Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya baadhi ya majengo ya Shule ya Sekondari ya Jenista Mhagama iliyopo Halmashauri ya Songea Mkoani Ruvuma kuungua kwa moto ikiwemo mabweni ya Wanafunzi wa kike pamoja na stoo ikidaiwa kuna hujuma, Serikali imeelezea juu ya tukio hilo...
Kusoma andiko la kwanza bofya hapa ~ Baadhi ya Majengo ya Shule ya Sekondari ya Jenista Mhagama yawaka moto, inadaiwa kuna hujuma
MKUU WA WILAYA AELEZEA
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile anasema “Moto huo umesababisha hasara kubwa, umeharibu majengo kadhaa, chakula cha Wanafunzi kimeteketea chenye thamani ya Sh. Milioni Moja, pia chakula kingine kilichosalia nacho hakipo katika mazingira mazuri kwa maana hiyo hakifai kutumika, pia magodoro, vifaa ya umeme navyo vimeungua.
Moto huo ulitoka mara tatu katika siku tatu tofauti, ulitokea Mei 31, 2025, Juni 1, 2025 na Juni 3, 2025.
Awali ilidaiwa kuwa ni Wananchi ndio wanafanya hivyo lakini Vyombo vya Dola vimechunguza na kubaini mhusika ni Mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika shule hiyohiyo, anaitwa Hamad Mushamu.
Mtuhumiwa huyo (Mwanafunzi) amekiri mwenyewe kuwa amechoma ili shule ifungwe, alisema amechoma ili shule hiyo ifungwe yeye apate muda wa kupumzika.
Ilipotokea moto mara ya kwanza kulifanyika kikao kujadili kilichotokea, Wazazi na Walimu waliposema kitu fulani hakijachomwa, baadaye Mwanafunzi huyo alienda akachoma tena hicho ambacho kilionekana hakijachomwa.
Alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa akishiriki vikao vya kujadili matukio ya moto, hivyo alikuwa anajua kinachotakiwa kuchomwa hadi Shule ifungwe.
Kwa sasa Mwanafunzi huyo ameshikiliwa na yupo chini ya ulinzi, anatarajiwa kupelekwa Mahakamani, tumezungumza na Wazazi wake nao pia wamesema mtoto wao ni mkorofi.
Masomo yanaendelea kama kawaida wakati hatua nyingine zikiendelea.