DC wa Ikungi: Tunachunguza tuhuma za Mwalimu wa Shule ya Mandimu (Singida) anayedaiwa kudhalilisha Wanafunzi

DC wa Ikungi: Tunachunguza tuhuma za Mwalimu wa Shule ya Mandimu (Singida) anayedaiwa kudhalilisha Wanafunzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mwanachama wa JamiiForums, aliandika kuhusu kinachondelea katika Shule ya Mandimu kuwa kuna Mwanafunzi ambaye anawadhalilisha Wanafunzi ikiwemo kuwapa adhabu kali kiasi cha kusababisha wengine waache Shule.

Shule hiyo inapatikana Kata ya Mungaa, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Serikali imesema kuwa suala hilo limefika kwao na linafuatiliwa kwa ukaribu.

Kusoma hoja ya Mwanachama, bofya hapa ~ Serikali imchunguze Mwalimu huyu wa Shule ya Mandimu (Singida), matendo yake ni tishio kwa Wanafunzi
Snapchat-2067079470 (1).jpg
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson
Akizungumza na JamiiForums, Apson amesema “Suala hilo limetufikia, nikaituma taarifa hiyo kwa Mkurugenzi na Afisa Elimu ambao wanashughulikia.

Nimeelekeza ufanyike uchunguzi ili kama ni jambo la kweli basi hatua zichukuliwe dhidi ya huyo Mwalimu kwa kuwa kuacha suala hilo lipite bila kufanya maamuzi linaweza kuathiri Jamii yetu.

Mbona sisi Viongizi hatupigi watu hata kama wanatukosea, kuna taratibu zinazotakiwa kufanyika, kwani kama ni kweli hapo pia kuna kosa la Jinai.
Snapinsta.app_464472406_8544548578956181_7690246347392947273_n_1080.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson

Nitoe pongezi tu kwa JamiiForums kwa kuibuka hoja kama hizo kwa kuwa zinasaidia Serikali na Mamlaka nyingine kutambua nini kinachozungumzwa na Wananchi.

Polisi nao wanaweza kuwa na nafasi yao ya kufanya uchunguzi wa suala hilo kwa kuwa linahusisha Jinai.

Hivyo, uchunguzi unafanyika na inawezekana kesho (Novemba 15, 2024) tukawa tumepata mrejesho wa kinachoendelea.
 
Kwa vyovyote vile huyo mwalimu hafai kuendelea kuhudumia jamii ya hapo, tayari hawana imani naye tena, pia hata usalama wake akibaki hapo ni questionable, hivyo nashauri hata uchunguzi ukionyesha kuwa mwalimu huyo hana kosa wamuhamishe tu,mwalimu anapaswa kuwa rafiki wa wqzazi na wanafunzi anaowahudumia, hivyo ikitokea amekuwa adui wa jamii basi atengwe na jamii hiyo.
 
Fact boss baada ya hili kubainika pia naomba kusafishwa kama nilivyochafuliwa
 
Back
Top Bottom