Debate: Kuajiriwa Vs Kujiajiri

Debate: Kuajiriwa Vs Kujiajiri

kwa io kama nimeajiriwa na mm nikaajiri vijana sita wa bajaji je bado sitatajirika??
Ukionyesha tu dalili ya kutajirika mara pap barua mezani unatakiwa ukaripoti eneo jipya la kazi nanguruwe huko mtwara na huku nyuma vijana wa bajaji wanafanya yao mjini, biashara yoyote ili ifanikiwe wewe uwe wa kwanza kutia mguu
 
Naona kila mtu anasifia kujiajiri. Naombeni muelewe tunaojiajiri tunapata changangomoto nyingi sana.siku hazifanani kuna siku unapata sanaa na maanisha faida ila kuna siku unaingia a big loss mpaka unajuta.
Natolea mfano wangu ninajikita na biashara ya ufugaji , kunakipindi soko linakuwa Zuri ila kuna kipindi unapata hasara soko sio Zuri au pale ambapo umeingiwa ugonjwa inafika wakati vifo vinatokea ndio hapo mtaji unakataa.omba usipatwe na ugonjwa usiotibika ni hasara...

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
Na ndo mana MO alianza na unga wa ngano lakn sa hv anatengeneza mpak pipi Ukiachilia mbali tambi, tanuka Mzee Baba , loss ikitembea upande huu , faida inaingia upande wa pili , kujiajiri akli inatakiwa iwe active 24 hrs
 
Mfanyabiashara anayepata Faida TZS 1,500,000/- na mwajiriwa anayepata mshahara TZS 1,500,000/- hawana tofauti ya mapato kwa mwezi. Issue ni matumizi ya Faida wanayopata kwa mwezi. Hilo Moja!

Jambo la pili namna kila mmoja anajiongeza kujazia kipato. Mfanyabiashara kukuza biashara yake na mwajiriwa kuwa na kipato Cha ziada. Then tunarejea pale pale, matumizi yakoje?

Ima tuweke Hili jedwali yaishe!
______&&&&&:&&Kipato. Matumizi
Mfanyabiashara
Mwajiriwa
mfanyabiashara anajibana sanaa hana matumizi ya hovyo akiwaza kuendeleza biashara yake..huku mfanyakazi akitumia anajua kitaingia tu mwisho wa mwezi
 
Elimu ni msingi wa mambo mengi muhimu, japo kuna watakaosema huhitaji elimu kuwa mfanya biashara lakini mifano hai niliyonayo, wafanya biashara wakubwa duniani kama Bill Gate na Microsoft, Marck Zuckerbergs na Facebook walipata mawazo ya biashara wakiwa ni wanafunzi wa elimu ya juu. Elimu yetu ni kinadharia sana kuliko vitendo.

Kijana aliyeanzisha New Convert Garden Soup, alikua ni mwanafunzi wa Biashara katika chuo kikuu cha Oxford. Hii ilikua project ya shule aliyopewa akiwa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu.
Tuangalie kwanza ufundishaji wa mitaala yetu ni wapi tunakosea.
100% correct! Watu wanawahimiza 'wasomi' wajiajiri lakini hili sio jambo rahisi kwao kulingana na elimu inayotolewa mashuleni/vyuoni
 
Good wish to all

Moja ya definition ya maisha ni mapambano na moja ya definition ya mafanikio ni ushindi,

Nilikuwa natafakari kitu nikasema ngoja nishare na home of great thinker. Dunia ya sasa watu wengi sana tunahimizwa kujiajiri hasa kipindi hiki cha tatizo la kidunia la ajira.

Hoja yangu, wapo watu wameajiriwa serikalini na sekta binafsi na wanalipwa mshahara mzuri tu may be 3m ambao kwa tz unaweza ukaishi vizuri sana wanahimizwa wajiajiri ambapo kwenye upande wa kujiajiri ni biashara chache sana zinaweza kukupa pato hilo kwa mwezi kama faida na tena sio uhakika. Na kwa nn mtu akiamua kuajiriwa na akatumia sehemu ya kipato chake kujiajiri wengi wao huwa wanapitwa mafanikio na watu waliocha ajira na wakajiajiri completely. Kuna siri gani katika ulimwengu wa kujiajiri ambao unamtaka mhusika awe direct involve kwenye hicho alichojiajiri na mafanikio yake.

Au kujiajiri ni overarated?
Au kuajiriwa ni underated? or it depend with month salary?
Kuna siri gani iliyojificha nyuma ya kujiajiri ambayo ni msingi wa mafanikio. Kuna mtu aliacha kazi yenye mshahara wa 6m plus bonus akaenda kujiajiri.
Je mishahara ya kwa mwezi na faida za kwenye biashara zote zikiwa sawa nini kitatokea Nani atakuwa amewin na nani atakuwa amelose.
Mlioacha kazi na mkajiajiri tupeni hizo siri na sisi tufanikiwe.

Help me guyz
Utapata maelezo mengi sana lakini shika haya ya muhimu maana nimepita kote.

Kuajiriwa: Kuna hofu ya kukosa kazi,kupata kesi,kufungwa au kufukuzwa ukiwa huna cha kuanzia,kufokewa na kusimamiwa na mtu kama mtoto wako,kukosa uhuru

2. Kujiajiri: haijalishi kunahitaji bidii na maarifa mengi sana ila kubwa hapo kwa mtu husika ni AMANI ktk mambo binafsi.

Kwisha
 
Elimu ni msingi wa mambo mengi muhimu, japo kuna watakaosema huhitaji elimu kuwa mfanya biashara lakini mifano hai niliyonayo, wafanya biashara wakubwa duniani kama Bill Gate na Microsoft, Marck Zuckerbergs na Facebook walipata mawazo ya biashara wakiwa ni wanafunzi wa elimu ya juu. Elimu yetu ni kinadharia sana kuliko vitendo.

Kijana aliyeanzisha New Convert Garden Soup, alikua ni mwanafunzi wa Biashara katika chuo kikuu cha Oxford. Hii ilikua project ya shule aliyopewa akiwa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu.
Tuangalie kwanza ufundishaji wa mitaala yetu ni wapi tunakosea.
Umeweka elimu kama chanzo cha mafanikio,kitu ambacho siyo kweli

Nje na kuwaza mitaala, hata wewe waza matajiri waliopo hapa nchini,siyo walioacha shule wakiwa vyuo,hawakusoma kabisa.

So usiwe na mifano ya watu wa mataifa mengine huko kwenye mbinu za namna zao na si za kiafrika
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Mamy , we live only once , kila sekunde ni ya thaman Sana, na ikisepa imesepa huku unaelekea umri wa kufunga mahesabu[emoji16]
We acha tu[emoji848]
 
Kuajiriwa ni Hulka ya mtu muoga na mvivu kimwili na kiakili na kujiajiri ni Hulka ya mtu mchapakazi na mwenye uwezo mkubwa kiakili na uthubutu wa kuona na kuzitumia fursa ipasavyo.. PERIOD!!
We mwehu nini unawaona waliojiriwa waoga na wavivu wakati ukianzisha hicho kibiashara chako unataka uajiri watu utaajirije watu unaowaona wavivu pumba kabisa
 
Kuna mkuu amesema kuwa akiajiri watu 6 kwaajiri ya kumuendeshea bajaji atatajirika ila watu wamembishia na wengine wamemuuliza yani utajirike kwa bajaji?

Ngoja tufanye hesabu:

kwasiku bajaji wanapeleka 25 kwaboss, nje ya service na hela ya wao kula 25000 x 6 = 150,000 hivyo kwasiku anakuwa na 150,000

Then 150000 x 30 inakuwa 4,500,000

Kwamwezi boss anakuwa na mil 4 na laki 5 hapa kuna waajiriwa wengi wanasubiri sana kwahuyu mtu......ukisema kunakukamatwa na mambo mengine basi jua wanalipia mambo ya muhimu mapema bajaji inakuwa Safe kufanya kazi.....pia hata bajaji akipiga 40 basi 25 yangu ailete nyumbani bado faida nitapata kubwa tu.....
 
Kujiajiri ni kuzuri kwasababu unajiwekea malengo binafsi ambayo wewe utafanya kazi ili uyatimize.....

ila ukijiajiri ni ngumu kuweza kuwa na kipato huru maana pesa yote itaishia kwenye kula, usafiri na familia.....

yani mshahara wetu kibongobongo nikwaajiri ya kula tu na kulipia makazi ili tufanye kazi ya serikali au maboss tukiwa wazima.....

Pia uwepo wa makato unaumiza sana waajiriwa yani mtu baada ya makato unakuwa na laki 4 tu au laki 5 hapo mwenye biashara ndogo tu kama ya kuuza viatu vya kike anaweza kukufikia na kukupita kwa mapato kiurahisi tu....
 
Mjadala mzuri lakn wachangiaji wako kwenye zile nyuzi zetu pemdwa za ulishwahi kula tunda kimasiara... huku hawana habar nako..
Mjadala mzuri kwako mkuu, huo mwingine ni mzuri kwao ndo maana wako bize nao

Mchango wako kwenye huu uzi ni upi, tunakusubiri
 
Back
Top Bottom