.......Kwanza kabisa kitu ambacho hawakielewi ni kuwa Ali hajasaini na Sony Music Ent. BMG (ishu yake sio 'global deal') bali amesaini na Sony Music Africa ambayo ni subsidiary ya Sony Music Entertainment!! Kwa ninavyoelewa Sony Music Africa wana sambaza mziki na kumanage wanamuziki ndani ya Africa pekee.. Sasa eidha Ali hajui alichosaini au chumvi inaongezwa kunogesha habari......
...
Mkuu "
The Bold" kwa taarifa tu ni kwamba Sony BMG ilikuwa ni kampuni ya muziki (Music and Entertainment company) ambayo ilikuwa ikimilikiwa kwa ubia wa asilimia 50-50 kati ya Sony Corporation of America (SCA) na Bertelsmann AG (BMG). Kampuni hiyo ya Sony BMG ilianzishwa March 3, 2004 (
Miaka 12 Iliyopita) lakini ilipofika tarehe 1/October/2008 (
Miaka 7 iliyopita) Sony Corporation walinunua asilimia 50 ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa awali na Bertelsmann AG (BMG) na hivyo kuifanya Sony BMG kuwa chini ya Sony Coporation of America kwa asilimia 100 na jina lake kubadilika na kuwa
Sony Music Entertainment (SME).
Ikumbukwe ya kwamba kampuni ya Sony BMG ilikuwa mmiliki wa recording labels mbalimbali kama vile
Arista Records, Columbia Records, Epic Records, J Records, Mchenry Records, Jive Records, RCA Victor Records, RCA Records, Legacy Recordings, Sonic Wave America, na nyinginezo nyingi na hivyo, mabadiliko haya (
Ya mwaka 2008) yaliathiri matawi yote ya Sony BMG duniani kote isipokuwa kwa Japan ambapo waliona kuwa mabadiliko ya aina hiyo yangepelekea kupunguza kwa kiasi kikubwa ushindani katika sekta ya muziki wa nchi hiyo. Kwa maana hiyo
Sony Music Entertainment Japan (SMEJ) ni tawi la Sony Music Entertainment (
Iliyokuwa awali Sony BMG) lakini hufanya shughuli zake bila kuathiriwa na sera za Sony Music Entertainment of America ambayo ndiyo kampuni mama....
Hata ukiangalia kwenye list ya wasanii waliosainishwa chini ya Sony Music (fuata link hii
https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_Sony_Music_artists yapo majina ya wasanii wote ulimwenguni (
e.g. Beyonce, Britney spears, Bow Wow, Avicii, drake, Alikiba na wengine wengi) ambao wako chini ya Sony Music.
Kwa mantiki hiyo, dili alilosaini Alikiba siyo kwa Africa pekee bali it’s a Global deal. MUNGU AMTANGULIE.