DCI Boaz vipi, Mbona amekimbia kesi ya Mbowe?

DCI Boaz vipi, Mbona amekimbia kesi ya Mbowe?

Inaweza isifike hatua ya Mbowe na wenzake kujitetea kama mahakama (judge) itaona hakuna kesi ya kujibu. Kitu ambacho kiko very likely kutokea siku ya Ijumaa 18/02/2022. Hifadhi maneno yangu.

DCI mstaafu, CP Robert Boaz ndiye mtu wa kwanza kupokea taarifa kutoka kwa Lut Deus Leo Urio (kulingana na ushahidi wa Urio), huyu alikua mtu wa muhimu sana kuja mahakamani kuthibitisha taarifa zote za Urio kwenda kwake DCI. Huyu ndiye aliyemfikishia taarifa hizi ACP Ramadhan Kingai (kulingana na ushahidi uliokwisha kutolewa). Huyu ndiye alitoa maelekezo kwamba Lut Urio awe anaendelea kuwasiliana na watuhumiwa na kumpatia taarifa ACP Kinngai. Robert Boaz alikua ni mtu muhimu kukamilisha ushahidi wa kumfunga Mbowe na wenzake, lakini ushahidi wake tumeukosa. Bado unaweza kujenga hoja kwamba kuna watu watakua na kesi ya kujibu??

Mkuu, kuwa na mahaba ya kiasi.
Kwa bahati mbaya sana- kesi sheria nyingi hazionyeshi hivyo- majaji wengi hupendelea pamoja na mapungufu yote watuhumiwa wajibu tuhuma zao. Mnaogopa nini kama hamna hatia?
 
duh!
we jamaa ni fala sana
hivi unakumbuka kesi ya uhamsho ilivyokula hela nyingi zaidi ya miaka 8 na ule ulinzi ulivyokuwa?
Mwisho niambie hii kesi iliisha vp?
DPP alisema hana nia ya kuendelea na mashtaka
 
Leo upande wa mashtaka umefunga ghafla kesi ya ugaidi inayowahusu washtakiwa wanne akiwemo Freeman Mbowe.

Katika hali ya kushangaza shahidi muhimu ambaye akitajwa karibu kila siku na mashahidi wa upande wa serikali DCI Boaz hajaitwa mahakamani kutoa ushahidi.

Ikumbukwe huyu ndiye aliyepokea taarifa kutoka kwa Luteni Urio, juu ya kuwepo mipango ya ugaidi, na yeye aliye andaa mpango kazi wa awali wa kesi hii. Boaz alitakiwa kuja kuieleza mahakama ni kwa jinsi gani aliiona hii kesi ni ya ugaidi, alitakiwa kuunga mkono ushahidi wa Urio na kuthibitisha kwamba kweli Urio alifika ofisini kwake, maana hapo Kuna utata mkubwa, alitakiwa kuieleza mahakama ni kwa Nini alikubali mpango wa kuharibia maisha makomandoo watatu ambao walikuwa na kazi zao, warubuniwe na Urio kwamba Kuna kazi ya ulinzi VIP kumbe wanatumbukizwa shimoni na kubambikiwa ugaidi, kifupi bila Boaz kutoa ushahidi muunganiko wa kesi nzima unakosekana.

Hii haijatokea kwa bahati mbaya, pengine hii kesi ni mchongo hivyo kumleta DCI mahakamani na kudhalilishwa siku 3 mfululizo ni Kibatala itakuwa ni aibu kwa taifa, lakini majibu mazuri zaidi wanayo upande wa mashtaka.
Anaogopa kukiri uongo na hatimaye kuaibika.
 
Kama Jaji akijifanya hamnazo na akaamua kuwa hawa watu wanne "WANA KESI YA KUJIBU"...

Basi, iwe isiwe, wote waliokwepa kuja kutoa ushahidi kuthibitisha makosa ya washitakiwa kama waleta mashitaka [Jamhuri], then wajiandae kuwa mashahidi wa upande wa utetezi....

That means, hawajakikwepa kizimba cha mahakama. Na hata chief Hangaya kupitia kwa AG wake ajiandae kuja kujibu maswali kizimbani....

Mpaka hapo, one can easily predict what would be maamuzi sahihi ya Jaji Tiganga siku ya Ijumaa tarehe 18/2/2022 yatakuwaje...

To cut it short, ni kuwa, THE GAME IS OVER....!!
Duh! Wanaliona hilo? Short of that, tujiandae kutazama tamthilia tamu na safi. "Uongo njoo utamu kolea".
 
Jidanganye!
.
Mbowe anakula mvua 30 na hamna kitu mtafanya
Kwa hiyo ijumaa ndio anahukumiwa miaka 30!!! Halafu wakimfunga bei za vitu zitashuka??? Kweli uchawi Ni laana!mrudie Mungu bado hujachelewa.
 
Hakuna serikali ambayo ingekubali kuchezewa kirahisi vile na Mbowe. Kumbuka Chui Jike ndio alikuwa anaingia madarakani na Mbowe akaamsha dude la kudai katiba mpya. Ila jambo la muhimu hili la mama kusema uongo linaenda kumaliza yeye mwenyewe ndani ya chama chake. Ni laana kubwa kwa akina kingai kutesa na kuumiza watu ambao hawana hatia. Hii kesi napenda iendelee ili Moses Linjenje tujue yupo wapi.
 
Kwa bahati mbaya sana- kesi sheria nyingi hazionyeshi hivyo- majaji wengi hupendelea pamoja na mapungufu yote watuhumiwa wajibu tuhuma zao. Mnaogopa nini kama hamna hatia?
Mkuu, kabla mtuhumiwa (watuhumiwa) kujitetea, ni lazima hakimu au jaji aone ipo kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashitaka. Ikiwa ataona na kusema kuna kesi ya kujibu, watajitetea tu ndugu. Hawawezi kuanza kijitetea bila kuambiwa na jaji kwamba kuna hoja za kujitetea.

Na wakiruhusiwa kujitetea, aibu inayokwepwa hadi Robert Boaz anashindwa kufika mahakamani, itakuwa wazi. Judge ameondoa kipengele cha kutoa wasilisho kutoka mawakili upande wa utetezi ambalo walitaka walitoe kwa mdomo, ungependa mbona.

Mkuu, subiri Ijumaa utarudi hapa.
 
Kusema kweli uonevu, ukatili na ukandamizaji waliofanyiwa hawa binadamu wenzao hii laana itawaandama wao na watoto wao milele!
 
Kama Jaji akijifanya hamnazo na akaamua kuwa hawa watu wanne "WANA KESI YA KUJIBU"...

Basi, iwe isiwe, wote waliokwepa kuja kutoa ushahidi kuthibitisha makosa ya washitakiwa kama waleta mashitaka [Jamhuri], then wajiandae kuwa mashahidi wa upande wa utetezi....

That means, hawajakikwepa kizimba cha mahakama. Na hata chief Hangaya kupitia kwa AG wake ajiandae kuja kujibu maswali kizimbani....

Mpaka hapo, one can easily predict what would be maamuzi sahihi ya Jaji Tiganga siku ya Ijumaa tarehe 18/2/2022 yatakuwaje...

To cut it short, ni kuwa, THE GAME IS OVER....!!
Wanajifanyaga hamnazo.. wanaweza waendelee na aibu
 
Hangaya alijifanya ana akili kuliko mwendazake, mwisho wa kesi hii ndio mwanzo wa anguko la kasi la ccm.
kauli ya umma sio chokochoko.
Hangaya kama Makamba kama Msukuma kama Nape.Mmoja ana elimu ya hapa na pale na kujifanya ana masters wakati hajawahi kusoma chuo kikuu.Mwingine amepata udaktari wakati darasa la saba yaani mchngo wake kwa jamii umempatia PhD,mmoja aliiba NECTA form four akafutiwa matokeo akaresit Forest Morogoro na mwingine alipigwa IV ya 29 Nsumba sec.1997.Mambo kama Mambo kasoro kurungu.
 
Mkuu, kabla mtuhumiwa (watuhumiwa) kujitetea, ni lazima hakimu au jaji aone ipo kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashitaka. Ikiwa ataona na kusema kuna kesi ya kujibu, watajitetea tu ndugu. Hawawezi kuanza kijitetea bila kuambiwa na jaji kwamba kuna hoja za kujitetea.

Na wakiruhusiwa kujitetea, aibu inayokwepwa hadi Robert Boaz anashindwa kufika mahakamani, itakuwa wazi. Judge ameondoa kipengele cha kutoa wasilisho kutoka mawakili upande wa utetezi ambalo walitaka walitoe kwa mdomo, ungependa mbona.

Mkuu, subiri Ijumaa utarudi hapa.
Jaji amechoka na comedy za Kibatala ndiyo maana kamtolea nje.
Hata hivyo alitaka afanye hivyo kwa sheria ipi? KIFUNGU CHA 40 NA 41 cha sheria ya makosa ya uhujumu uchumi hiyo nafasi anayo jaji tu.
Na kama mpaka jana Kibatala na wenzake walikua hawajamshawishi jaji hata kama wakipewa miezi 3 hawana jipya.

“if you have left persuading the jury until the closing address - you’ve almost certainly lost. Successful persuasion, and persuading a jury in particular, is usually a gradual process”( Ian McClintock SC).

Mawakili wa serikali waliwashitukiza na itawachukua mda kutoka katika mshituko huo.
 
Sijui kwanini tunakubali kuhadaika kiurahisi hivi [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hiyo kesi haiwezi kuisha kiurahisi hivyo mark my words hawa watu watafungwa tu ingawaje ni ukweli mchungu ila watafungwa hii kesi imekaa vibaya hawawezi tumia gharama kubwa then wawaachie kiurahisi hivyo
Mahakama haihukumu bila ushahidi.Hakuna ushahidi wa usiotia shaka katika madai ya Jamuhuri,kumeet standard ya beyond reasonable doubt siyo hisia na maneno yasiyo corroborate na ushahidi mwingine.There is a latin maxim " Actus reus non facit reum nisi mens sit rea.Lazima kuwa na Nia ovu halafu tendo ovu ili jinai ithibitike bila kuacha shaka.Kama jaji Tiganga ataamua kudhalilisha mhimili wa mahakama na taaluma ya sheria muache atadhalilika yeye binafsi na yatampata makubwa kama sauli.
 
Mahakama haihukumu bila ushahidi.Hakuna ushahidi wa kuondoa shaka katika madai ya Jamuhuri,kumeet standard ya beyond reasonable doubt siyo hisia na maneno yasiyo corroborate na ushahidi mwingine.There is a latin maxim " Actus reus non facit reum nisi mens sit rea.Lazima kuwa na Nia ovu halafu tendon ovu ili jinai ithibitike bila kuacha shaka.Kama jaji Tiganga ataamua kudhalilisha mhimili wa mahakama na taaluma ya sheria muache atakuwa dhalilika yeye binafsi na yatampata makubwa kama sauli.
Mkuu acha ukasuku soma uelewe
ninakuwekea vifungu vilivyotumiwa na mawakili wa serikali na jaji kutufikisha hapa tulipo.

Dismissal of charge
40 At any stage of the proceedings the Court may, if satisfied that the accused person has no case to answer, dismiss the charge and acquit the accused person. [s.39] Procedure on close of case for the prosecution

41.-(1) Where after the prosecution closes it case the Court finds that the evidence for the prosecution establishes a case sufficient to require the accused person to defend himself against the economic offence charged, it shall so inform the accused person and require him to adduce evidence in his defence.

(2) Where the Court is satisfied that the evidence adduced by the prosecution up to the close of its case is not sufficient to found a conviction of the economic offence charged, but that it established a case in relation to a cognate offence which is an economic offence and for which the accused person may be convicted in the alternative, or if the case for the prosecution establishes other economic offences in addition to that charged, the Court shall inform the accused of its finding and require him to defend himself against the offence established by the prosecution instead of the offence charged, or against those other economic offences established by the evidence as well as the offence charged. (3) An accused person who elects to give evidence in his defence may do so either on oath or without taking the oath, but shall in either case be subject to cross-examination by the prosecution as well as the Court. (4) Where an accused person who is required to defend himself elects with no apparent excuse not to say anything and, in addition, not to call any witness or witnesses, an inference adverse to him may be drawn, and the Court as well as the prosecution may comment on his failure to give evidence in his defence.
 
Sijui kwanini tunakubali kuhadaika kiurahisi hivi 😀😀😀😀 hiyo kesi haiwezi kuisha kiurahisi hivyo mark my words hawa watu watafungwa tu ingawaje ni ukweli mchungu ila watafungwa hii kesi imekaa vibaya hawawezi tumia gharama kubwa then wawaachie kiurahisi hivyo
Watafungwa Kwa sababu wana hatia,au Kwa sababu ya gharama zilizotumika?ni lini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeanza kujali pesa ya Umma?
 
Hakuna serikali ambayo ingekubali kuchezewa kirahisi vile na Mbowe. Kumbuka Chui Jike ndio alikuwa anaingia madarakani na Mbowe akaamsha dude la kudai katiba mpya. Ila jambo la muhimu hili la mama kusema uongo linaenda kumaliza yeye mwenyewe ndani ya chama chake. Ni laana kubwa kwa akina kingai kutesa na kuumiza watu ambao hawana hatia. Hii kesi napenda iendelee ili Moses Linjenje tujue yupo wapi.
Moses lijenje yupo Dar tena ni mchungaji wa kanisa
 
Jaji amechoka na comedy za Kibatala ndiyo maana kamtolea nje.
Hata hivyo alitaka afanye hivyo kwa sheria ipi? KIFUNGU CHA 40 NA 41 cha sheria ya makosa ya uhujumu uchumi hiyo nafasi anayo jaji tu.
Na kama mpaka jana Kibatala na wenzake walikua hawajamshawishi jaji hata kama wakipewa miezi 3 hawana jipya.

“if you have left persuading the jury until the closing address - you’ve almost certainly lost. Successful persuasion, and persuading a jury in particular, is usually a gradual process”( Ian McClintock SC).

Mawakili wa serikali waliwashitukiza na itawachukua mda kutoka katika mshituko huo.
Na kingereza chako cha ugoko tar 18 mnalazwa na viatu. Save hii comment.

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom