Debate: Kuajiriwa Vs Kujiajiri

Vitabu vya aina gani kwa mfano
Mi ni mwajiriwa ila ninawekeza kwenye kilimo (miti ya matunda)
Maarifa yangu napata sanaa kutoka kwa Robert Koyasaki.
Anavitabu vingi sanaa vimenifungua mfano, Rich Dad Poor Dad, Before you Quit your Job na Financial quadrants.

Vitabu vyake vimenifungua sanaa.

#YNWA
 
Kama hakuna tofauti ya kuajiriwa na kujiajiri kwa nini watu wengi wenye mafanikio makubwa ni walio upande wa kujiajiri???
mishahara ina limit ila mapato ya kujiajiri hayana limit.
Huwezi kuajiriwa ukalipwa mshahara wa milioni 500 kwa mwezi ila aliyejiajiri ana uwezo wa kuipata hiyo kwa mwezi kutegemea na ukubwa wa biashara yake
 
Kuamua KUAJIRIWA au KUJIAJIRI, ni wazo la kufikirisha na kutukumbusha jinsi ya kuamua kwa busara kulingana na wakati na hali ya mtu kimaisha, hususan uwezo binafsi, mahusiano (connections), mazingira na mtaji.

Mbali na mshahara, ajira inakupa mtaji, uzoefu na mahusiano fulani kabla ya kuamua kujiajiri. Aidha, ukiugua au kupata tatizo lolote, mshahara unabaki palepale, yakiwemo mafao ya kuacha ajira au kuzeeka.

Dosari kubwa ya kuajiriwa ni kukosa uhuru wa kujiamulia binafsi. Pia masharti ni mengi ambayo yakikiukwa unaweza kupoteza ajira.

Raha ya kujiajiri ni uhuru wa kufanya maamuzi binafsi muda wowote pasipo ruhusa au kibali cha mtu yeyote yule. Ila, ili ufanikiwe unahitaji uwe na uvumilivu, nidhamu ya kazi na matumizi ya fedha, kujifunza kila wakati, kutokata tamaa na kutozembea na/au kuepuka uvivu.

Pamoja na maelezo haya, siku hizi watu wanafanya yote, wanaajiriwa bila kuacha kujiajiri kwa kuwa na kazi au biashara binafsi pembeni. Mwishowe waajiriwa wote nao huishia kujiajiri maana kuna kustaafu au kuachishwa ajira.

Kwa muhtasari, ifuatayo ni orodha ya nguzo za mitaji ya mafanikio katika maisha:

1. Afya Njema
2. Wazo au fikra pevu
3. Vipaji
4. Rasilimali asili (ardhi, maji, madini, nk)
5. Elimu/maarifa
6. Teknolojia
7. Mahusiano mema
8. Matumizi bora au sahihi ya muda.

Hayo ndiyo huwaletea watu mafanikio makubwa katika maisha (zikiwemo pesa), wawe wameajiriwa au kujiajri.

Na tukumbuke kuwa pesa ni matokeo, si mtaji. Mtaji halisi ni hizo nguzo! Nina mada mahsusi kwa kila nguzo.
 
Ivi unapokuwa unasema elimu yetu haitufundishi ku seize opportunities unakuwa una compare na elimu ipi??? maana sisi mfumo wetu wa elimu tumeucopy kutoka kwenye developed country mbona wao wana move forwad

may be sijakuelewa!!!!
Sasa hapo ndo utofauti ulipo tunasoma yaliyofanywa na yanayofanywa na watu wenye uchumi mkubwa na wanasoma maarifa walionayo kwenye mazingira na wamendeleza wao wenyewe kutoka vizaz na vizaz. Sasa waafrica tunashupaza shingo kujaziana mitahara nakati hata uchumi wakufanyia demo darasani hamna.

Mm nilivyokua secondary nilikua najiulizi Kama huwezi ona hata application ya electrolysis mtaani hata. Lakini ukirudi shule unakuta vijana wako busy wanasolve maswali yakila aina ili mradi waende ud kusoma engineering na Mambo kibao. Kana kwamba wakimaliza ud ukweli utabadilika
 
Hongera kwa muamuzi yako mkuu,natumai umeshafika mbali sasa hivi.
 
Watu wanaojiajiri kwa kawaida huwa wanauwezo mkubwa wa kifikra na kupambanua mambo mbali mbali,

ikiwemo kivipi aikuze biashara yake aibrand na apate faida na asipate asala, tofauti na watu walioajiriwa mara nyingi kuuchemsha ubongo wake huwa ni mtihani,

na mara nyingi watu hawa hata wakianzisha biashara huwa haiendelei kwa kukosa mtu mbunifu na mchemshaji ubongo wake,

but all in all wote hufanikiwa katika maisha japokuwa mfanyabiashara aliyekuwa serious hufanikiwa zaidi.
 
Horrible life[emoji36][emoji36]

Fuvk off

Ngoja nisake mitaji nitakapodumbukia Mungu tu anajua!
 
Congrats![emoji122][emoji122]

Au ujenge myumba/ apartments za kupangisha at least ndo utakula hela mwajiriwa

Mwajiriwa mwajiriwa aaaaaaugh! I hate this word, ni masikini sana asee labda uwe mwizii[emoji848]
 
Unanipa mzuka we jamaa!

Mama ako typical na mama angu[emoji1787][emoji1787]
 
watumishi wa serikali miaka mitano hawana annual increament. wameongezewa makato ya bodi ya mkopo kutoka 8% mpaka 15%. Bora mfanyabiashara anaweza kwa namna flani kukwepa kodi ila muajiriwa huwezi kukwepa kodi za serikali
Very true[emoji848]
 
Upo sahihi sana japo umesahau kuiinclude powerbank kutoka kwa wataalamu.
 
Maarifa yamefichwa kwenye vitabu soma vitabu.
Hakuna maarifa yaliyofichwa kwenye kitabu mzee, kila siku nalipinga hili.

Niambie hapa nani kaficha maarifa kati hawa:

Wa kwanza ni mtu mmoja mwenye maarifa kachukua karatasi, kayaandika maarifa yale af akayachapisha na kuyasambaza ili kila mtu aweze kuyapata,kwa mabadilishano ya pesa kidogo. Na nakala hizo zaweza kuwepo miaka na miaka au

Wa pili mwenye maarifa ila kabunda nayo bila kusambaza popote mpaka umauti unamkuta.
 
Naona kila mtu anasifia kujiajiri. Naombeni muelewe tunaojiajiri tunapata changangomoto nyingi sana.siku hazifanani kuna siku unapata sanaa na maanisha faida ila kuna siku unaingia a big loss mpaka unajuta.

Natolea mfano wangu ninajikita na biashara ya ufugaji , kunakipindi soko linakuwa Zuri ila kuna kipindi unapata hasara soko sio Zuri au pale ambapo umeingiwa ugonjwa inafika wakati vifo vinatokea ndio hapo mtaji unakataa.omba usipatwe na ugonjwa usiotibika ni hasara...

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…