DC Temeke: Mtu akipiga Picha na hela akamatwe

DC Temeke: Mtu akipiga Picha na hela akamatwe

Typical banana republic stuff!

Jitu linajiamkia tu na kutunga sheria zake lenyewe.

Tunaongozwa na majuha kuanzia juu kabisa mpaka huku chini.

Kama Rais wa nchi anaweza kusema sasa vyama vya siasa ni marufuku kufanya mikutano ya kisiasa halafu baadaye anakuja kusema ni rukhsa bila ya kuwa na mamlaka yoyote yale ya kufanya hivyo, nini kitachowazuia wateule wake kuamka na kujitungia sheria zao wao wenyewe?

Kesho mwingine anaweza akaibuka na kusema kwenye mkoa au wilaya yake ni marufuku kwa wanawake kukata viuno wakiwa wanacheza muziki.

Such pronouncements are par for the course for banana republics.
Mjinga mwingine huyu hapa FIU wana mamlaka ya kuuliza.
 
(ML) Money Laundering Act na sheria ya kodi kuna kitengo kipo pia cha (FIU) Financial Intelligence Unit wana mamlaka kisheria kuuliza umetoa wapi pesa. Maelezo lazima yanyooke. Lazima utuonyeshe biashara yako pia lazima utuambie kama kodi umelipa. Watanzania wengi akili hawana. Na uelewa ni finyu kama ww bwisye
DC ana gubu la kunyimwa kinyeo, akwende huko na masheria yake uchwara.

Tena ngoja nikarekodi video muda huu nione kama ataleta pua yake kuniuliza swali rorose.
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amelagiza Jeshi la Polisi la Wilaya ya Temeke kukamata Watu wote ndani ya Wilaya hiyo ambao wanapiga picha na kujirekodi video wakiwa na hela kwenye mitandao ya kijamii waseme hizo hela wametoa wapi na kodi wamelipa kiasi gani.

Amesema "Mtu akipiga picha na mahela mengi kuonesha maisha ni rahisi namna hii kama ni wa Temeke kamata, hakuna hela uliyoitolea jasho ina majigambo, hela uliyotolea jasho inafichwa kama ambavyo Mtu hasemi nimepata mshahara"

Amesema hayo Julai 10, 2024 akiongea na wakazi wa Mbagala juu ya mmomonyoko wa maadili na matukio ya kiuhalifu. Akisistiza kuwa wanaopost za hela huwashawishi vijana kujihusisha na madawa ya kulevya au ushirikina.

Kuna mwingine wa mkaa. Ni marufuku kubeba mkaa kwenye pikipiki
 
Kwani ni mtumishi wa serikali hadi umuulize katoa wapi? Na Akinunua gari kwa hizo pesa asipige nalo picha pia?
 
(ML) Money Laundering Act na sheria ya kodi kuna kitengo kipo pia cha (FIU) Financial Intelligence Unit wana mamlaka kisheria kuuliza umetoa wapi pesa. Maelezo lazima yanyooke. Lazima utuonyeshe biashara yako pia lazima utuambie kama kodi umelipa. Watanzania wengi akili hawana. Na uelewa ni finyu kama ww bwisye
Hawa wanamchunguza kwanza mtu na kujiridhisha kama kuna viashiria vya uvunjwaji wa sheria. hawakurupuku kama huyo dc kilaza alivosema kwamba mtu akipost picha na fedha anakamatwa.
Huyo dc mshamba na utakuta haelewi kabisa kuna vyombo hivyo ulivyovitaja vipo kazini24/7 vikiwa na utaalamu na nyenzo za kutosha kufanya kazi hizo.
Hivyo vyombo vinachunguza watu bila hata wao wenyewe kujua wanachunguzwa hata hao wapiga picha na hela vinawachunguza
Kila benk kuna maafisa vipenyo ambao kazi zao ni kuripoti miamala yote ya kiasi kikubwa ya fedha na inachunguzwa legity yake.
Viongozi wengi sasa hivi ni wakurupukaji na wala sio waelewa wanafanya mambo au wanatoa kauli ambazo zinawafanya waonekane kama nu watu wenye uelewa mdogo sana hadi inatia wasiwasi ameteuliwaje kwenye nafasi hiyo
 
Hiyo ndio kazi kiongozi anafanya?
Huwezi kumpangia mtu mzima aishije maisha yake,pesa ni yake shida iko wapi?
Kila mtu ajali mishe zake,na kila mtu aheshimu maamuzi ya mwingine endapo hajavunja sheria.
Wamefanyia kazi pesa zao let them be.
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amelagiza Jeshi la Polisi la Wilaya ya Temeke kukamata Watu wote ndani ya Wilaya hiyo ambao wanapiga picha na kujirekodi video wakiwa na hela kwenye mitandao ya kijamii waseme hizo hela wametoa wapi na kodi wamelipa kiasi gani.

Amesema "Mtu akipiga picha na mahela mengi kuonesha maisha ni rahisi namna hii kama ni wa Temeke kamata, hakuna hela uliyoitolea jasho ina majigambo, hela uliyotolea jasho inafichwa kama ambavyo Mtu hasemi nimepata mshahara"

Amesema hayo Julai 10, 2024 akiongea na wakazi wa Mbagala juu ya mmomonyoko wa maadili na matukio ya kiuhalifu. Akisistiza kuwa wanaopost za hela huwashawishi vijana kujihusisha na madawa ya kulevya au ushirikina.

Wakamatwe waekeze wamelipa kodi kiasi gani.Kama wamelipa kodi stahiki, waachiwe huru

Tena ilitakiwa sheria ziwe ngumu kweli kweli.Watu hawafanyi kazi halali,wanawaza wizi,utapeli, kuuza madawa ya kulevya na ushirikina wa kutoa kafara watu kwa sababu ya tamaa tu ya pesa wanayotamanishwa na watu wachache.
Wengine wanafanya hivyo ili DM wafatwe na vitoto vya 2000 na wanavichezea sana.
Huu uhuni ukomeshwe
 
Kuna maeneo wanapaswa kuwajibika ipasavyo ila siyo kwenye huu upuuzi.
Viongozi wapenda tension kwenye vitu visivyo na tija ila kufanya madini, mafuta na gas vitulete utajiri nchi aaaaah
 
Viongozi wetu wameshazisoma akili zetu kupenda mambo rahisi rahisi yaaiyokuwa na tija wala hata siwalaumu.

Ndio maana wanazungumza mambo ya kijinga maana hata sisi tunayapenda kuyasikia.

Ukiweka habari ya uvumbuzi wa kemikali fulani itapata wachangiaji wachache kuliko habari ya Zuchu kupata boyfriend mpya, au usajili mpya wa Yanga.
 
Kupiga picha na hela zako kunahujumu vipi uchumi?

Acheni ulofa nyie.
Wanachakaza pesa kwa kuzishikashika.
Pesa hutunzwa bank sio nyumbani maana wanahatarisha maisha yao
Pili wanasababisha sonona kwa wasio na hela kujiona masikini hivyo kupelekea kujinyonga au kufa kwa stress.
Naoendekeza adhabu kali kwa wahusika.
 
Back
Top Bottom