Deconstructing Lowassa

Deconstructing Lowassa

Wanabodi,

Mimi sifa zote nam mwagia FMES na hakika mkuu unaona mbali sana...
Nakumbuka mwaka wa kwanza tu Kikwete akiwa madarakani ulituambia kuhusu Lowassa na wapi anakolenga. tena kuna wakati ulisisitiza kuwa upo uwezekano Lowassa anajiandaa kuchukua 2010 akiwa bado Waziri mkuu, hatasuibiri tena 2015 likaja swala la yeye kuunda timu yake against Kikwete hata kabla swala la Richmond halijalipuka...
Nasikitika sana kwamba kuna baadhi ya watu wangu wa karibu ambap walikuwa sana ktk misafara ya Lowassa walijiunga naye...Hawa watu walikuwa wakimng'ong'a Kiwete na ajabu kuna baadhi Kikwete kisha washtukia ama kwa kutojua kawapeleka nje ktk balozi. Lakini bado Kikwete amezungukwa na wanafiki... wanafiki ambao siku moja watamgeuka kama Julius Kaizari..

Lowassa ni mtu hatari sana na bila shaka nadhani hata Mkapa alikuwa akimwogopa Lowassa kuliko Kikwete mwenyewe. Hivi sasa naamini kabisa kuwa Kikwete ni mtu aliyewekwa na watu, ana ubia mkubwa na watu ktkt urais wake laa sivyo hawa watu wasingekuwepo CCM...
Hapa ndipo napompendea marehemu mwalimu Nyerere, watu kama hawa wala wasingepewa nafasi... wangekiona cha moto na pengine kupigwa hata hizo bakora mnazosema kila siku..Hivi kweli rais wa nchi hiii Kikwete akiwapiga bakora watu kama hawa mtasema ni Dikteta!.. Kikwete akiwatia ndani wafisadi wakubwa kama hawa mtasema ni kiongozi mbaya!...
Hili ndio swala ambalo siku zote sikubaliani nalo hata kidogo, watu kama hawa wanatakiwa watumikie Segerea miaka mitano tu inatosha, wakitoka huko watatia akili..

Mkandara kazi ni kwamba does Kikwete think that way ? Aanayaona haya yunayo yasema hapa ? Akisikia hata kwa kuambiwa anaelewa ?
 
Rais hafahamu madaraka aliyopewa kikatiba. Another SI.
 
Kusafisha Tanzania kunahitaji moyo na kunahitaji Mtu ambaye yuko tayari kuwa dictator kwa muda na kutoa maamuzi mazito sana. MAFISADI tulionao tanzania si binadamu ni watu ambao wanatembea wakati wamekufa.

Ukisha kuwa na watu wa mtindo huu huwa ni hatari nafikiri na JK anawaona anawachekea lakini ajue hawa ni marehemu, maamuzi yao huwa yanakuwa na maafa makubwa sana.

Bado nafikiria hivi tutampata wapi rais dikteta, mbaye akiingia madarakani anatoa tiba ya hawa wanaotembea wakati ni wafu?
 
Nakumbuka mwaka wa kwanza tu Kikwete akiwa madarakani ulituambia kuhusu Lowassa na wapi anakolenga. tena kuna wakati ulisisitiza kuwa upo uwezekano Lowassa anajiandaa kuchukua 2010 akiwa bado Waziri mkuu, hatasuibiri tena 2015 likaja swala la yeye kuunda timu yake against Kikwete hata kabla swala la Richmond halijalipuka...

Mkuu wangu Bob,

Heshima mbele, ngoja nijaribu one more time kuuweka ninaouona kuwa ni ukweli wa kinachofanyika sasa hivi, again haya ni maoni yangu binafsi reading the situation:-

1. Inaanzia kwa Malecela, alipokuwa waziri mkuu, sio siri kuwa mzee alianza kampeni toka siku ya kwanza kuutafuta urais, akam-recruit Lowassa kama waziri wa ofisi yake, na kama mtu wake wa karibu ndiye aliyekuwa akifanya kampeni zote, ndio maana na yeye Lowassa alipoingia tu alirudia njia zile zile, za kwenda all the way mpaka chini, Kikwete hakujua haya ndio sasa haelewi cha kufanya maana jamaa yupo kila kona na very strong than ever!

2. Lowassa ana watu watatu wazito kwenye kona yake, yaani mzee wa mbeya, na ra, na sasa amem-recruit na mkapa, mimi mkapa alipokwenda kusemea jimboni kwake tu, nilijua kuwa tayari amejiunga na Lowassa, kujiunga kwa mkapa katika hili kundi kinabadili sura nzima ya this game na kuwapa almost a veto hili kundi na ndio matokeo ya mama Anna Abdallah kupiga kelele sasa baada ya kuwa kimyaa muda mrefu sana, ni kwa nini alikuwa kimyaa na anongea sasa?

(a). Yeye siku zote alikuwa the favored wa mkapa, dakika za mwisho kabla mkapa hajaondoka, alimsaidia big time kwa kupindisha katiba ya CCM na kuwaamuru kuwa mwenyekiti na katibu wa UWT ni lazima waingie bungeni automatically, mama Anna Abdalah ni mwenyekiti wa UWT, nia na madhumuni ya huo ubabe ilikuwa kumpa nafasi huyu mama kuendelea kuwa mbunge, bila kugombea tena, maana alijua kuwa hawezi shinda tena ubunge jimboni.

(b). Wakati hiii inalazimishwa mtandao walikuwa pembeni, hawakutaka hii kitu na waliahidi kuwa siku wakipata urais wataiondoa kabisaa, na huyu mama alikuwa akiwapiga vita sana kwenye cc wasipewe urais, ndio maana mtandao wapopata urais tu kitu cha kwanza kilikuwa kumlipa mumewe kwenye uspika, alipoona haya mama akanywea akawa kimyaa hata kwenye cc au nec akawa haongei tena, akiogopa kuwa watamtoa yeye next, lakini mtandao wakawa bussy kugombea power wakamsahau.

(c). Kwa nini anaongea sasa, ni kwa sababu siku zote yeye ni mtu wa mkapa, wakuu unajua magazeti yetu yanaandika kuhusu nec juzi Dododma, lakini hakuna anayeligusa la effect ya mkapa kuwepo pale Dodoma kwenye nec, ukweli ni kwamba aliletwa na kina Lowassa, kuwepo kwake kulikuwa na nia nyingi sana mojawapo ikiwa ni kuwaogopesha wabunge wanaolilia haki, na pia kumtisha muuungwana kuwa be careful na unachofanya si unajua tuliyoyafanya mimi na wewe mpaka ninakupa urais?

-It worked guys kwa sababu hakuna yoyote aliyekuwa pale mkutanoni aliyeshindwa kuona hili kuwa upande wa pili ulizidiwa na rais alishindwa kuonyesha ujasiri, na the fact kwamba Mwakyembe bado yuko nje ya bunge kwa matibabu kundi la Lowassa wakauchulia huo kama ni ushindi, ndio maana ilibidi mama Kilango ni lazima aje bungeni kuwashitua tena kuwa ngoma bado wakuu,

(d). Mama Anna Abdalah anaongea sasa kwa sababu anajaribu kukishikilia kiti cha UWT, ili aendelee kuwa mbunge, lakini kina mama wameshaamua kuwa sasa basi, Mama Kahama anajitayarisha kuchukua nafasi, na mama anajua kuwa mama Kilango, ni mpigaji mzuri wa kampeni za uchaguzi, na anajua kuwa hana mpango wa kumsaidia, na yeye mama Anna Abdalah hana anythig to gain maana anjua kuwa kama ni ubunge hawezi kuapata tena, kama ni uenyekiti hawezi kupata tena, kwa hiyo alipoombwa na kundi la Lowassa kufanya hii kazi haikuwa taabu kwake kuifanya, kwa kutegemea kuwa watamsaidia kupata uenyekiti wa UWT, ili arudi bungeni ndio hasa maana ya haya makelele baada ya kuwa kimyaaa siku zote!

4. Lowassa na kundi lake sasa hivi wanajitayarisha kugombea urais, bila au with muungwana, wameshafika kwenye ver serious stage na kuna mtu tayari wanamtayarisha, ninaamini kuwa their strategy ni kutomugsa muungwana kwa sasa, ila kumkata asiwe na connection na kila kona na kum-isolate as much as they can ili afike mahali awe peke yake so far wameanza kufanikiwa kwenye hilo, ndio maana sasa hivi muungwana yuko kona yake peke yake na Membe, na siku zote kukimbilia kwa tinga kupata ushauri, huku akiwapa support kwa siri sana kundi la wabunge wanaodai haki, lakini mkutano wa nec ulikuwa very damaging kwa kundi la hawa wabunge, kukosekana kwa Mama Kilango na Mwakyembe, kulionekana dhahiri kuwa ni pigo kubwa sana kwao ingawa Sendeka alijitahidi sana, lakini ukweli ni kwamba they lost!

5. Na ni hiyo momentum kutoka NEC ndiyo imewapa nguvu mpaka kupitisha bajeti, sio siri kuwa sasa hivi tuna serikali ya Lowassa ndani ya serikali yetu ya jamhuri, hawa jamaa ni wakali na ni very rich, na wamerubuni watu wengi sana muhimu, tumebaki sisi wananchi, ukweli ni kwamba kuacha watu wachache sana hapa JF wala sio wote, wananchi hawaelewi kinachoendelea na ndio hasa nguzo muhimu ya hawa jamaa wa Lowassa, ni wananchi wasioelewa anything, media yetu ndio hiyo masikini wa Mungu, hili kundi wako determined, wako arrogant na wanataka power ili waendeleze uhuni wao, they are coming, je kweli wabunge Zitto, Dr.Slaa, Mwakyembe, Mama Kilango, Seleli, na Manyanya watatosha pekee kuwasimamisha lile kundi? Sijui?

6. Spika six, naye sasa yupo kwenye life-support, maana yeye ndiye anayetakiwa next ango'lewe, alikoswa koswa kwenye ishu ya Manji na Mengi, lakini sasa wako nyuma yake wanamtafuta kwa kila njia, sasa wanachohitaji hawa wahuni ni kumnunua Mama Makinda, naibu Spika awape mapungufu ya Six, ili wammalize, akiisha six tu, basi it is over kwa hiyo ukweli ni kwamba pamoja na kwamba sio ukweli mzuri, lakini sasa hivi sisi wananchi tuna tegemeo moja tu nalo ni the devil we know yaani Six? Je ataweza mikiki ya hili kundi la wahuni? Atasimama mpaka mwisho kwa niaba ya sisi wananchi?

Unajua it is a shame kwamba wananchi tumeruhusu it to come down this options, ambazo ukweli ni kwamba ni no options kwetu wananchi, taifa zima hatuwezi ku-hang by thread kwa kumtegemea Spika na looking the record Six anajulikana kwa kubadili mawazo akizidiwa, ndio maana ninasema kuwa hatuna otpions, hapa sasa ni kusali tu na kuendelea kuwapigia makelele mafisadi na kumuomba Mungu atusaidie na hii mikono ya mafisadi, lakini ukweli ni kwamba kuna dalili za kutosha kuwa wananchi tunakaribia kushindwa, kwa sababu the events of this week ni wazi kuwa wananchi hatuwezi kuitegemea sauti moja tu Mama Kilango, we are almost done kama sio tayari!

Mungu Iabriki Tanzania, Tusife Moyo!
 
Mkuu wangu Bob,

je kweli wabunge Zitto, Dr.Slaa, Mwakyembe, Mama Kilango, Seleli, na Manyanya, watatosha pekee kuwasimamisha lile kundi? Sijui?

Spika six

Mungu Iabriki Tanzania, Tusife Moyo!

Mkuu ubarikiwe, tumeelewa kinachoendelea hila wasikate tamaa kazi ni ngumu sana kuliko hata South Africa wakati wanapambana na makaburu. yanahitajika mawazo na strategy mpya.
 
Field Marshall es,
Mkuu nakuamini sana maneno yako.. nakumbuka ule usemi - An ear to the ground (science of ordinary mortals)...tunahitaji watu kama wewe kabla hatujachelewa.
Inatisha mkuu, inatisha sana na sijui kama Kikwete anayaona haya.. msemo wa Lunyungu!
 
The task of deconstructing Lowassa does not end with Lowassa himself, it involves everyone who is his ally, supporter and sympathiser.

I am pretty much convinced by 99% that Lowassa in one way or another he has been involved directly or indirectly in most of Ufisadi issues.

From IPTL, Valhambia, EPA and Richmond, there is an individual or two who are closely related to EL in some sort of way.

Even though we may not have substantial evidence due to corruption and his team strong arm tactics, it is safe to say that Lowassa does not represent Maslahi ya Wananchi, he is an agent if not the key person for Mafisadi na Wahujumu.

His political tactics to undermine the President and the Speaker are known. He has managed to infilitrate the key people at TISS who have pledge allegience to him and not the President who is Commonder in Chief of our Armed forces.

I recall a statement from one of JK handlers and support staff who lamented the nomination of EL as Prime Minister and the talk of power struglle from day one of his premiership.

One of the best thing ever to happen to CCM was not to appoint Lowassa as Makamu Mwenyekiti. Even though he missed that opportunity, I will not be surprised if his camp will push for Lowassa to replace Makamba as Secretary General.

On this journey to Deconstruct Lowassa, I am inviting everyone to uproot every story that they know of what Lowassa has done. From his day at UDSM, AICC, Deputy to Sokoine and many other places.

We need to expose this infidel, who is egomaniac and self centered.
 
Mkuu maneno yako yana uzito unaostahili lakini Mungu si wa kuchezewa. Kuna mtu ninayemwamini sana, siku moja kabla ya Lowassa kujiuzulu, nilimwambia Lowassa lazima ang'oke, akaniambia maneno kama yako kwamba ana pesa, watu na nguvu kubwa na hakuna wa kumgusa hadi awe RAIS. Leo hii hata yeye haamini kilichotokea. Ili Lowassa awe rais inabidi yatokee yanayotokea Zimbabwe sasa ama yaliyotokea Kenya (jambo ambalo sitoshangaa) maana wananchi wa Tanzania wa sasa hata huko vijijini wamemuelewa vyema na hatopita. Hata wanaomtetea ni watu kama Serukamba ambaye kwa mila zatu za Kiafrika, namuombea Mungu amuondolee tatizo alilobalo na kuomba Mungu atuepusha vijana wetu wa kiume tulionao wasiangukie katika balaa alilonalo. Siwezi kumsema vibaya maana bado tuna vizazi.

Mkuu si useme tu kama jongoo halipandi mtungi.....
 
Ndugu FMES,
Hiyo makala yako ya juu naomba tuianzishie kichwa chake peke yake na kiwe UKWELI JUU YA LOWASSA. Pia ikiwezekana basi na tufanye CHAIN LETER na kila atakayesoma basi na aiutume kwa watu wote anaowafahamu. Nafikiri itasaidia kupeleka ujumbe kwa watu wengi kujua nini kinatokea. Nilishawahi kusikia jinsi hawa jamaa walivyokuwa madarakani kabla Mkapa hajaondoka. Kumbe kweli hii kitu. Sasa najua kwa nini Kikwete ananywea. Ila kama Mahakama na Polisi na Jeshi na UWT nk viko chini yake bado, si AWAKOLIMBE tu hasa wale VINARA? Ama kweli kazi ipo. Kwa maana hii naomba idhini kabisa kuanza kuituma hii makala kwa jamaa zango wote wajue kinachoendela maana TAIFA inabidi liokolewe kwa udi na Uvumba...
 
Mkuu haina noma shukrani kwamba hata wewe umekubali kuwa ni ukweli kuhusu taifa letu, ila kama nilivyosema ni maoni yangu tu kwa kuangalia kinachoendelea, unaweza kuituma anywhere,

Ingawa nitaitoa hivi kairbuni wiht more ishus kwenye gazeti moja nchini, hapo nimeitoa in the form of Raw tu, na haraka haraka!.

Ahsante Mkuu
 
On this journey to Deconstruct Lowassa, I am inviting everyone to uproot every story that they know of what Lowassa has done. From his day at UDSM, AICC, Deputy to Sokoine and many other places.

We need to expose this infidel, who is egomaniac and self centered.

Maneno mazito sana haya mkuu, I am down!
 
Kama ni hivyo basi ni vema kusubiri. Ningeliomba tu iwe katika Kiswahili na Kiingereza. Wengi Tanzania vijijini hawajui hiyo lugha. Pana wakati Fundi Mchundo alisema ni lugha gani CCM wanatumia vijijini na Wapinzani wanatumia ipi. Ukienda kijijini a kumwaga Kiingereza na/au hapo unaelezea BoT, EPA, kubadilisha majina hotel ili wapsilipe kodi, hotel ya Serengeti nk kwa kweli watakuona kituko. Lakini hamna haja ya kukata tamaa. Tutakuwa tunawaandikia hadi vijijini jamaa wabadilike. Haya, macho yanawasha kusubiri hiyo FULL WARAKA.
 
Maneno mazito sana haya mkuu, I am down!

Nauungana nawe kwa hili pia .Hii ni vita wao wanapugania kule sisi huku kwa njia nyingine .Ni muda muafaka huu jamani .Ndiyo maana JF tuko .Ila wewe ES hujasema nani nakununuliwa hapa JF na Upinzani .Sambamba to your call naomba na wewe tumwagie maana tuweze kuokoa jamii kubwa na hata Wapinzani wajielewe kwamba tuna wamulika .
 
Lunyungu,

Wewe unanijua mkuu mimi hueka chambo, na watu wenye kutaka ukweli kutafuta na hawajawahi kukuta uongo, hebu zilalie macho hizi utakuja kiniambia ukweli ulipo!

Zitafute mkuu, zipo hizi tena iso siri tena!
 
Najua ziko na nimesha mtaja mmoja ni John Cheyo .Wengine sijapata hebu nipe basi hata kwa PM kama hapa huwezi kumwaga .Mgombea wa wao akina Lowasa ni Masha .
 
FMES,
Tangu nisome makala yako jana imenipa kutafakari mambo mengi sana. Nafikiri tusikate tamaa kiasi hicho. Tegemeo letu limebaki moja yaani KARATA ya Mwisho. Hii nafikiri anayo Kikwete. Sasa inategemea Kikwete ataicheza wakati gani. Hii imenikumbusha ile story ya THE GODFATHER. Mzee Don Carleon alikuwa kaishiwakabisa nguvu. Hata jamaa zake wengine walikuwa wamenunuliwa na wapinzani wake. Siku ya MAZISHI ya SANTINO mwanae au SONNY ndipo alipofanya maajabu (Samahani kama ntakuwa nimechanganya). Wakati mazishi yakifanyika, watu wake walikuwa BUSSY waki-eliminate adui zake wote. Mazishi yanaenda, baba yuko KAZINI kwa sana!! Sasa inategemea Kikwete ana akili kiasi gani. Kama HANA AKILI basi kweli TUMEKWISHA. Kama kama wanamu-underestimate basi inabidi tuseme SOON UFISADI UTAISHA maana wameshajiweka wao wote kwenye KAPU MOJA. Nasema hivi kwa sababu moja kubwa sana. Mlisema kuwa yule BOSS Othman nani sijui ni Mpelelezi na ni RAFIKI WA KIKWETE. Hosea kapanda na hivyo aliyekuja ni mtu wa Kikwete na atakuwa kazini kukusanya DATAs. Riport zote za uchunguzi wa UFISADI ziko kwake. Wauza unga ziko kwake nk nk. Anaweza subiri LAST MINUTE akacheza ule mchezo walimfanyia Boss wa Fat yaani RAGE kule Tabora. Walimuweka ndani na sasa imeonekana HANA HATIA ila ubunge hana wala KITI hana. Nafikiri Muungwana kwa kutumia hizo riport zote anaweza KIHAKI na KISHERIA kuwakamata na kuwafungulia mashitaka Mamvi, ANBEN, Dialo. Mramba, Msabaha, R Azziz, Chenge, Mwanyika, Mamvi Son, nk nk.
KIKWETE KAZI KWAKO. UKIFANYA MCHEZO JAMAA WATAKUMALIZA. Siye tuko na wewe maana BETTER THE DEVIL YOU KNOW, ingawa huyu shetani FISADI, mhhh hadi unasema labda nijaribu mwingine...
 
The task of deconstructing Lowassa does not end with Lowassa himself, it involves everyone who is his ally, supporter and sympathiser.

I am pretty much convinced by 99% that Lowassa in one way or another he has been involved directly or indirectly in most of Ufisadi issues.

From IPTL, Valhambia, EPA and Richmond, there is an individual or two who are closely related to EL in some sort of way.

Even though we may not have substantial evidence due to corruption and his team strong arm tactics, it is safe to say that Lowassa does not represent Maslahi ya Wananchi, he is an agent if not the key person for Mafisadi na Wahujumu.

His political tactics to undermine the President and the Speaker are known. He has managed to infilitrate the key people at TISS who have pledge allegience to him and not the President who is Commonder in Chief of our Armed forces.

I recall a statement from one of JK handlers and support staff who lamented the nomination of EL as Prime Minister and the talk of power struglle from day one of his premiership.

One of the best thing ever to happen to CCM was not to appoint Lowassa as Makamu Mwenyekiti. Even though he missed that opportunity, I will not be surprised if his camp will push for Lowassa to replace Makamba as Secretary General.

On this journey to Deconstruct Lowassa, I am inviting everyone to uproot every story that they know of what Lowassa has done. From his day at UDSM, AICC, Deputy to Sokoine and many other places.

We need to expose this infidel, who is egomaniac and self centered.

Shame on us guys, all this comes just because of what happenned at the NEC/Wabunge meeting. I thought JF is a place where people can accept facts when presented to them, and not just a place to argue for the sake of our own interest.

I was reading Ansbert Ngurumo on the weekend, one thing that i took away from that article was how we were all forced to believe that EL is this 'fuckin monster fisadi' within CCM, and if removed from power, all will go well. He went on to say, unfortunately that did not happen, we have more problems within oursleves than Lowassa.

With all due respect REV, this is no a battleground for curse words, rather a battleground for ideas, facts & constructive arguments to build our country, we all love our country dearly, and we should make sure JF remains that way.

EL have made mistakes as a leader, because he was not afraid to make decisons, but he has achieved sooo much as well with the same style. On the mistakes, lets use some facts to judge, otherwise, its a big injustice.

I respect so much EL for what he has done to this country, lets judge him on that and thank him. Lets challenge our current leaders to do better than what he has done.
 
With all the good presentation, you screwed up by cursing. Karibu Kaka we need those who will oppose the motion!
 
With all due respect REV, this is no a battleground for curse words, rather a battleground for ideas, facts & constructive arguments to build our country, we all love our country dearly, and we should make sure JF remains that way.

EL have made mistakes as a leader, because he was not afraid to make decisons, but he has achieved sooo much as well with the same style. On the mistakes, lets use some facts to judge, otherwise, its a big injustice.

I respect so much EL for what he has done to this country, lets judge him on that and thank him. Lets challenge our current leaders to do better than what he has done.

KGB,

Since you have decided to stand tall and defend EL, list down 15 of his accomplishments for all his service for Tanzania!
 
Edward Lowassa is a dead horse. Beating up on him is a waste of cerebral resources.
 
Back
Top Bottom