The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amemshauri msajili wa vyama vya wafanyakazi Tanzania kutathmini upya demokrasia ya uwanzishwaji wa vyama vingi vya wafanyakazi kwa kada moja kutokana uwepo wa athari unaopelekea ushindani usio na sababu
Wilman ametoa ushauri huo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha walimu Tanzania CWT halmashauri ya wilaya ya songea Mkoani Ruvuma uliofanyika katika ukumbi wa Anglican Songea ambapo amesema kuwa uwepo wa chama mbadala Cha walimu ambacho kinahudumia walimu wa serikali moja kinepelekea kuwa na ushindani na siyo kutetea haki na maslahi ya walimu.
Aidha Mkuu wa Wilaya huyo amesisitiza nidhamu kwa viongozi wa chama cha walimu na kuwataka kuheshimu mamlaka zilizowapa nafasi
Naye katibu wa chama cha Walimu CWT halmashauri ya wilaya ya Songea Adrian Ngairo ameishukuru Serikali kwa kupokea ombi la upandishaji wa madaraja ya walimu takribani 440 ambao wamepandishwa madaraja.
Ameongeza kuwa walimu 255 wa halmashauri ya songea wameondolewa katika chama cha walimu kwa kukukiuka sheria za chama hicho na wamebaki wanachama 1250.