Debate: Kuajiriwa Vs Kujiajiri

Kujiajiri ingekuwa rahisi maccm yasingekuwa yanaiba kura na kuua watu ili yatangazwe mashindi.
 
Ni vizuri sana kujiweka kwenye position ya KUYAWEZA YOTE kwa wakati mmoja au tofauti,
Zote ni mbinu za utafutaji na zote zina mafanikio tegemea hali yako, mazingira husika, uwezo husika n,k

HAKUNA TOFAUTI ZA MSINGI KATI YA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI
Kama hakuna tofauti ya kuajiriwa na kujiajiri kwa nini watu wengi wenye mafanikio makubwa ni walio upande wa kujiajiri???
 

Usitenganishe wala kutofautisha kati ya kujiajiri na kuajiriwa vyote vinategemeana, na vyote ni muhimu, pia elimu ya chuo ya kuhitimu haikufanyi uchague ajira au uchague utavuna kipato kwa njia gani elimu ni msingi na ufunuo wa mambo mengi knowledge is power,

Ni vyema uajiriwe then ujiajiri yani ufanye vitu hivi kwa wakati mmoja au pia umalize kimoja uje kingine elimu yako iwe ya kuongeza ubunifu juu ya mambo hayo mawili,

Ukiajiriwa utapata mengi ili uje kujiajiri, ajira itakupa exposure, utapata mtaji na pia utafahamiana na wengi yani utajenga network ya watu, utajiri namba moja duniani ni kuwa na network, kwahiyo msidharau kuajiriwa ni vyema kutambua mambo haya ni yanakujengea kuja kuwa tajiri kama una malengo tu
 
Elimu sio lazima ikusadie, bali wewe ndiyo uisadie elimu sijui kama unanielewa lakini...
 
mjadala mzuri lakn wachangiaji wako kwenye zile nyuzi zetu pemdwa za ulishwahi kula tunda kimasiara... huku hawana habar nako..
Waache banah kila mmoja wetu ana vipaumbele vyake katika maisha, usifikie hatua kuwalazimisha watu waje kuchangia, mwingine yupo jf hapa akipata likes nyingi tu yeye kwake ni faraja, so wewe uliekuwepo hapa jadili mada,
 
Kuajiriwa ni Hulka ya mtu muoga na mvivu kimwili na kiakili na kujiajiri ni Hulka ya mtu mchapakazi na mwenye uwezo mkubwa kiakili na uthubutu wa kuona na kuzitumia fursa ipasavyo.. PERIOD!!

Kuajiriwa ni hulka ya mtu muoga? Mbona unapotosha watu, hivi mtu kamaliza chuo hana hata mtaji anaanzaje kujiajiri, na pia ni biashara chache sana nimeona zikifanikiwa mtu akope anaanza biashara, mikopo iwe ya kuongeza nguvu tu kwenye biashara
 
Kama hakuna tofauti ya kuajiriwa na kujiajiri kwa nini watu wengi wenye mafanikio makubwa ni walio upande wa kujiajiri???
Ni vile huwajui au sbb nchi yetu ni dhaifu sana kwenye UJASIRIAKAZI, hata UJASIRIAMALI nidhaifu

Nikupe mfano mmoja tu uliza mshahara wa CEO wa Safaricom then utafute matajiri wafanyabiashara wa kitanzania wenye kipato hicho,
 
Ni vile huwajui au sbb nchi yetu ni dhaifu sana kwenye UJASIRIAKAZI, hata UJASIRIAMALI nidhaifu

Nikupe mfano mmoja tu uliza mshahara wa CEO wa Safaricom then utafute matajiri wafanyabiashara wa kitanzania wenye kipato hicho,
Nimekuelewa mzee
 
Ni vile huwajui au sbb nchi yetu ni dhaifu sana kwenye UJASIRIAKAZI, hata UJASIRIAMALI nidhaifu

Nikupe mfano mmoja tu uliza mshahara wa CEO wa Safaricom then utafute matajiri wafanyabiashara wa kitanzania wenye kipato hicho,
Umewahi kujiuliza mwenye hiyo safaricom anaingiza shilingi ngapi kwa mwezi? Au unadhani safaricom haina mmiliki ?
 
Hapa kwa kuongezea nyama umeongelea discipline ya pesa katika jambo la matumizi, pia ni nguzo ya mafanikio, pesa unayotumia zaidi pasipo utunza na kuzalisha ni bure kutegemea kuona ni yenye tija
 
Kumbuka hili

Ukifa umeajiriwa watoto wako hawatarithi ajira yako ila ukifa una biashara watoto wako watarithi biashara zako.
Usiongelee kwa nadharia tu fikirisha pia wazo lako kivitendo.. Ni kwanini ajira yako ionekane inakuja kuwaandalia watoto wako urithi kwaninj urithi umeweka hapa katika kuchugua mkondo wa kipato yani uchague kujiajiri hata kama mambo yamegoma ili tu watoto waje kurithi,fanya na zalisha kitu unachoona utaweza kukujengea utajiri, swala la watoto wekeza snaa kwenye elimu yani fanya elimu iwe mrithi wa kwanza, tafuta shule zitakazo wajenga watoto wako waje kujitegemea na sio tegemezi kwenye mirathi yako, wazazi wengi tunaanguka hapa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…