emmanueljohnson76
New Member
- Jun 27, 2013
- 2
- 0
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyeusi ni nyeusi tu, ukiita nyeupe ni uongo; lakini ukiwa mnafiki unaweza kufanya hivyo ili kujifariji, lakini wenye kutambua mambo watang'amua.Yaani hapa hata kama ni mtoto mdogo unaelewa tu kuwa huyo afisa anayesifiwa lazima yuko nyuma ya pazia katika kuandika habari hii.
Yaani wewe mmoja tu uwe msafi kuliko wote hao umekuwa Mungu?
Acheni kuchafua wenzenu kwenye mitandao ya kijamii.
Taratibu za kiutumishi ziko wazi.
Wewe unauona Uratibu ni mdogo? Posho ya 250,000/= kila mwezi nje ya mshahara, pikipiki mpya na fuel allowance (sijui kiasi gani); watu wenye roho za korosho wanaumia!!Uongo! Uratibu milion kwa kipi? Mbn uratibu hauna mafungu yoyote? TUHUMA ZA KUPIKA
Hivi inawezakana kweli hao wazee uliowataja hapo juu hawayajui haya? Labda....!!DSO,
Pccb
shughulikia hilo.
Hakuna mtu aliye nyuma ya pazia; malalamiko haya nimeyatoa mimi binafsi kutokana na historia ya mambo yanayoendelea kwenye ofisi ya DEO Magu tangu enzi za Salyankanga kabla hata huyu Afisa aliyehamishiwa Misungwi na Glory hawajaletwa Magu.Yaani hapa hata kama ni mtoto mdogo unaelewa tu kuwa huyo afisa anayesifiwa lazima yuko nyuma ya pazia katika kuandika habari hii.
Yaani wewe mmoja tu uwe msafi kuliko wote hao umekuwa Mungu?
Acheni kuchafua wenzenu kwenye mitandao ya kijamii.
Taratibu za kiutumishi ziko wazi.
Mkuu kandukamo1; hawa watu wanakera sana; lakini ni heri kusema kuliko kunyamaza. Kama wanaendelea kukupa majibu yao ya hovyo hovyo, weka mambo hadharani kila mtu aone u.pumba.vu wao; anaweza kutokea mkombozi.Likewise nipo wilaya hii na nina malalamiko yangu ambayo majibu nipewayo ni ya hovyo sana. Hawa wa.pumba.vu aliowataja ukiwa confront kwa hoja wanaona kama unawaonea kisa ni wanawake.
Hao ndio tunaowatafuta hivi kwa nini watu wanapenda kuisingizia idara kuficha maovu?Hata Geita DC imewaka moto matokeo ya Std VII 2019 kimkoa imeshika nafasi ya mwisho kutokana na DEO Said kuwavuruga walimu wakuu na kuwapoka madaraka. Rushwa ya ngono na kuwapa cheo walimu wakuu kwa M.1 kwake kawaida.
Mbaya zaidi kwenye kikao cha wenyeviti wa walimu wakuu kilichofanyika Dodoma alimuacha Mwenyekiti aliochaguliwa na walimu wakuu na kumpeleka Rafiki yake Mkuu kutoka katoro.
Kwa hiyo walimu wamekufa moyo wa ufundishaji. Jamaa anajiita yeye ni Afisa usalama. Serikali kazi kwenu.
Takukuru changamkeni.
Halmashauri gani?Samahani kwa kudandia mada. Jana kuna walimu walikuja ofisini kwangu nikawasikia wakilalamika eti kwenye halmashauri yao kuna maofisa baadhi wameenda wao kusimamia mtihani wa kidato cha nne badala ya kuteua walimu ambao wako shule kila siku. Hii nayo imekaaje?
Mkuu namba force huyo anayesema majungu kazini hajui asemalo. Huyo Salyankanga alikuwa DEO wa hovyo sana aliyedidimiza kabisa morali ya waalimu wengi kwa sababu ya rushwa. Mawakala wake hapo ofisini walikuwa ni haohao wakina Johari, Prisca na kakijana kanaitwa Buhatwa ni kakiraka hapo vifaa na takwimu. Salyankanga hakuwa na aibu ya kuomba rushwa; alikuwa radhi kumgandamiza mwalimu mwenye elimu na uwezo, anayestahili madaraka kisa hajatoa rushwa, ama ya pesa ama ya ngono kama ni mwanamke.Acha watu wazungumze kama ni majungu pita hivi
Asante sana mkuu andaskooHagwila.
Nakupongeza kwa kuamua kuliweka wazi hili na inaonesha wazi upo well detailed, wahusika wakipita hapa au hata wakihitaji msaada wako “piyemu” bila shaka utawapa ushirikiano wa kutosha.... concern yangu ni huyo mbunge ambaye naona unamtaja kwa kurudiarudia kuonesha una imani naye.
Huyu mbunge wenu (Kiswaga) mbona ni kilaza mzuri tu zaidi ya umaarufu wa kibiashara na ku-take advantage ya raia wa “ndoho tabu”, japo hoja yako ni ya msingi sana na binafsi natamani kuona hiyo network ya kina Johari ikiwa overhauled.... pengine mwandikie ujumbe DED moja kwa moja au hata Jafo kwa njia ambayo ujumbe utawafikia.
OpHayajakukuta ndugu yangu; siku utakayonyanyasika kisawasawa utaelewa, japo sikuombei. Fikiria, una vigezo vyote vya kukustahilisha kupata nafasi au huduma fulani; badala ya kupewa hiyo nafasi au huduma, unaambiwa toa laki 3 hadi 5 ndipo upate hiyo nafasi au rushwa ya ngono (kwa wanawake). Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
Nimemtetea nani?Hakuna lolote ni fitina tu na roho mbaya inakusumbua. Unaemtetea mwenyewe hana lolote analolijua zaidi ya kuendeleza tabia za mzee saryankanga