Debate: Kuajiriwa Vs Kujiajiri

kwa io kama nimeajiriwa na mm nikaajiri vijana sita wa bajaji je bado sitatajirika??
Ukionyesha tu dalili ya kutajirika mara pap barua mezani unatakiwa ukaripoti eneo jipya la kazi nanguruwe huko mtwara na huku nyuma vijana wa bajaji wanafanya yao mjini, biashara yoyote ili ifanikiwe wewe uwe wa kwanza kutia mguu
 
Na ndo mana MO alianza na unga wa ngano lakn sa hv anatengeneza mpak pipi Ukiachilia mbali tambi, tanuka Mzee Baba , loss ikitembea upande huu , faida inaingia upande wa pili , kujiajiri akli inatakiwa iwe active 24 hrs
 
mfanyabiashara anajibana sanaa hana matumizi ya hovyo akiwaza kuendeleza biashara yake..huku mfanyakazi akitumia anajua kitaingia tu mwisho wa mwezi
 
100% correct! Watu wanawahimiza 'wasomi' wajiajiri lakini hili sio jambo rahisi kwao kulingana na elimu inayotolewa mashuleni/vyuoni
 
Utapata maelezo mengi sana lakini shika haya ya muhimu maana nimepita kote.

Kuajiriwa: Kuna hofu ya kukosa kazi,kupata kesi,kufungwa au kufukuzwa ukiwa huna cha kuanzia,kufokewa na kusimamiwa na mtu kama mtoto wako,kukosa uhuru

2. Kujiajiri: haijalishi kunahitaji bidii na maarifa mengi sana ila kubwa hapo kwa mtu husika ni AMANI ktk mambo binafsi.

Kwisha
 
Umeweka elimu kama chanzo cha mafanikio,kitu ambacho siyo kweli

Nje na kuwaza mitaala, hata wewe waza matajiri waliopo hapa nchini,siyo walioacha shule wakiwa vyuo,hawakusoma kabisa.

So usiwe na mifano ya watu wa mataifa mengine huko kwenye mbinu za namna zao na si za kiafrika
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Mamy , we live only once , kila sekunde ni ya thaman Sana, na ikisepa imesepa huku unaelekea umri wa kufunga mahesabu[emoji16]
We acha tu[emoji848]
 
Kuajiriwa ni Hulka ya mtu muoga na mvivu kimwili na kiakili na kujiajiri ni Hulka ya mtu mchapakazi na mwenye uwezo mkubwa kiakili na uthubutu wa kuona na kuzitumia fursa ipasavyo.. PERIOD!!
We mwehu nini unawaona waliojiriwa waoga na wavivu wakati ukianzisha hicho kibiashara chako unataka uajiri watu utaajirije watu unaowaona wavivu pumba kabisa
 
Kuna mkuu amesema kuwa akiajiri watu 6 kwaajiri ya kumuendeshea bajaji atatajirika ila watu wamembishia na wengine wamemuuliza yani utajirike kwa bajaji?

Ngoja tufanye hesabu:

kwasiku bajaji wanapeleka 25 kwaboss, nje ya service na hela ya wao kula 25000 x 6 = 150,000 hivyo kwasiku anakuwa na 150,000

Then 150000 x 30 inakuwa 4,500,000

Kwamwezi boss anakuwa na mil 4 na laki 5 hapa kuna waajiriwa wengi wanasubiri sana kwahuyu mtu......ukisema kunakukamatwa na mambo mengine basi jua wanalipia mambo ya muhimu mapema bajaji inakuwa Safe kufanya kazi.....pia hata bajaji akipiga 40 basi 25 yangu ailete nyumbani bado faida nitapata kubwa tu.....
 
Kujiajiri ni kuzuri kwasababu unajiwekea malengo binafsi ambayo wewe utafanya kazi ili uyatimize.....

ila ukijiajiri ni ngumu kuweza kuwa na kipato huru maana pesa yote itaishia kwenye kula, usafiri na familia.....

yani mshahara wetu kibongobongo nikwaajiri ya kula tu na kulipia makazi ili tufanye kazi ya serikali au maboss tukiwa wazima.....

Pia uwepo wa makato unaumiza sana waajiriwa yani mtu baada ya makato unakuwa na laki 4 tu au laki 5 hapo mwenye biashara ndogo tu kama ya kuuza viatu vya kike anaweza kukufikia na kukupita kwa mapato kiurahisi tu....
 
Mjadala mzuri lakn wachangiaji wako kwenye zile nyuzi zetu pemdwa za ulishwahi kula tunda kimasiara... huku hawana habar nako..
Mjadala mzuri kwako mkuu, huo mwingine ni mzuri kwao ndo maana wako bize nao

Mchango wako kwenye huu uzi ni upi, tunakusubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…