DED/DEO Magu watoto wako hatarini Magu Shule ya Msingi

DED/DEO Magu watoto wako hatarini Magu Shule ya Msingi

Hao Uliowataja Bado Wapo Kwenye Vyeo Vyao
Hawajaachia Ngazi
 
Duuu mmejipanga aisee, wasiwasi wangu ni hii njia mnayotumia.
DED, DEO Msingi na watendaji wengine mnaohusika na Idara ya Elimu hapo wilayani Magu; fuatilieni kwa karibu utendaji wa huyo Mwalimu Mkuu Magu S/Msingi mkizingatia historia ya matukio ya ovyo aliyoyafanya shule alizotoka (Nyanguge na Nyambitilwa) kabla hamjamhamishia Magu S/Msingi.
Kwa nini hamwavui madaraka watu wazembe na wenye uwezo hafifu wa kiuongozi kama huyo Mwalimu?
Mbona kuna walimu wengi sana tens wenye Stashahada na Shahada ambao hamwapi madaraka, badala yake mnaendelea kukumbatia walimu wakuu wasiokuwa na sifa, tena wazembe na wakorofi kama huyo?
Mtasema mnasubiri STD VII wamalize mitihani ndio mmwondoe huyo mwalimu!! Kwani sasa hivi anafanya nini cha maana shuleni hapo zaidi ya kuwavuruga waalimu, wanafunzi na wazazi?
Hana ushirikiano na waalimu wake; mizozo isiyoisha kwa sababu ya ubabe na kutokutaka kushauriwa; lugha chafu kwa waalimu na wazazi na kuwanyanyasa wanafunzi.
Mchanga na kokoto kwa ajili ya ujenzi wa hilo jengo jipya vimesombwa na watoto kwa kuokoteza mitaani, hata kuiba kwenye saiti za watu na shule jirani ya Nyalikungu! Hilo jengo mbona limechangiwa fedha na wazazi?
Bado amewabebesha watoto maji mpaka mtoto wa STD I amegongwa na pikipiki akivuka barabara kwenda lamboni na hatujui nini majaaliwa ya mtoto huyo!
BADO mwalimu huyo anadiriki kutamka ndani ya Staff Room kwamba yeye hajali kuandikwa kwenye Facebook; anasema AFADHALI mtoto huyo angekufa kabisa ili aandikwe vizuri!
Jamani! Ninyi mnaona huyu mama ni wa kawaida?
Nijuavyo mimi, akinamama wana huruma kuliko wakinababa; yeye huyu vipi?
Unawezaje kumtakia mtoto asiye na hatia AFADHALI YA KUFA, ili uandikwe vizuri kwenye Facebook?
Hata kuta zina masikio; usitamke jambo baya dhidi ya mtu ukiamini eti hatalisikia! Ni suala la muda tu.
DED na DEO Msingi Magu, mvueni madaraka huyo mama; hafai kuwa Mwalimu Mkuu.
Watoto wa STD VII Magu S/Msingi hawataathirika kimasomo kwa kuondolewa ukuu wa shule huyo mama; mimi naamini, badala yake watoto watanufaika maana waalimu watapata morale ya kufanya kazi vizuri zaidi, maana watapata nafasi ya kupanga mipango yao vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa walivyokabwa koo!
MSIPOJALI MADOGO, NA MAKUBWA MTAACHA. Tchao.
 
Kiujumla kuwa mkaazi au mtumishi ktk wilaya hii ya magu nikama laana vile, navionea wivu vijiji vitakavyotengwa kuwa ndani ya wilaya ya kisesa, au sanjo, au isangijo, sijajua itapewa jina gani hii wilaya mpya ambayo
Mh magufuri kawaahidi wana kisesa,
Maana magu hata umpeleke Dr au pr . Hamna kitu, hata magufuri ataiacha km ilivyo.
We jiulize kunajengo la makao makuu ya wilaya mpaka sasa miaka 7 limekwama, sio rais wala waziri mkuu au makamu wa rais analizungumzia , nalipo njiani.
Huduma zte ni mbovu, wabunge wanaopitishwa mpk unasema hivi hakuna watu ndani ya wilaya na jimbo hilo?
Magu imewahi kutoa mpaka manaibu waziri wa fedha lakini hamna kitu.

Tunamshukuru magufuri kuikata magu , ili wanamagu waumizane wenyewe ni moja ya wilaya ambazo hazifai hii nchi .
Kisesa ikipewa wilaya, itawaka sana, wadau na wana jf nitaftieni kiwanja cha 2ml. Ukipata ni pm, ila kiwe maeneo ya kisesa na viunga vyake, pembezoni mwa barabara.
 
Taarifa nzuri sana.Huu uwanja haushindwi kwa lolote hili litaisha kwa muda mfupi.
Huwa natafakari sana, "kwa nini mtu anashindwa kuwajibika mpaka asukumwe sukumwe?" Why? Mtu anakuwa so disorganized. Kufanya kazi na watu wa design hii ni ngumu sana. Halafu mara nyingi ni wabishi mnoo!
 
Umenena vema Hagwila; DED na DEO Msingi Magu, wafanye uchunguzi wa hayo majongolito ya mwalimu huyo ambaye yuko chini yao. Shule ipo, waalimu wapo, wanafunzi wapo na wazazi wapo; ukweli utathibitika tu.
Na kama itashindikana, TAKUKURU iingie kazini, full stop!! Msilete mchezo hapa!!
 
Back
Top Bottom