Pre GE2025 DC wa Longido aliyesema alihusika kutengeneza mazingira ya Madiwani kushinda 2020 atenguliwa

Pre GE2025 DC wa Longido aliyesema alihusika kutengeneza mazingira ya Madiwani kushinda 2020 atenguliwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu DC, Nape na mwenzao Januari hawakusoma kile kitabu cha darasa la pili au la tatu "HERI MIMI SIJASEMA" jamaa walikwenda kujificha chini ya majani, kutoroka vita, maadui walipokuja wakawa wanakanyaga majani wakiwatafuta
Wa kwanza akasema "...mbona mnatukanyaga kama majani?" Adui akamdunga mkuki
Wa pili akamlaumu mwenzake akisema"...wewe acha ujinga kwanini unasema?" Adui akamdunga mkuki
Wa tatu akasema "...heri mimi sijasema?" Adui akamdunga mkuki
Wote wakafa
 
Halafu kaongea kwa kujigamba sana bila kujua anapanda mbegu ya chuki
 
Na yeye Samia alisema ukweli ndio maana hakuna aliyemfukuza.
Na wakati huo mtumbuaji ndio alikuwa anapenda kauli za kibabe kama hizo. Na aliongea hivyo ili kumfurahisha boss wake.
Tofauti ni kwamba, watendaji wengi wa serikali bado hawajamuelewa Samia au wanamdharau. Samia hapendi watu wanaojipiga kifua na kijimwambafai.
 
Samia anaweza kuwa Kiongozi mzuri tu kama akiachana na Siasa za kibabe.
Na kibaya ni kwamba hawezi kuacha siasa za kibabe kama ana mpango wa kugombea mwakani. Bila ubabe hawezi kushinda uchaguzi na wala hawezi kupata idadi ya wabunge watakaomuwezesha kuunda serikali.
 
Hata kama mmetengua uteuzi wake lakini Marco Ng’umbi kasema ukweli mchungu.

Kauthibitishia Umma mambo matatu-;

1. Kathibitisha kuwa Maccm hatakubaliki,

2. Kathibitisha kuwa maccm huwa yanaiba Kura,

3. Kathibitisha kuwa Serikali huwa inateka watu na kuwatupa kwenye mapori.View attachment 3084430
Amemuonea tu kwa sababu amesema ukweli mchungu.
 
Attachments

  • 5810871-156c33252d331784831e630b50148deb.mp4
    2 MB

Back
Top Bottom