.
Tofautisha utovu wa nidhamu na kuvunja Sheria.
 
Nilidhani haya mambo yameisha.Huyu Kasongo wa Tabora katoka wapi tena?! Mama kula kichwa huyu kabla jimbi hajawika.Hatutaki majitu maonevu,madhalilishaji,majuaji ,yenye mavurugu kwenye nchi yetu.Kama anapenda mambo hayo ya mavurugu apelekwe Goma,Bukavu au Bunia .
 
hivi sifa za ukuu wa mkoa na wilaya ni zipi

Ukose akili ya kutafakari, ubakie na akili ya kumsifia Rais tu.

Mtu pekee mwenye sifa hizo halafu hajapewa uDC ni Mwashambwa tu!! Wamemwonea sana. Amejitahidi kufuta akili yake yote, lakini hawajamwona.
 
UKosefu wa weledi kwa huyo DC na RC wake.
 
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitwapwaki Tukai ameliagiza Jeshi la polisi kumkamata na kumuweka ndani Abraham Lwakajunguti ambaye ni mkuu wa chuo cha mmDadini Lusu kilichopo wilayani Nzega kwa madai ya utovu wa nidhamu akishindwa kutoa majibu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati walipokua kwenye mkutano wa hadhara alipotakiwa kutoa maelezo juu ya kikundi cha watu wanaoingia kuchimba madini ya dhahabu kwenye eneo la chuo hicho bila kuwa na leseni halali.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Paul Chacha akaagiza mkuu huyo wa chuo aondolewe kwenye nafasi ya ukuu wa chuo hicho cha madini kutokana na utovu huo wa nidhamu.

View attachment 3242769
Huu ni ujinga na ulimbukeni wa madaraka
 
Acheni ushabiki, uruhusu watu wachimbe madini eneo la serikali bila vielelezo, halafu uendelee kw cheo chako! Yaani mkeo, agawe mbuzi/ ng'ombe kwa mtu pasipo ruhusa yako, halafu umhoji hakupi majibu, usimuelekeze aripoti kwa wazazi wake!

Sasa tukiishi kwenye jamii isiyo na utaratibu, tutakuwa na tofauti gani na nyumbu!
 
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitwapwaki Tukai ameliagiza Jeshi la polisi kumkamata na kumuweka ndani Abraham Lwakajunguti ambaye ni mkuu wa chuo cha mmDadini Lusu kilichopo wilayani Nzega kwa madai ya utovu wa nidhamu akishindwa kutoa majibu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati walipokua kwenye mkutano wa hadhara alipotakiwa kutoa maelezo juu ya kikundi cha watu wanaoingia kuchimba madini ya dhahabu kwenye eneo la chuo hicho bila kuwa na leseni halali.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Paul Chacha akaagiza mkuu huyo wa chuo aondolewe kwenye nafasi ya ukuu wa chuo hicho cha madini kutokana na utovu huo wa nidhamu.

View attachment 3242769
Hivi hizi nafasi watu wanazipataje?
 
Yani wakishamuweka ndani wanamshtaki kwa kosa gani na sheria ipi?
 
Mkuu wa wilaya au wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa eneo lake ana mamlaka kikatiba ya kumhifadhi mtu yeyote isipokuwa mteule wa Rais tu kwa masaa 44
Ujinga tu ,hii sheria inatumika vibaya , kama kiongozi unatakiwa sikiliza hoja , wenda mkuu wa chuo alikua na hoja za maana ,sasa unamkatisha mtu ajifika mpaka mwisho hii maana yake ni nini? na hapa zarau zipo wapi.

Uyo mkuu wa mkoa na wilaya waondolewe mara moja
 
Huyu mkuu wa mkoa atakua na shida, juzi kagombana na mtu wa GPSA leo tena mkuu wa shule. Ina maana wa kudharauliwa amekua yeye tu?
Kuna shida kubwa na RC Chacha, either ni psychopath au anaumwa asperger's sydrome. Anahitaji kuonana na madaktari wa magonjwa ya akili
 
Mtupe mamlaka ya DC na Rc kwenye kuvua watu kwenye nafasi zao
 
Back
Top Bottom