DC Temeke: Mtu akipiga Picha na hela akamatwe

DC Temeke: Mtu akipiga Picha na hela akamatwe

YAni matatizo yaliyojaa kwenye wilaya anayo tawala yamemshinda lakini bado anawapigia kelele watu wanaopiga picha na pesa zao anajua wamezipataje 🤔 na wakisha kamatwa watashitakiwa kwa kesi gani🤔 akitoka zake hapo anaenda kuimba mapambio ulaji unaendelea kuwepo 😅
 
Hiki cheo kitafutiwe kazi maalumu ya kueleweka.
Au kifutwe kabisa.

Sasa unamkamata mtu kakiuka sheria gani?

Halafu anasema eti hela inatakiwa ifichwe ,
Ndio huko CCM mnavyofundishana?
 
Kama wadau walivyopendekeza vyeo vya U DC na U RC vifutwe hawakukosea! Hawana kazi kabisa.
 
Hii ndio Taarifa mpya kutoka kwa DC wa Temeke Sixtus Mapunda, aliyoitoa kwa Wakazi wa Wilaya hiyo, bado hatujajua kama hicho nacho ni Kipaumbele cha maendeleo na wala hatujajua pia Sheria ambayo inavunjwa na vibopa hao wa mitandaoni, Pia hatukuambiwa kupost mwisho sh ngap ama hata kupost elfu 5 pia ni kosa.

Bali tunatoa wito kwa wote wenye kiherehere cha kufanya hivyo, akiwemo DOTTO MAGARI kwamba wasithubutu kuja Temeke, watadakwa kama kuku mwenye mdondo

Taarifa kamili hii hapa

View attachment 3038358View attachment 3038360
Kiuhalisia sio poa sema nae kimtindo zinamtoa udenda!
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amelagiza Jeshi la Polisi la Wilaya ya Temeke kukamata Watu wote ndani ya Wilaya hiyo ambao wanapiga picha na kujirekodi video wakiwa na hela kwenye mitandao ya kijamii waseme hizo hela wametoa wapi na kodi wamelipa kiasi gani.

Amesema "Mtu akipiga picha na mahela mengi kuonesha maisha ni rahisi namna hii kama ni wa Temeke kamata, hakuna hela uliyoitolea jasho ina majigambo, hela uliyotolea jasho inafichwa kama ambavyo Mtu hasemi nimepata mshahara"

Amesema hayo Julai 10, 2024 akiongea na wakazi wa Mbagala juu ya mmomonyoko wa maadili na matukio ya kiuhalifu. Akisistiza kuwa wanaopost za hela huwashawishi vijana kujihusisha na madawa ya kulevya au ushirikina.

Kupiga picha umeshika hela ni kujitoa fotokopi uwe na hela marambili, ni kosa kutengeneza pesa.
 
Hii ndio Taarifa mpya kutoka kwa DC wa Temeke Sixtus Mapunda, aliyoitoa kwa Wakazi wa Wilaya hiyo, bado hatujajua kama hicho nacho ni Kipaumbele cha maendeleo na wala hatujajua pia Sheria ambayo inavunjwa na vibopa hao wa mitandaoni, Pia hatukuambiwa kupost mwisho sh ngap ama hata kupost elfu 5 pia ni kosa.

Bali tunatoa wito kwa wote wenye kiherehere cha kufanya hivyo, akiwemo DOTTO MAGARI kwamba wasithubutu kuja Temeke, watadakwa kama kuku mwenye mdondo

Taarifa kamili hii hapa

View attachment 3038358View attachment 3038360
Hawa watu wanapataje hizi nafasi? Level of incompetence inatisha
 
Tuna tatizo la uongozi sana kila siku vituko tu mara utasikia mwingine anakamata sijui madada poa anavamia nyumba za kulala wageni anamtoa kila mteja na kumkamata!,mara mwingine anadai kwenye wilaya yake hataki sherehe za unyago! Huyu naye kaja na yake! Ipo siku watu watakatazwa kwenda kujisaidia muda wa kazi!
Maana mtu unajiuliza pesa yako umezitafuta mwenyewe sasa ukiamua kupiga picha nazo shida ipo wapi? Yaani hawa watu ni mahasidi sana na wana roho mbaya sana kwa sababu wao wakiona mtu amepata vihela kidogo wanaumia sana wanatamani watu wote wawe masikini tu ili tuendelee kuwa watumwa wao tu.
 
Sio ustaarabu kupiga hela na picha hadharani.
Unakuwa unajihatarisha usalama wako binafsi.
Huna escort unapiga picha na maburungutu ya pesa ukitekwa serikali ilaumiwe wakati wewe ndo umewashawishi wezi wakukabe.
Mkuu wa wilaya ndo Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama laZima adhibiti huu uhuni
 
Hii ndio Taarifa mpya kutoka kwa DC wa Temeke Sixtus Mapunda, aliyoitoa kwa Wakazi wa Wilaya hiyo, bado hatujajua kama hicho nacho ni Kipaumbele cha maendeleo na wala hatujajua pia Sheria ambayo inavunjwa na vibopa hao wa mitandaoni, Pia hatukuambiwa kupost mwisho sh ngap ama hata kupost elfu 5 pia ni kosa.

Bali tunatoa wito kwa wote wenye kiherehere cha kufanya hivyo, akiwemo DOTTO MAGARI kwamba wasithubutu kuja Temeke, watadakwa kama kuku mwenye mdondo

Taarifa kamili hii hapa

View attachment 3038358View attachment 3038360
wee kiherehere mwenzio kaleta uzi nawewe unaleta😕😕
mrembo kiherehere wewe😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom