Pre GE2025 DC wa Kisarawe, Petro Magoti achangia Mifuko 300 ya Saruji Ujenzi wa bweli la Msikiti, ahimiza na wengine wachangie ili Watoto Warudi mapema kusoma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Binadamu mna nongwa, bila yeye kukifungia hicho kituo mpaka kesho hao madogo wangekua wanaliwa na mbu tu.

Magoti ni shujaa wa hilo, apongezwe.
Kwani hao madogo walianza jana kusoma?
 
Haka kajamaa kenye kibiongo kalikurupuka kakagusa dini ya wanaotawala kwa sasa!
Kaliposhituka, wenye dini Yao, wameenda kulia Lia kwa mtume wao pale magogoni, kakaona Bora kafanye juu chini, kapereke chochote msikitini, ndio hiyo cement,
ukikauliza, pesa ya kununulia hiyo cement imetoka kwenye bajeti ipi ya wilaya! Ilipangwa lini? Je huko ilipochukuliwa, nakisi italipwaje?
Upuuzi mtupu
 
Ndio uongozi huo kiongozi ana wadau wengi ni kuwaambia wadau na kuendesha harambe kwa kushirikisha jamii husika.
Na sio mambo ya amri amri tu unatatua changamoto baada ya kusikia changamoto zao.
Mazingira yakiwa magumu kiongozi unayafanya yawe rahisi.
 
Hata mzee mstaafu Mangula anamjua vizuri!
Ila jamani haya maisha sijui kama malaika wangekuwa wanatuandikia Obituary tukifa ili zisomwe hadharani watoto na ndugu zetu wangeficha wapi sura zao!
Alivyo mzee wa mikakati mikali siku ya utambulisho huko kisarawe kaonyesha familia ya mke tu yake kaificha!
 
Nadhani walianza muda mrefu, wamesoma kwa shida mpaka Magoti alipowaibua.
Mmh sio kweli neenda votuo vingi vya dini ya kiislamu viko hivo ata ukiweka ma bweni watoto wengi watapendelea kulala mskitini.......ni kutojua utamaduni wa dini ya kiislamu na mila zao ndo linalo msumbua magoti, watu wazima wanaacha majumba yao na kulala mskitini sembuse hao watoto wa madrasa.
 
Safi sana, Waislam mshindwe wenyewe sasa.

Mfanye mabweni ya kisasa na muweke majiko ya maana na wapishi, siyo mnawaweka wanafunzi kijinga jinga.
 
Kwahiyo hayo mazingira magumu yanawekwa kwa makusudi?
Malazi duni, watoto wa miaka 3 hadi 8 kujipikia na kulala mahala pabovu na kutoenda shule??

Na kama uliangalia hata yule sheikh alikiri kua amefanya kosa, na walikua na mipango ya kuboresha maana walishanunua matofali, walishafanya upembuzi yakinifu juu ya hilo bweni.
 
Kwani DC awe na huruma ya watoto wakiislamu kuliko wazazi wao wenyewe, aiche unafiki hapa k.koo kuna watoto zaidi ya 1000, hawana pa kuishi na pa kula....kwanini asikisanye hao kwanza.
 
Itakuwa wazee wenye busara wamemuweka chini wakamchana live ... Kuna watu wa kuwachezea unavyotaka lakini sio imani ya kiislam .. DC utafanye ziara za kushtukiza misikitini usiku wa manane
 
Kwani DC awe na huruma ya watoto wakiislamu kuliko wazazi wao wenyewe, aiche unafiki hapa k.koo kuna watoto zaidi ya 1000, hawana pa kuishi na pa kula....kwanini asikisanye hao kwanza.
Sasa huyo ni Dc wa huko kariakoo??

Ishu sio huruma ni je haki za mtoto zimefuatwa?
Mzazi yuko Tanga huko anajua hata mtoto wake ananala wapi?

Kila kitu mkiendelea kukiweka kwenye mlengo wa kidini, mtaishia kusema mnaonewa kila siku.
 
PAMOJA NA YOTE HAYA, LAKINI NI BUDI VITUO HIVI VIKAJULIKANA NA BAKWATA, NA HATA WAALIMU WAKE WAKAWA WANATAMBULIKA NA BAKWATA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…