Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amelagiza Jeshi la Polisi la Wilaya ya Temeke kukamata Watu wote ndani ya Wilaya hiyo ambao wanapiga picha na kujirekodi video wakiwa na hela kwenye mitandao ya kijamii waseme hizo hela wametoa wapi na kodi wamelipa kiasi gani.
Amesema "Mtu akipiga picha na mahela mengi kuonesha maisha ni rahisi namna hii kama ni wa Temeke kamata, hakuna hela uliyoitolea jasho ina majigambo, hela uliyotolea jasho inafichwa kama ambavyo Mtu hasemi nimepata mshahara"
Amesema hayo Julai 10, 2024 akiongea na wakazi wa Mbagala juu ya mmomonyoko wa maadili na matukio ya kiuhalifu. Akisistiza kuwa wanaopost za hela huwashawishi vijana kujihusisha na madawa ya kulevya au ushirikina.