DC Pangani, Zainab Abdallah ana moyo wa pekee. Alimshauri mumewe kuongeza mke kutokana na yeye kuwa busy na majukumu

Si kweli, hiyo ni propaganda ya kukandamiza wanawake.
Kwa imani yako mkuu,siyo imani yetu.Mwanamke wa kiislamu mpaka kufua nguo za mumewe sio wajibu wake,mwanaume afue mwenyewe,na kama anafua mke basi kwa mapenzi kwa mume wake.Wanawake wakiislamu wanayofuraha kamili na hata kazi ngumu wasifanye,wapendwe,na kazi yao ngumu inatakiwa iwe pyumbu tu.
 
Hii imenikumbusha kuna dada mmoja dini sawa na DC aliwahi mshauri mumewe amuoe rafiki yake (rafiki wa mkewe) ili kumuepusha kuruka ruka hovyo, kwa maana alikuwa hajatulia, leo yupo na mwanaume huyu kesho yupo na yule. Mume nae akaridhia.
 
Wanawake wa namna hii ni wachache sana. Lakini haya mambo ya kuoa mke zaidi ya mmoja hayajaanza leo. Hata kwa Wakristo, Biblia imeonesha ni jinsi gani watu wa zamani walivyokuwa na mke zaidi ya mmoja na bado MUNGU alikuwa upande wao. Mfano mzuri na Yakobo(Israeli) na mfalme Daudi. Hawa walikuwa na wake wengi na bado MUNGU alikuwa anawabariki usiku na mchana. Ukisoma Biblia utaona jinsi wake za Yakobo walivyomruhu alale na "mahouse girl" wao pia tena bila kinyongo kabisa.

Mimi huwa nasema kuwa MUNGU huwa anajali sana kilicho ndani ya "roho" ya mtu na siyo mambo ya mwili kama kuwa na wake wangapi. MUNGU ni Roho, na yeye huangalia zaidi yale yaliyo ya "rohoni". Kama unampenda MUNGU kwa moyo wako wote na kuzishika "Amri" zake, basi hata kama utaoa wanawake 100 wala yeye hana shida. Pia ukisoma Amri zote za MUNGU hakuna hata moja inayokataza kuoa mke zaidi ya mmoja, hakuna, siyo kwenye agano la kale wala siyo kwenye agano jipya.
 
we nawe wa ajabu kumbe eeh?.
mbona mnakuwa na roho hiyo? hv hamjui kama nyie wanawake mko wengi zaid yetu wanaume..
sasa hao wengne wanaozagaa mitaani watapata wapi hifadhi kama si kuwaonea huruma kama hii ya bi Zainabu.
Vibaya hivyo...Simara
Jamani si ulitaka nikuoneshe msimamo wangu? matokeo yake unaniambia wa ajabu ha ha ha ha haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…