DC Nzega aagiza kukamatwa kwa mkuu wa chuo cha madini kwa kumdharau RC Tabora

DC Nzega aagiza kukamatwa kwa mkuu wa chuo cha madini kwa kumdharau RC Tabora

Huyu mkuu wa mkoa atakua na shida, juzi kagombana na mtu wa GPSA leo tena mkuu wa shule. Ina maana wa kudharauliwa amekua yeye tu?
Hajiamini, anadhani huo ukuu wa mkoa ndio kila kitu.Kwa hiyo kudhalilisha watu hivyo anahisi ndio anaonekana kufanya kazi. Tatizo wajinga wajinga hawa kupewa madaraka bila kujitambua.
 
Kwasababu hiyo anaweza kumuweka mtu ndani bila hata kosa lolote.

Kifungu kipi cha sheria kinampa hiyo mamlaka yakuweka mtu ndani bila sababu?.
Tofautisha utovu wa nidhamu na kuvunja Sheria.
katiba inamruhusu ambayo ndo sheria mama
 
Huyo chacha anavyoongea na sura yake anaonekana kuna mshipa haupo sawa kwenye ubongo
Alaf huyo madam kuna sehemu anamwambia "kama una uhakika na cheo chako sisi tuna uhakika zaidi" ana prove namna madaraka yanagawiwa kama pipi na watu fulani kwa watu fulani serikalini,
Ndio maana wote pamoja na mkuu wa mkoa wake wa mkoa kwa kutuonesha uwezo wao mdogo wamejiamulia kumuweka mtu ndani badala ya kuwasiliana na mwajiri wake ambaye wala sio serikali.
Foolishly .
 
Ujinga tu ,hii sheria inatumika vibaya , kama kiongozi unatakiwa sikiliza hoja , wenda mkuu wa chuo alikua na hoja za maana ,sasa unamkatisha mtu ajifika mpaka mwisho hii maana yake ni nini? na hapa zarau zipo wapi.

Uyo mkuu wa mkoa na wilaya waondolewe mara moja
ebu msikilize vizuri , ameulizwa anasema inawezekana , jibu gani la kumpa bosi wako?
 
Acheni ushabiki, uruhusu watu wachimbe madini eneo la serikali bila vielelezo, halafu uendelee kw cheo chako! Yaani mkeo, agawe mbuzi/ ng'ombe kwa mtu pasipo ruhusa yako, halafu umhoji hakupi majibu, usimuelekeze aripoti kwa wazazi wake!

Sasa tukiishi kwenye jamii isiyo na utaratibu, tutakuwa na tofauti gani na nyumbu!
Unaropoka wakati hujui chochote. Kuna mahali wamesema kuwa mkuu huyo ameruhusu watu kuchimba madini eneo la chuo?

Hicho chuo kipo ndani ya keseni ya utafiti madini, na kinaimiliki hiyo leseni kwaajili ya training ya wanachuo wake wa UDSM, sasa kuna watu wanaingia na kuchimba kwa kuiba, kwa akili yako ndogo, unataka mkuu huyo wa hiyo branch ya UDSM awepo kila eneo kulinda wakati wote? Basi huyo RC akamkamate Rais mstaafu Jakaya Kikwete, maana ndiye mkuu wa chuo.
 
Kati ya Wakuu wa Mikoa aliowateua Mhe. Rais, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ni kati ya Wakuu wa Mikoa wachache ambao ni wachapa kazi. Mhe. Chacha wasikukatishe tamaa. Chapa kazi.
 
Who is RC by the way? Akome kama alivyokoma kunyonya ziwa la mama yake.
 
Kati ya Wakuu wa Mikoa aliowateua Mhe. Rais, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ni kati ya Wakuu wa Mikoa wachache ambao ni wachapa kazi. Mhe. Chacha wasikukatishe tamaa. Chapa kazi.
mimi simjui in person lakini napenda sana anavyoweka discpline ya watumishi wa mkoa wake
 
Nijuavyo uteuzi wa mkuu wa chuo (kama ni cha seriali) unafanywa na Rais. Inashangaza mkuu wa mkoa/wilaya kumuagiza Rais atengue uteuzi wake. Nafikiri wa kutenguliwa ni wao kwa kosa la ‘insubordination’
Hicho siyo chuo kikui Wala taasisi ya elimu ya juu ni kikampasi Cha madini. Hivyo mkuu wa chuo ndiyo anakuteua.
 
Huyu mkuu wa mkoa atakua na shida, juzi kagombana na mtu wa GPSA leo tena mkuu wa shule. Ina maana wa kudharauliwa amekua yeye tu?
Huwa anawaprovoke watu kupitia madaraka yake wakati ni bogus fulani, hivyo watu wanampa ukweli wake. Kwakuwa tuna katiba mbovu, ndio analeta za unanjua mimi ni nani?
 
ebu msikilize vizuri , ameulizwa anasema inawezekana , jibu gani la kumpa bosi wako?
Ulitaka akubali kwa kitu ambacho hana huakika nacho? Mfano apo ulipo ukaulizwa jirani yako kauliwa na jirani yake na hujui ,je utatoa jibu gani.

Uyo mkuu wa mkoa alishindwa nini kumuita ofisin kwake kupata majibu sahii kabla kwenda kwenye huo mkutano.
 
RC/DC ni wapumbavu sn, wao ni mamlaka ya nidhamu ya huyo mkuu wa chuo? taratibu za kiutumishi zinasemaje?
 
Kwasababu hiyo anaweza kumuweka mtu ndani bila hata kosa lolote.

Kifungu kipi cha sheria kinampa hiyo mamlaka yakuweka mtu ndani bila sababu?.
Tofautisha utovu wa nidhamu na kuvunja Sheria.
Mkurugenzi wa Halmashauri, jiji, manispaa nk

Mtendaji wa kijiji au mtaa

Mtendaji kata nk

Ushangai kuwa wanaweza kukuweka ndani pia? Kwa sheria za mahakimu au mahakama, wamepewa nguvu hiyo ya kutekeleza hilo ktk maeneo yao

Kwa cheo cha walinzi wa amani
 
Unaropoka wakati hujui chochote. Kuna mahali wamesema kuwa mkuu huyo ameruhusu watu kuchimba madini eneo la chuo?

Hicho chuo kipo ndani ya keseni ya utafiti madini, na kinaimiliki hiyo leseni kwaajili ya training ya wanachuo wake wa UDSM, sasa kuna watu wanaingia na kuchimba kwa kuiba, kwa akili yako ndogo, unataka mkuu huyo wa hiyo branch ya UDSM awepo kila eneo kulinda wakati wote? Basi huyo RC akamkamate Rais mstaafu Jakaya Kikwete, maana ndiye mkuu wa chuo.
Yeye ni msimamizi wa shughuli zote ktk eneo hilo na anawajibika pia kwa lolote.
 
Back
Top Bottom