Deal ya Ali Kiba na Sony: Makosa yanayojirudia..


Hebu ajiulize tu Vanilla Ice/ Mc Hammer/ Ja Rule/ DMX na wengineo wako wapi hivi sasa na wanafanya nini...
 


yale yale ukiwa na management mbovu lazima uteleze tu nakaya alikuwa na muda gani ktk game? unawezeje kusema zama zake zimekwisha? sugu na afande sele utawaitaje?
 
Mkuu nakusamehe bure kwakuwa hujui ulisemalo
 
Kumuona ambae haumpendi akipiga hatua mbele hua inaleta maumivu sana ndio maana sishangai vijana waliotoboa tunawatangazia kua ni drug dealers,Freemasons nk mara nyingi sisi wenye chuki hatukosi sababu za kumkosoa tusiempenda hasa akiwa anasonga mbele ndio faraja pekee kwetu tumejaa chuki,wivu na umaskini.
Nikutakie kila la heri kijana mpambanaji kwenye kusaka mafanikio na kamwe usiogope haters maana wapo kibao,Ali K walianza na menagement yako wakasema sana na leo watakomaa na ishu ya Sony ilimradi tu ukate tamaa acha kuangalia walioanguka wewe songa mbele Mungu akufanyie wepesi kwenye hustle zako na jitihada zako ndio njia ya mafanikio.
 

Una hakika?
 
Wabongo tumezoea kukurupuka hasa kwenye kusaini mikataba....wengi hawasomi mikataba na pia hawaielewi!!
 
Kaka najua unaongea ukweli sana ila sijajua kama hakuna msanii aliyefanikiwa akiwa na sony....kufanikiwa kwa mtu hakutokani na matokeo taliyopita ila ni kufanya kazi kwa bidiii.....ulichoongea kina ukweli sana sana ila huyu ni ali kiba nikumuombea kwa mungu afanikiwe ili wengine nao wafuate nyayo zake....ali kiba atatakiwa kufanya kazi bora sana sana....jambo la kuwa na sony ni its easy kufanya kolabo maana una status tayari na sony watakuunganisha vizuri.....hili deal linaweza kuwa na distribution ya kazi zake tu,videos na mauzo ya album
Dili bado halijajulikana sana so lets wait n see mambo yaliyopo sony navyojua hawa manage msanii. Msanii itakuwa bado yupo na management yake ila wao wanakukuza zaidi tu
 
Asante mkuu
 
Mi hata sikutegemea kukutana na haya!!!!! Mbona mpo ivyo nyie binadamu lakini? Hatakiwi afanye chochote yeye? Kila afanyalo anavutwa kurudishwa nyuma!? Kinawaumae? Basi riziki hupanga Mungu... Muacheni na maisha yake...
 
Hata Rose Muhando siku hizi avumi tena na ni baada ya kuingia mkataba na hao so called Sony...
Sijui alibweteka au ndio anavyosema mdau...hawana ujuzi wa ku market kama kina Babu Tale (kwi kwi kwi)
 

Mkuu "The Bold" kwa taarifa tu ni kwamba Sony BMG ilikuwa ni kampuni ya muziki (Music and Entertainment company) ambayo ilikuwa ikimilikiwa kwa ubia wa asilimia 50-50 kati ya Sony Corporation of America (SCA) na Bertelsmann AG (BMG). Kampuni hiyo ya Sony BMG ilianzishwa March 3, 2004 (Miaka 12 Iliyopita) lakini ilipofika tarehe 1/October/2008 (Miaka 7 iliyopita) Sony Corporation walinunua asilimia 50 ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa awali na Bertelsmann AG (BMG) na hivyo kuifanya Sony BMG kuwa chini ya Sony Coporation of America kwa asilimia 100 na jina lake kubadilika na kuwa Sony Music Entertainment (SME).

Ikumbukwe ya kwamba kampuni ya Sony BMG ilikuwa mmiliki wa recording labels mbalimbali kama vile Arista Records, Columbia Records, Epic Records, J Records, Mchenry Records, Jive Records, RCA Victor Records, RCA Records, Legacy Recordings, Sonic Wave America, na nyinginezo nyingi na hivyo, mabadiliko haya (Ya mwaka 2008) yaliathiri matawi yote ya Sony BMG duniani kote isipokuwa kwa Japan ambapo waliona kuwa mabadiliko ya aina hiyo yangepelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa ushindani katika sekta ya muziki wa nchi hiyo. Kwa maana hiyo Sony Music Entertainment Japan (SMEJ) ni tawi la Sony Music Entertainment (Iliyokuwa awali Sony BMG) lakini hufanya shughuli zake bila kuathiriwa na sera za Sony Music Entertainment of America ambayo ndiyo kampuni mama....

Hata ukiangalia kwenye list ya wasanii waliosainishwa chini ya Sony Music (fuata link hii https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Sony_Music_artists yapo majina ya wasanii wote ulimwenguni (e.g. Beyonce, Britney spears, Bow Wow, Avicii, drake, Alikiba na wengine wengi) ambao wako chini ya Sony Music.

Kwa mantiki hiyo, dili alilosaini Alikiba siyo kwa Africa pekee bali it’s a Global deal. MUNGU AMTANGULIE.
 
"So sijauona mkataba lakini naweza kuimagine skeleton yake ikoje" hapa ndo umeprove failure huwezi kuimagine kitu kilichokuzidi uwezo afu unasema upo karibu na music industry ukiwa kama nani producer,manager,dj,distributor,au una dili na mikataba ya wasanii? Si lazima kuweka ujuaji kwenye kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…