DC wa Ubungo, Lazaro Twange azungumzia uhaba wa Maji na ubovu wa Barabara Kimara, asema kuna Mkandarasi amekimbia 'site'

DC wa Ubungo, Lazaro Twange azungumzia uhaba wa Maji na ubovu wa Barabara Kimara, asema kuna Mkandarasi amekimbia 'site'

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Jacob Twange amewataka wataalam wanaosimamia miundombinu ya barabara kufanya kazi kwa haraka na kukamilisha kwa wakati ili wananchi wapate huduma.

Mh. Twange ametoa maelekezo hayo katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto mabalimbali za wananchi , iliyofanyika Februari 11, 2025 katika kata ya Kimara.

"Lazima tuhakikishe tunakwenda na Kasi ili tuendane na muda miradi hii iishe kwa wakati, wananchi wapate huduma kwa haraka"

Akijibu baadhi ya hoja na changamoto za barabara zilizoibuliwa, Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Ubungo Mhandisi Lydia Machibya amesema barabara zinahudumiwa na TARURA ni barabara ya Kam College, Sisimizi, Victoria na barabara ya Lukuvi ambazo baadhi tayari zimetengewa fedha na wakandarasi wanaendelea na kazi.

Pia soma:
~
Hivi Mkandarasi anayejenga Barabara ya Kivulini - Kimara ameitelekeza Barabara? Imeharibika zaidi ya ilivyokuwa awali
~ Dawasa kwanini Hakuna Maji Maeneo ya Kimara, na hamtoi taarifa Yoyote
~ KERO - Wakazi wa Kimara Korogwe tumechoshwa na mgawo wa Maji, DAWASA mko wapi?
~ Wakazi wa Kimara na kata zake hawana maji zaidi ya wiki sasa, DAWASA hamuelezi maji yatatoka lini!
~ Maji yamekuwa adimu huku kwetu Kimara kuanzia Kibo, Baruti, Korogwe
 
Back
Top Bottom