Nakumbuka mwaka wa kwanza tu Kikwete akiwa madarakani ulituambia kuhusu Lowassa na wapi anakolenga. tena kuna wakati ulisisitiza kuwa upo uwezekano Lowassa anajiandaa kuchukua 2010 akiwa bado Waziri mkuu, hatasuibiri tena 2015 likaja swala la yeye kuunda timu yake against Kikwete hata kabla swala la Richmond halijalipuka...
Mkuu wangu Bob,
Heshima mbele, ngoja nijaribu one more time kuuweka ninaouona kuwa ni ukweli wa kinachofanyika sasa hivi, again haya ni maoni yangu binafsi reading the situation:-
1. Inaanzia kwa Malecela, alipokuwa waziri mkuu, sio siri kuwa mzee alianza kampeni toka siku ya kwanza kuutafuta urais, akam-recruit Lowassa kama waziri wa ofisi yake, na kama mtu wake wa karibu ndiye aliyekuwa akifanya kampeni zote, ndio maana na yeye Lowassa alipoingia tu alirudia njia zile zile, za kwenda all the way mpaka chini, Kikwete hakujua haya ndio sasa haelewi cha kufanya maana jamaa yupo kila kona na very strong than ever!
2. Lowassa ana watu watatu wazito kwenye kona yake, yaani mzee wa mbeya, na ra, na sasa amem-recruit na mkapa, mimi mkapa alipokwenda kusemea jimboni kwake tu, nilijua kuwa tayari amejiunga na Lowassa, kujiunga kwa mkapa katika hili kundi kinabadili sura nzima ya this game na kuwapa almost a veto hili kundi na ndio matokeo ya mama Anna Abdallah kupiga kelele sasa baada ya kuwa kimyaa muda mrefu sana, ni kwa nini alikuwa kimyaa na anongea sasa?
(a). Yeye siku zote alikuwa the favored wa mkapa, dakika za mwisho kabla mkapa hajaondoka, alimsaidia big time kwa kupindisha katiba ya CCM na kuwaamuru kuwa mwenyekiti na katibu wa UWT ni lazima waingie bungeni automatically, mama Anna Abdalah ni mwenyekiti wa UWT, nia na madhumuni ya huo ubabe ilikuwa kumpa nafasi huyu mama kuendelea kuwa mbunge, bila kugombea tena, maana alijua kuwa hawezi shinda tena ubunge jimboni.
(b). Wakati hiii inalazimishwa mtandao walikuwa pembeni, hawakutaka hii kitu na waliahidi kuwa siku wakipata urais wataiondoa kabisaa, na huyu mama alikuwa akiwapiga vita sana kwenye cc wasipewe urais, ndio maana mtandao wapopata urais tu kitu cha kwanza kilikuwa kumlipa mumewe kwenye uspika, alipoona haya mama akanywea akawa kimyaa hata kwenye cc au nec akawa haongei tena, akiogopa kuwa watamtoa yeye next, lakini mtandao wakawa bussy kugombea power wakamsahau.
(c). Kwa nini anaongea sasa, ni kwa sababu siku zote yeye ni mtu wa mkapa, wakuu unajua magazeti yetu yanaandika kuhusu nec juzi Dododma, lakini hakuna anayeligusa la effect ya mkapa kuwepo pale Dodoma kwenye nec, ukweli ni kwamba aliletwa na kina Lowassa, kuwepo kwake kulikuwa na nia nyingi sana mojawapo ikiwa ni kuwaogopesha wabunge wanaolilia haki, na pia kumtisha muuungwana kuwa be careful na unachofanya si unajua tuliyoyafanya mimi na wewe mpaka ninakupa urais?
-It worked guys kwa sababu hakuna yoyote aliyekuwa pale mkutanoni aliyeshindwa kuona hili kuwa upande wa pili ulizidiwa na rais alishindwa kuonyesha ujasiri, na the fact kwamba Mwakyembe bado yuko nje ya bunge kwa matibabu kundi la Lowassa wakauchulia huo kama ni ushindi, ndio maana ilibidi mama Kilango ni lazima aje bungeni kuwashitua tena kuwa ngoma bado wakuu,
(d). Mama Anna Abdalah anaongea sasa kwa sababu anajaribu kukishikilia kiti cha UWT, ili aendelee kuwa mbunge, lakini kina mama wameshaamua kuwa sasa basi, Mama Kahama anajitayarisha kuchukua nafasi, na mama anajua kuwa mama Kilango, ni mpigaji mzuri wa kampeni za uchaguzi, na anajua kuwa hana mpango wa kumsaidia, na yeye mama Anna Abdalah hana anythig to gain maana anjua kuwa kama ni ubunge hawezi kuapata tena, kama ni uenyekiti hawezi kupata tena, kwa hiyo alipoombwa na kundi la Lowassa kufanya hii kazi haikuwa taabu kwake kuifanya, kwa kutegemea kuwa watamsaidia kupata uenyekiti wa UWT, ili arudi bungeni ndio hasa maana ya haya makelele baada ya kuwa kimyaaa siku zote!
4. Lowassa na kundi lake sasa hivi wanajitayarisha kugombea urais, bila au with muungwana, wameshafika kwenye ver serious stage na kuna mtu tayari wanamtayarisha, ninaamini kuwa their strategy ni kutomugsa muungwana kwa sasa, ila kumkata asiwe na connection na kila kona na kum-isolate as much as they can ili afike mahali awe peke yake so far wameanza kufanikiwa kwenye hilo, ndio maana sasa hivi muungwana yuko kona yake peke yake na Membe, na siku zote kukimbilia kwa tinga kupata ushauri, huku akiwapa support kwa siri sana kundi la wabunge wanaodai haki, lakini mkutano wa nec ulikuwa very damaging kwa kundi la hawa wabunge, kukosekana kwa Mama Kilango na Mwakyembe, kulionekana dhahiri kuwa ni pigo kubwa sana kwao ingawa Sendeka alijitahidi sana, lakini ukweli ni kwamba they lost!
5. Na ni hiyo momentum kutoka NEC ndiyo imewapa nguvu mpaka kupitisha bajeti, sio siri kuwa sasa hivi tuna serikali ya Lowassa ndani ya serikali yetu ya jamhuri, hawa jamaa ni wakali na ni very rich, na wamerubuni watu wengi sana muhimu, tumebaki sisi wananchi, ukweli ni kwamba kuacha watu wachache sana hapa JF wala sio wote, wananchi hawaelewi kinachoendelea na ndio hasa nguzo muhimu ya hawa jamaa wa Lowassa, ni wananchi wasioelewa anything, media yetu ndio hiyo masikini wa Mungu, hili kundi wako determined, wako arrogant na wanataka power ili waendeleze uhuni wao, they are coming, je kweli wabunge Zitto, Dr.Slaa, Mwakyembe, Mama Kilango, Seleli, na Manyanya watatosha pekee kuwasimamisha lile kundi? Sijui?
6. Spika six, naye sasa yupo kwenye life-support, maana yeye ndiye anayetakiwa next ango'lewe, alikoswa koswa kwenye ishu ya Manji na Mengi, lakini sasa wako nyuma yake wanamtafuta kwa kila njia, sasa wanachohitaji hawa wahuni ni kumnunua Mama Makinda, naibu Spika awape mapungufu ya Six, ili wammalize, akiisha six tu, basi it is over kwa hiyo ukweli ni kwamba pamoja na kwamba sio ukweli mzuri, lakini sasa hivi sisi wananchi tuna tegemeo moja tu nalo ni the devil we know yaani Six? Je ataweza mikiki ya hili kundi la wahuni? Atasimama mpaka mwisho kwa niaba ya sisi wananchi?
Unajua it is a shame kwamba wananchi tumeruhusu it to come down this options, ambazo ukweli ni kwamba ni no options kwetu wananchi, taifa zima hatuwezi ku-hang by thread kwa kumtegemea Spika na looking the record Six anajulikana kwa kubadili mawazo akizidiwa, ndio maana ninasema kuwa hatuna otpions, hapa sasa ni kusali tu na kuendelea kuwapigia makelele mafisadi na kumuomba Mungu atusaidie na hii mikono ya mafisadi, lakini ukweli ni kwamba kuna dalili za kutosha kuwa wananchi tunakaribia kushindwa, kwa sababu the events of this week ni wazi kuwa wananchi hatuwezi kuitegemea sauti moja tu Mama Kilango, we are almost done kama sio tayari!
Mungu Iabriki Tanzania, Tusife Moyo!