DED, DEO Msingi na watendaji wengine mnaohusika na Idara ya Elimu hapo wilayani Magu; fuatilieni kwa karibu utendaji wa huyo Mwalimu Mkuu Magu S/Msingi mkizingatia historia ya matukio ya ovyo aliyoyafanya shule alizotoka (Nyanguge na Nyambitilwa) kabla hamjamhamishia Magu S/Msingi.
Kwa nini hamwavui madaraka watu wazembe na wenye uwezo hafifu wa kiuongozi kama huyo Mwalimu?
Mbona kuna walimu wengi sana tens wenye Stashahada na Shahada ambao hamwapi madaraka, badala yake mnaendelea kukumbatia walimu wakuu wasiokuwa na sifa, tena wazembe na wakorofi kama huyo?
Mtasema mnasubiri STD VII wamalize mitihani ndio mmwondoe huyo mwalimu!! Kwani sasa hivi anafanya nini cha maana shuleni hapo zaidi ya kuwavuruga waalimu, wanafunzi na wazazi?
Hana ushirikiano na waalimu wake; mizozo isiyoisha kwa sababu ya ubabe na kutokutaka kushauriwa; lugha chafu kwa waalimu na wazazi na kuwanyanyasa wanafunzi.
Mchanga na kokoto kwa ajili ya ujenzi wa hilo jengo jipya vimesombwa na watoto kwa kuokoteza mitaani, hata kuiba kwenye saiti za watu na shule jirani ya Nyalikungu! Hilo jengo mbona limechangiwa fedha na wazazi?
Bado amewabebesha watoto maji mpaka mtoto wa STD I amegongwa na pikipiki akivuka barabara kwenda lamboni na hatujui nini majaaliwa ya mtoto huyo!
BADO mwalimu huyo anadiriki kutamka ndani ya Staff Room kwamba yeye hajali kuandikwa kwenye Facebook; anasema AFADHALI mtoto huyo angekufa kabisa ili aandikwe vizuri!
Jamani! Ninyi mnaona huyu mama ni wa kawaida?
Nijuavyo mimi, akinamama wana huruma kuliko wakinababa; yeye huyu vipi?
Unawezaje kumtakia mtoto asiye na hatia AFADHALI YA KUFA, ili uandikwe vizuri kwenye Facebook?
Hata kuta zina masikio; usitamke jambo baya dhidi ya mtu ukiamini eti hatalisikia! Ni suala la muda tu.
DED na DEO Msingi Magu, mvueni madaraka huyo mama; hafai kuwa Mwalimu Mkuu.
Watoto wa STD VII Magu S/Msingi hawataathirika kimasomo kwa kuondolewa ukuu wa shule huyo mama; mimi naamini, badala yake watoto watanufaika maana waalimu watapata morale ya kufanya kazi vizuri zaidi, maana watapata nafasi ya kupanga mipango yao vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa walivyokabwa koo!
MSIPOJALI MADOGO, NA MAKUBWA MTAACHA. Tchao.