Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani hao madogo walianza jana kusoma?Binadamu mna nongwa, bila yeye kukifungia hicho kituo mpaka kesho hao madogo wangekua wanaliwa na mbu tu.
Magoti ni shujaa wa hilo, apongezwe.
Haka kajamaa kenye kibiongo kalikurupuka kakagusa dini ya wanaotawala kwa sasa!Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti ametoa mifuko ya saruji 300 akianza kutanguliza mifuko 150 kwa ajili ya ujenzi wa bweni (hosteli) litakalotumika kwa ajili ya Watoto wanaopata mafunzo ya Dini ya Kiislamu Wilayani hapo ikiwa ni siku mbili tangu alipotoa maelekezo ya kusitishwa kulaza Watoto Msikitini hapo kutokana na mazingira kutokuwa rafiki ya kufundishia na kulaza watoto.
View attachment 3041341
Mifuko 150 imetolewa kwa Msikiti wa FALAF na Mifuko mingine 150 imetolewa kwa Msikiti wa Abdul-Aziz-Asharqiy, kwaajili ya Mabweni ili Watoto wasomee mazingira mazuri ambapo Misikiti yote ipo Kiluvya Madukani Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani
DC Magoti alifika eneo la tukio akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na kukuta Watoto 96 wapo kituoni hapo na kumuelekeza Sheikh wa Msikiti kusitisha huduma hiyo na kuagiza Watoto hao warejeshwe kwenye famili zao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, DC Magoti amesema:
Lengo kubwa la Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwa kila shughuli lazima tushirikishe viongozi wa dini, mimi nikiwa Msaidizi wake ngazi ya Wilaya, tulipopata taarifa kuhusu uwepo wa mazingira haya ambayo sio mazuri tukaona tuwatoe ili ufanyike utaratibu mzuri ili kuboresha mazingira.
Ikiwa Serikali inaweza kujenga miundombinu ya gharama kubwa kwa nini tushindwe kujenga hosteli nzuri na ya kisasa kwa faida ya Watoto wetu!
Baada ya kutoa maelekezo ya Watoto kuondolewa pale, kesho yake nilirejea eneo la tukio Usiku wa Saa Nne nikakuta utekelezaji umefanyika wa kuwaondoa Watoto hao.
Mimi naheshimu sana dini, natambua ndio inaleta upendo, mshikamano na viongozi wa dini mnafanya kazi kubwa sana.
Kwa leo kwa kuanzia, nimeleta mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa hosteli.
Wale wanaotaka kutuchonganisha tuwakemee na kuwataka nao waje kuchangia ili Ujenzi uishe mapema watoto waendelee na Masomo.
Mimi kama mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama ni jukumu langu kuangalia usalama wa Watu wote wa Kisarawe.
Niwaombe, lengo lenu ni zuri lakini twendeni kwa haraka ili tujenge hosteli ya kisasa na itakayokuwa na mazingira bora.
Pia soma: Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Hata hapo hapo msikitini wanaweza wakapata elimu zote hizo ya dini na hii ya kujua kusoma na kuandikaNi lazima hao watoto walelewe hapo msikitini kwanini wasipelekwe shule wakapate elimu watoe ujinga?
Alivyo mzee wa mikakati mikali siku ya utambulisho huko kisarawe kaonyesha familia ya mke tu yake kaificha!Hata mzee mstaafu Mangula anamjua vizuri!
Ila jamani haya maisha sijui kama malaika wangekuwa wanatuandikia Obituary tukifa ili zisomwe hadharani watoto na ndugu zetu wangeficha wapi sura zao!
Nadhani walianza muda mrefu, wamesoma kwa shida mpaka Magoti alipowaibua.Kwani hao madogo walianza jana kusoma?
Mmh sio kweli neenda votuo vingi vya dini ya kiislamu viko hivo ata ukiweka ma bweni watoto wengi watapendelea kulala mskitini.......ni kutojua utamaduni wa dini ya kiislamu na mila zao ndo linalo msumbua magoti, watu wazima wanaacha majumba yao na kulala mskitini sembuse hao watoto wa madrasa.Nadhani walianza muda mrefu, wamesoma kwa shida mpaka Magoti alipowaibua.
Kwahiyo hayo mazingira magumu yanawekwa kwa makusudi?Mmh sio kweli neenda votuo vingi vya dini ya kiislamu viko hivo ata ukiweka ma bweni watoto wengi watapendelea kulala mskitini.......ni kutojua utamaduni wa dini ya kiislamu na mila zao ndo linalo msumbua magoti, watu wazima wanaacha majumba yao na kulala mskitini sembuse hao watoto wa madrasa.
Kwani DC awe na huruma ya watoto wakiislamu kuliko wazazi wao wenyewe, aiche unafiki hapa k.koo kuna watoto zaidi ya 1000, hawana pa kuishi na pa kula....kwanini asikisanye hao kwanza.Kwahiyo hayo mazingira magumu yanawekwa kwa makusudi?
Malazi duni, watoto wa miaka 3 hadi 8 kujipikia na kulala mahala pabovu na kutoenda shule??
Na kama uliangalia hata yule sheikh alikiri kua amefanya kosa, na walikua na mipango ya kuboresha maana walishanunua matofali, walishafanya upembuzi yakinifu juu ya hilo bweni.
Kosa lake ni lipi ?Anajikosha!!! Hatudanganyiki. Msimamo wetu uko palepale
Sasa huyo ni Dc wa huko kariakoo??Kwani DC awe na huruma ya watoto wakiislamu kuliko wazazi wao wenyewe, aiche unafiki hapa k.koo kuna watoto zaidi ya 1000, hawana pa kuishi na pa kula....kwanini asikisanye hao kwanza.
Msikiti umesajiliwa kutoa elimu ya kawaida au ya dini?Hata hapo hapo msikitini wanaweza wakapata elimu zote hizo ya dini na hii ya kujua kusoma na kuandika
Zote thus inamiliki shuleMsikiti umesajiliwa kutoa elimu ya kawaida au ya dini?
Sasa si waboreshe wenyewe, RC huwa wanafanya wenyeweZote thus inamiliki shule
Tuwasaidie nao wawe na uwezo kama RCSasa si waboreshe wenyewe, RC huwa wanafanya wenyewe